Kuna haja ya kumblock ex wako? - RAHA ZA KITANDANI

Kuna haja ya kumblock ex wako?


Kuendelea kuwa na urafiki kwenye mitandao ya kijamii na mpenzi wako wa zamani (ex wako) ni sawa na kutaka kujua yanayoendelea kwa jirani ambaye huongei nae.
Upo msemo usemao, ‘Absence makes the heart grow fonder’ ukimaanisha kutokuweo kwa mtu huufanya moyo kumpenda zaidi. Na ukweli wa mambo ni kwamba, si mara zote kumblock ex wako kutakufanya umchukie, wakati mwingine waweza jikuta unampenda zaidi kutokana na kumkosa kama msemo unavosema.
Watu wengi huchukulia suala la kumblock ex kama jambo la kawaida na lenye manufaa sababu linasaidia kuedelea na maisha mengie kirahisi na kuepukana na jambo lolote linaloweza kumfanya ajikute anarudi katika mahusiano ambayo ameona hayana manufaa kwake.