ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI - RAHA ZA KITANDANI

ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI


Karibuni tena Wapendwa  2zungumzie mambo tofauti ktk maisha ya mwanaadam. Ni mara nyingine tena 2nakutana 2kizungumzia kuhusu Adhabu kubwa ya mpenzi anayekusaliti ktk mapenzi. endelea ... 

Wanaume wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti, hutunisha misuli kwa kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa wana mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.
 Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno haya: “mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Mikosi Gesti” au “vipi yule bwege alikuuliza jana ulipochelewa kurudi”.  Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.
 Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume au mke. Watu huazimana magari au pesa, lakini laazizi hakuna jasiri wa namna hiyo! Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo,  kesho yake watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.
 Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.
 Ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
 Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume’ mwingine kwa maeneo  fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti.