MABISHANO YA VIUNGO - RAHA ZA KITANDANI

MABISHANO YA VIUNGO


Siku moja viungo vilibishana baada ya kuchoka kutegeana kufanya kazi ya kuutumikia mwili. Kila kiungo kilijitapa kuwa bora kuliko chengine. Mdomo ulianza kwa kusema mimi ni bora kuliko nyinyi nyote. Kwa sababu mimi ndie ninaeweza kutamka maneno, nikasema, mkapata chakula na kuweza kunufaika.Pia kama si mimi chakula hakiwezi kupita mwilini na hivyo basi mwili mzima utashindwa kufanya kazi. Macho yakasema kumwambia mdomo; ``Wewe huwezi kuishi bila kula lakini mimi naweza. 
Pia nikiwa mimi sifanyi kazi mwili hauwezi kuona yanayotokea na wala kuona kitu kizuri wala kibaya. Hata chakula huwezi kukiona kama si mimi. Kusikia hivyo masikio yakasema; ``Mimi ndio hasa ninasikiliza kila kitu na kuupa mwili ujumbe. Wakati mwengine wewe macho unaweza kuona kitu lakini wakati mwengine inawezekana huwezi kuona kitu kinachokuja hivyo ni rahisi kuuhatarisha usalama wa mwili. 
Kubwa zaidi mimi nakusaidia wewe mdomo kujua nini useme unapozungumza sambamba na kuufanya mwili nzima uweze kusimama vizuri bila kuyumba. Kusikia hivyo mdomo ukanyamza kimya lakini mara pua ikadaka. 
Pua ikaanza kwa kujisifu. Mimi ndio hasa naweza kuusaidia mwili kusikia harufu nzuri au mbaya. Kwa mfano mdomo hauwezi kuhisi kuwa chakula kinanuka aua kumechacha bila mimi kunusa chakula hicho. Mikono nayo ikaja juu kwa kusema; mimi ndio ninatafuta kila kitu na kukipeleka kwenu. 
Chakula hakiendi mdomoni bila mimi kukichukuwa na kukiweka huko. Wakati mwengine masikio yanaingia wadudu au kupata uwasho. Mimi ndio nasaidia kuondoa matatizo hayo. Hata mwili unapokabiliana na maadui mimi ndio ninapanbana.Kwa upande mwengine; mguu nao ukasema kumwambia mikono. ``Mimi ni bora kuliko wewe kwani mimi ndio nina kwenda huku na huko kuwasaidia nyinyi nyote.’’ 
Kusikia maneno hayo kichwa kikasema mimi ndio kiongozi wenu nyote. Nikiondoka mimi tu hakuna ateweza kuishi tena. Nyote mtakufa na kusahaulika kabisa. Kusikia hivyo viungo vyote vikasalimu amri na kurejea kufanya kazi kama kawaida