Ukidanganya kufika kileleni wakati wa sex leo utaharibu maisha yako ya sex kesho.
July 19, 2019
Edit
Ndio! ndio! ndio! ni kawaida ya wanawake wengi kudanganya kuwa wamefika kileleni wakati wa sex.
Kwa utafiti ambao umeshafanyika Katika Chuo Kikuu cha Brigham Marekani ilibainika kuwa asilimia 43 ya wanaume walidanganywa na wake zao kuwa wanafika kileleni.
Utafiti huo unaonyesha ni asilimia 87 wanaume wanafika kileleni wakati wa sex na kwa wanawake ni asilimia 49.
Wanawake wengi kushindwa kufika kileleni kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokumaliza tendo hilo, hofu ya usalama, na tatizo la kisaikolojia, kuwa na woga wa kutofika kileleni,
Na taitizo ambalo mara nyingi huwakuta wanawake ni hofu ya kuwaumiza wanaume wao kwa kumwambia ukweli kuwa hawajafika kileleni.
Tatizo kubwa linakuja sasa, kama mwanamke ukianza ku fake kuwa umefika, unaweza kujisikia haja ya kuendelea na kujikuta unajiwekea ukuta kwa njia ya mawasiliano kuhusu kile unachohisi kwako ni vizuri na kile ambacho sio.
Utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake wengi hushindwa kuwaambia waume zao ukweli kwa kudhani kuwa mwanaume amesharidhika na hata akimwambia hataweza kufanya tofauti.
Utafiti huo pia unaonyesha kwamba wanaume wengi hua na mashaka juu ya furaha ya kufika kwa wapenzi wao, na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba wanaume wengi hawajui wanawake zao wanataka kufanyiwa nini wakati wa sex.
Ufumbuzi wa tatizo hilo kwa wanawake ni kuwa na maongezi yalioko wazi na wapenzi wao.Inapendekezwa kuwa wakati mzuri wa kuongelea hilo ni wakati ambao hamfanyi mapenzi.
Kuongelea suala hilo positively na sio kwa ukali, kuongea kwa mfano kama “nataka tujaribu kufanya tofauti leo” na sio kuongea kama “Tukifanya mapenzi hua hufanyi hivi” na hiyo itakua njia bora ya wote wawili katika mahusiano yenu.