Ukikosa sababu usivumilie Katika mapenzi - RAHA ZA KITANDANI

Ukikosa sababu usivumilie Katika mapenzi


NIMEWASIKIA washauri wengi wakisema uvumilivu ni kitu muhimu katika mapenzi! Bila shaka hata wewe umewahi kuambiwa na wazazi au rafiki zako “vumilia tu” ukiaminishwa kuwa ndoa au mapenzi yana changamoto nyingi zinazohitaji uvumilivu. Kama hujui, uvumilivu ni mzigo mzito; ukikubali kuvumilia, lazima uwe na sababu ya kufanya hivyo.