Uaminifu Nguzo Muhimu Katika Mahusiano.
June 28, 2019
Edit
By Danieller Kitimbo
Katika maisha ya mwanadamu kitu cha muhimu ni upendo. Upatapo mtu anayekupenda na kukuthamini na kukuelewa maisha yako huwa yanabadilika hata mwonekano wa nje wa mtu huwa unabadilika.
Jambo la msingi katika maisha ya mwanadamu ni uaminifu. Haswa kwenye maswala ya mahusiano;mahusiano yanapo kuwa na upendo ila bila uaminifu ni kazi sana kudumu.Uaminifu ndio nguzo moja wapo kuu nayo beba mapenzi baina ya watu wa wawili ambao wanapendana.
Uaminifu sio swala tu la kuwa na mpenzi moja, bali uaminifu inahusisha kuwa wawazi juu ya jambo Fulani linalohusiana na maisha yenu wote wawili.wengi hufikiri uaminifu ni swala la kuwa na mpenzi moja la hasha sio kweli.Bali uaminifu ni kitendo cha uwezo wa kuuliza kitu pale uonapo jambo haliko sahihi na unashindwa kuelewa.
Kukosekana kwa uaminifu kunaleta kugombana kutokuaminiana na pia mwisho huleta kuvunjika kwa mahusiano ambayo hugharimu muda mwingi sana wa mtu mpaka hapo atakapo kuja kukaa sawa na kurudi katika maisha yake ya kawaida,na mara nyingine humfanya mtu kuwa mwoga sana katika kuanzisha mahusiano mapya na mpenzi mwingine.
Usipende kusikia jambo ila penda kuwa mwonaji wa jambo zaidi na kuwa msikilizaji wa jambo zaidi kuliko kusikia au kuambiwa jambo juu ya mpenzi wako.
MAPENZI NI UAMINIFU.