HADITHI: Hii dunia Ina mambo, Soma hii stori, kweli siri haina wawili - RAHA ZA KITANDANI

HADITHI: Hii dunia Ina mambo, Soma hii stori, kweli siri haina wawili


📦SIRI HAINA WAWILI📦
👂Imesimuliwa kuwa
🙇Palitokea mtu maskini jina lake ban hashim na alikuwa na mke maisha yake alijishuhulisha katika kilimo.
🌼Siku moja wakati akilima aliokota fungu la dhahabu shambani alilibeba akafurahi na kushukuru licha ya kuwa alikuwa na hofu sana
🌼Kwani alifikiri angelihadithia watu wasingemuamini kwa umaskini wake wangedhani huenda ameiba na hakuna ambae angeweza kuinunua dhahabu hio ila wangemtapeli tu
🌼Aliondoka akiwa ameibeba dhahabu yake katika mfuko akaingia nayo nyumbani kwake na kuificha bila mkewe kujua chochote
🌼Alipofikiria kumwambia mkewe juu ya mali alioipata aliogopea kuwa huenda mkewe akawatangazia majirani kisha wakaibiwa na wezi
🌼Akafikiria sana mwisho akapata ufumbuzi aliingia chooni akakaa muda kisha akamfata mkewake huku akiwa na uwoga
🌼Kisha akamwambia mke wangu ntayokuambia tafadhali iwe siri wala yoyote asijue nae mkewe alimuahidi kuwa angeiitunza siri hio pasi na mtu kujua
Akamwambia nilipoingiaa chooni kujisaidia ghafla walitoka ndege wawili kisha wakakimbia kimaajabu mkewe kuskia hivo alistaajabu😳 kwa lililomtokea mumewe
🌼Siku ya pili mkewe alikwenda kwa jirani yake wa karibu kisha katika stori mara akamwambia shoga angu lililompata mume wangu nila ajabu jana kaingia chooni baada ya kujisaidia wakatoka ndege watatu kisha wakaruka kimaajabu jirani alishangaa kisha akamwambia usiseme mume wangu alinikataza nisihadithie
🌙Ikapita muda jirani nae siku ameketi na watu akawasimulia jamani mnahabari mke wa ban hashim amenisimulia kuwa mumewe aliingia kujisaidia mara wakatoka ndege wanne wakarukaa kimaajabu habari zikazidi kuenea katika mji wao na kila alie hadithia aliongeza ndege mmoja ,3,4,5,6 mpaka ikafika kwa mfalme kuwa kuna mtu kajisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabu
🌼Jambo hili lilimshangaza sana mfalme 👳😳akatuma watu wakamkamate huyu mtu na wamlete kwake ili amuone huenda mtu wa ajabu sana
🌼Walitoka watu 🚶🏃wakamfata wakamwambia mfalme anakuita akashuhudie kwako juu ya habari kuwa wewe umejisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabu
🚶👬Basi Alitoka akaongozana na hao watu huku akiwa amebeba mfuko wake wa dhahabu bila ya watu kujua alichobeba mpaka wakafika mbele ya mfalme
🌼Mfalme 👳akamwambia je ni kweli wewe ndie ulie jisaidia ndege 100 kisha wakaruka kimaajabu?
🌼Ban hashim alicheka😬😆 kisha akamwambia mfalme hizi habari nilimsimulia mke wangu👂 kuwa nilijisaidia ndege wawili nashangaa zimeenea na kila alieambiwa alipomhadithia mwenzake aliongeza ndege mmoja mpaka imefika kwako niliambiwa kuwa nimejisaidia ndege 99 kisha na wewe ukaongeza mmoja wakatimia 100
👳Mfalme kusikia hivo alicheka 👳😆kusikia kisa hichi kisha ban hashim akamwambia mfalme mimi niliokota dhahabu shambani nikaona hakuna ataeweza kuinunua sana watanidhulumu💴💵 au kuniua 🔫na kwako sikuweza kukuletea kwani hawaingii ovyoo watu kwa mfalme ndio nikafanya hivi ili niweze kuja kwako kwa urahisi na dhahabu ni hii akaiweka mbele ya mfalme kisha mfalme alimpa pesa nzuri💰 zilizokuwa sawaa na mali yake akarudi na kuishi kwa furaha na mke wake.
📦Kisa hichi kinafunza kuwa ukiletewa habari✉ na mtu basi ichunguze na usizidishe kitu kwani watu huongeza yao au kupunguza kwa kila wanalolisikia na inatufunza mke kuwa na siri na mumewe na sio kuzitangaza kwa majirani
Kwani habari zinaruka kama mfano wa vumbi kuenea kwa haraka.
🌼Licha ya kuwa ban hashim alipata urahisi wa kuuza dhahabu yake lakini na kama ingekuwa madhara basi angeangamia kwa mdomo wa mkewake🙉🙊.
🚧Mwisho kisa hiki hakikutaja majina ya wahusika kilipo mfikia ban hashim alikisaidia kukitia majina ya wahusika ili kisipoteze sifa yake ya uweneaji😊
🌴🐪KISIWA CHA IMANI🐪🌴

😁😁😁😂😂😂

🙉🙉🙉Usisahau kushare kichekesho hiki.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wacheke😁😁😁💯✔