Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 8)
July 03, 2019
Edit
Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM.
SEHEMU YA 8
Wakati wao wanaingia ndani upande wa pili Hamad na Ticha wakiwa njiani wanarudi mjini ghafla walikutana na gari nyeusi imezuia bara bara mbele yao, walipata mshangao sana wakapunguza mwendo kisha wakasimama, upande alikokuwa amekaa Ticha alitokea mtu amevaa nguo ya kumfunika uso wake kama gaidi akamtandika Risasi Ticha na kutoeka. Alikimbia fasta mpaka kwenye gari hilo leusi lililokuwa limezuia bara bara kwa mbele akaingia ndani na kukanyaga mafuta, tairi zilizungushwa, rami ikasuguliwa vizuri jamaa akatoeka kimuundo huo akimuacha ticha katika wakati mgumu wa jeraha, risasi ikimpatia maumivu makali mno ya kushindwa kustahimilia na kupoteza fahamu.
*****
Seid na mama yake waliingia ndani wakiwa na furaha ya kutembelewa na wageni na kuachiwa chochote kitu, walijua siku hiyo uhakika wa kula vizuri upo.
"Mama leo nadhani tunakula nyama. Alisema Seid akiwa amekaa chini amejiegamiza ukutani na mguu mmoja kuusimamisha, alimuangalia mama yake aliekuwa anajifuta futa jasho usoni kwa kutumia khanga yake aliyokuwa amejifunga.
"Heee mwanangu unawaza kula tu wewe baba.
"Sasa tufanyie nini hiyo fedha uliyopatiwa?. elfu 20 chukua kumi lete tule vizuri leo.
" Ila kweli mwanangu, basi hapa itabidi uchukue baiskel yako uende sokoni uchukue japo nyama na viungo viungo hivi, Mungu ametuonamo, tunavyoishi yeye ndiye anaejua, ipo siku moja atatuokoa tu na hizi shida tulionazo. Tusiache kumuomba.
" Hilo ndilo la msingi mama yangu, dua kwa sana ndio kinachotakiwa, na hasa kuhusu masomo yangu Mungu aweze kuweka uwepesi matokeo yangu yarudi, naamini ipo siku mama tutafanikiwa tu nshallah. Alisema seid. Alimaliza na neno nshallah akanyanyuka chini na kusimama.
" Sasa nipe hiyo pesa niende huko sokoni.
Bi najma aliposikia mwanae amesema hivyo aliziangalia pesa alizopewa ziko wapi na kutoa elfu kumi kumpatia, aliichukua seid na kuangalia kwa kuigeuza geuza akaachia tabasam.
"Tena hiki chakula nataka nikipike mimi mwenyewe uone nilivyo vizuri kwenye kupika mama.
"Ebu nitokee huko unajua kupika wewe!.
"Sasa mama hutaki au.
"Una miaka 20 mwanangu, mama yako nazeeka tena utoto upunguzege Eh!.
"mtoto hakui kwa mama, ila si tutampelekea na bibi?.
"hayo meno anayo?.
"We unayo? ,, seid alimtupia swali mama yake kama utani baada ya kumuuliza kama bibi yake ana meno
"Ebu nenda huko nna miaka 40 tu sijazeeka kiivyo mwanangu ila bibi yako anaenda kwenye tisini yule sasa hivi.
Seid alitoka na kumuacha mama yake anacheka, akachukua baiskel na kwenda kwenye soko la kiwengwa lililoko pwani mchangani kwa ajili ya kuchukua mazaga zaga ya mapishi ili wale vizuri siku hiyo bila kujua kilichomkuta hamad na ticha kipindi wanaondoka.
Alijikokota na baiskeli akijaribu kuzinyonga pedeli kwa nguvu ili afike haraka sokoni, uso wake ulionekana kuwa wa furaha kutokana na kujua mapema kuwa angekula chakula kizuri siku hiyo tofauti na masiku mengine yote.
Uso kwake ukiwa na furaha za kumwaga, upande wa pili kwa Hamad sura yote ilikuwa imeharibika kwa kuchanganyikiwa baada ya ticha kupigwa risasi, ubongo uliripuka na kushindwa afanye nini kwa haraka, jasho liliuzunguka uso wake huku na mwili wote ukihisi muwasho.
Hakujua afanye nini licha ya kuweza kutulia sehemu moja na kukosa papara za kuushughulisha moyo, alituliza akili, akijua endapo atakuwa na itikadi za kudata tu kutokana na kile kilichoko mbele ya macho yake hatofanya chochote. Alikuwa akipenda sana kumfatilia Wiliam shujaa alieishi miaka zaidi ya 100 duniani na kufanya mengi ikiwemo kuwakomboa watu zaid ya mia nne waliokuwa wametekwa katika meli ya uharamia somaria na kuwarudisha nchini Uingereza bila kukwama katika harakati za uandishi wake. Mawazo ya kuukumbuka ushujaa wa huyu jamaa yalimuingia, alitulia akashusha pumzi japo tayari na machozi ya presha yalishaanza kumlenga lenga, alitoa cm na kubonyeza namba za emergency call, police station akapiga, Cm haikuita sana ikapokelewa.
" Mahonda police station tukusaidie tafadhali. Ilisema sauti ya upande wa pili iliyosikika kuwa nzito kwenye cm.
" Hal,,loo haloo! Naomba mnisaidie haraka iwezekanavyo, tumevamiwa na mtu tusiomfahamu kipindi tunatoka kiwengwa, mwenzangu amepigwa risasi mimi ni mtoto wa mzee shaibu. Alisema hamad.
" Umesema uko wapi? Aliuliza kamanda, alipoambiwa mtoto wa mzee shaibu tu hakuitaji maelezo mengi zaidi.
" kiwengwa.
" Naomba nipate maelezo yote na aina ya gari iliyowavamia.
" Ilikuwa ny'e ny'eusi. Alisema pumzi zikikatika na kushindwa kabisa kuongea sentensi ndefu.
" Namba za gari?.
" ZNZ 654 AD.
Aliweza kujieleza vizuri hamad japo alishaelemewa na mzigo uliokuwa mbele yake, kamanda wa police alimuomba apunguze presha aendeshe gari kwa makini kupitia njia ya mahonda iendayo mjini atakutana na gari ya wagonjwa na watampeleka Ticha hospital haraka iwezekanavyo, huku yeye akifanya juu chini kuhakikisha anateua vijana wa kuifanya kazi ya kulitafuta gari lililowafanyia uhalifu.
Cm ilikatika hamad akafanya vile alivyoambiwa, mikono ilikuwa inatetemeka na kuwa na misisimko isiyoisha, alishika usukani wa gari akakanyaga mafuta na kuanza kulitoa gari taratibu, Huku kamanda wa police mahonda aliejulikana kwa jina la saleh, aliepokea taarifa za kuvamiwa kwa hamad aliteuwa vikosi makini kutoka katika idara yake, vijana wanne wanne magari manne tofauti waende haraka kufatilia uhalifu huo uliotokea ikiwezekana kulipata hilo gari.
Bila kupoteza muda vijana hao waliochaguliwa. Waliokuwa wakifanya kazi katika kituo cha police cha mahonda waliingia kwenye magari na kuanza safari.
Gari moja lilipita njia inayoelekea Donge na matatu kupita njia iendayo kinyasini, yalipofika kinyasini moja lilikata njia ya kiwengwa, mawili kusonga mbele.
Na yenyewe yalipofika mbele yaligawanya moja likaelekea njia ya matemwe lengine likanyoosha kuelekea nungwi wakiamini kufanya hivyo lazima gari lipatikane labda tayari liwe limeingia mafichoni.
Taarifa zilizidi kusambaa ndani ya mda mfupi, Kamanda Saleh alizisambaza haraka baada ya kujua aliempatia habari ni mtoto wa mtu mkubwa Serikalini ndani ya Zanzibar. Aliwasiliana na makamanda wenzake mjini ili nao waweze kujiweka sawa kuingia bara barani kulisaka hilo gari.
Vituo vingi vya idara ya police vilipata kufahamu nini kinaendelea na kuwa tayari kusimama imara ili mtu aliefanya huo uhalifu akamatwe, walimwagika mabara barani na silaha nzito nzito wengine wakipakizana kwenye magari kwa ajili ya kufanya doria. Bara bara ya mfenensini ilifungwa kwa muda pamoja na round ya baut ya mjini inayokutanisha magari yatokayo bububu na kwengine kwenda bandarini na stend kuu ya darajani, walihakikisha wanafanya kazi kwa makini zaid, tayari walishajua kama watafanikiwa kwa hilo watatengeneza majina na kupata kuonekana katika vyombo vya habari kutokana na Tukio lenyewe japo limetokea ghafla.
Hamad alijitahidi kuendesha gari mpaka kufika mahonda, miwani ilishajaa mvuke wa joto ilibidi aivue, Ticha alikuwa pembeni yake akiwa hoi hajitambui. Walipofika na gari ya wagonjwa ndio ilikuwa inafika eneo hilo, walifungua milango haraka wakamtoa, walimuingiza katika amburance na kuanza safari ya kumpeleka haraka mjini hospital ya serikali m/mmoja.
Hamad alichukuliwa mpaka ndani ya kituo, Askar watatu walimzunguka wakiwa tayari kuandika ripoti za kile atachowaambia.
Kabla ya kuanza kumhoji, cm ya mezani ilianza kuita, kamanda alichomoa na kuweka sikioni.
" Police station mjini no 886, Tunaomba mtoto wa mheshimiwa afike kituo kikubwa kwa ajili ya kuandika ripoti haraka. Alisema wa upande wa pili ambaye alikuwa police pia anaefanya kazi mjini.
" Sawa mkuu.
Alitoa cm sikioni na kuirudisha kwenye meza, aliwaangalia vijana wake huku akisema.
" Inabidi akaandike Ripoti mjini haraka iwezekanavyo, chukueni gari lililobaki mwende nae mjini, kijana ingia ndani ya gari lako uongozane na vijana hawa ukaojiwe juu ya lililokukuta, ulinzi uko salama, nawaamini sana vijana wangu.
Hamad hakujibu chochote, aliinuka kwenye kiti alichokuwa amekaa, akatoka nje huku vijana watatu wakiingia katika difenda nyeusi. Alifika kwenye gari akafungua na kuingia ndani, aliwasha safari ya kwenda mjini ikaanza akiwa hana amani kabisa moyoni mwake.
Gari lake lilitangulia nyuma ikafata ya mapolice. Bado tafuta tafuta ya sehemu mbali mbali iliendelea kulitafuta gari lenye usajili wa namba ZNZ 654 AD. huku kukiwepo mawasiliano ya karibu ili kujuzana kuhusu taarifa za kila kinachoendelea kona zote.
Wananchi waliokuwa sehemu mbali mbali za bara bara walikuwa wanashangaa mapolice wanavyopiga doria jioni hiyo, kitendo kilichosababisha wengi wawe na maswali tofauti tofauti.
"Amy vipi leo kuna nini mbona doria!?.
mpemba mmoja aliekuwa anachoma maindi alisikika akimuuliza amy yake aliekuwa pembeni.
" Itakuwa kuna uhalifu ushafanyika tayari na hivi Zanzibar ilivyoharibika sasa hivi sijui!.
" Au washaiba wanyamwezi maana haweshi siku hizi kuvamia mabenk yetu, juzi tu hapo Piople's bank of Zanzibar wamevamia wakaondoka na mamilioni.
kabla hawajaendelea gafla waliona linatokea gari jeusi likiwa linatimka mbio nyingi sana bara barani. watu wote waliokuwepo sehemu hiyo iliwabidi watoke mbio mbio kwa uoga, walijua tayari pashakucha, hawakukaa sawa wakaziona difenda mbili zikiwa mwendo kasi, risasi nne kwa mkupuo zililia juu kwa juu, baadhi ya wakina mama walianguka chini kwa presha huku wengine wakikimbia mbio, mtu mmoja alisikika anasema akikimbia
" Jamani hivi hii zanzibar yetu ishakuwaje sasa hivi?, kila siku vita! Kila siku vita hatupumui jamani tushachoka sieee tushachoka Wallah Ah!.
Difenda mbili zilizofanikiwa kuliona gari hilo maeneo ya bumbwini likijaribu kutafuta upenyo wa panya ili kuingia vijijini na kuanza kutimuana nalo mbio, askar wa difenda hizo walipeleka mawasiliano kwa vituo vyote vya police vilivyo karibu na bara bara, ili vijaribu kuzuia bara bara zote hasa bara bara inayochomoza bumbwini kwenda mjini au kitope, kwani ndio sehemu walioko wakilifukuza kwa karibu.
Seke seke hizo zikiwa zinaendelea Baba yake hamad mzee Shaibu habari zilimfikia, Alichanganyikiwa ghafla kutokana na kumpenda sana mwanae, alipiga cm haraka kwa maofisa usalama kuuliza usalama wa mtoto wake kwanza .
" Ndugu zangu mimi ni Mzee shaibu, nimepata habari za Ticha mtu aliekuwa ameongozana na kijana wangu kupigwa risasi na kuambiwa kuna kash kash zinaendelea huko vipi mwanangu yuko salama?. Aliuliza.
"Mzee wangu mwanao yuko salama kabisa, tunaomba usiwe na wasi wasi jeshi la police linafanya kazi yake.
" Na imetokana na nini hiyo hali.
"hatujaweza kujua chochote kwa sababu anaejua kila kitu ni Hamad mwanao na bado hajaojiwa.
"vipi kuhusu Ticha.
kabla ya kumaliza kuongea cm ilikata, alitikisa kichwa.
"Jamani ni nini hiki kinatukuta zanzibar, mbona amani inatoeka kila siku? tunaishi roho juu juu juu ya familia zetu wallah kwa nini!
Hali ilikuwa bado si shwari maeneo tofauti tofauti, watu walilaani ovyo ovyo juu ya tendo wanaloliona, wengine walipata presha na kuzimia hapo hapo. Kwa bahati nzuri hakukuwa na magari mengi katika bara bara za shamba, maskari walishawasiliana kila sehemu kuhakikisha wanaliwinda gari hilo lililoonekana kuwa imara, Risasi kadhaa zilipigwa juu kuangalia kama litasimama lakini wapi, Difenda zilizokuwa zinalifukuza zilishakuwa nne.
Baada ya kuchukua muda mrefu wakipiga risasi juu bila kusimama, askar mmoja aliekuwa na cheo kuliko wengine alisikika akisema "Lengeni gari asituzingue mpumbavu huyo.
Askar walianza kulenga gari, Risasi moja ilifanikiwa kulenga tairi, tairi liliachia pumzi na kuliacha gari likianza kukosa mwelekeo. Risasi nyingine ilipiga tairi la pili kwa nyuma, ndipo gari lilianza kufuja na kushindwa kutembea tena baada ya kuvamia nguzo ya umeme.
Difenda zililizunguka gari hilo maaskari wakikaa makini kwa ajili ya kushambulia endapo kitatokea kitu tofauti, walishuka na kuanza kutembea taratibu. Moja ya maskar aliushika mlango wa gari lililofanya uhalifu na kuufungua haraka, ndipo alitoka jamaa yule yule aliemtandika risasi Ticha akiwa ameshikilia bastola mkononi.
" Tulia hivyo hivyo kama unataka salama ya kuishi, na wambie wenzako waweke vikaragosi vyao chini!. Alisema mhalifu akinyoosha bastola yake kumnyooshea askari aliefungua mlango wa gari, lakini kitendo chake cha kuongea japo alikuwa amejifunga kitambaa usoni, baadhi ya maaskari waliosikia sauti walihisi sauti hiyo kuifahamu, haikuwa ngeni masikioni mwao.
Askari huyo hakuwa na silaha alinyoosha mikono juu, askar mwengine aliekuwa nyuma akasikika akisema
"Mjinga mkubwa shusha Silaha yako haraka kabla sijamwaga ubongo wako, huna mtu wa kumtisha hapa, uko peke yako tuko zaid ya kumi teremsha bastola yako kwa usalama.
" Mnaweza kuwa zaid ya kumi na bado mkawa mabwana wadogo tu kwangu,endapo utathubutu kushut na mimi naondoka na huyu mwenzenu kwa sababu sishindwi kumshut kabla yenu hamjanishut. Alisema.