ZIJUE AINA 10 ZA WANAUME AMBAO NI PASUA KICHWA - RAHA ZA KITANDANI

ZIJUE AINA 10 ZA WANAUME AMBAO NI PASUA KICHWA


1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband).
HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband).
Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.
3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband).
Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.
4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband).
Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.