ZIJUE SABABU ZA KUCHELEWA KUOLEWA
September 06, 2019
Edit
NDOA ni muungano wa maisha yote kati ya watu wawili unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii. Katika utamaduni wa nchi nyingi uhusiano huo ni kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu na unalenga ustawi wao na uzazi wa watoto katika familia.
Mara nyingi harusi inafanyika kwa ibada maalumu kadiri ya dini ya wahusika. Miaka ya hivi karibuni nchi chache zimeanza kuruhusu ndoa kati ya watu wawili wa jinsia moja. Huo ni mpango wa Shetani na sio mapenzi ya Mungu.
Bila shaka mpenzi msomaji hasa wale mama, dada na shangazi zetu, mtakuwa pamoja nami pale ninaposema asilimia kubwa ya wanawake wengi Dunia ni kuona wakiolewa kwa kufunga ndoa na kuishi na wanaume wa maisha yao.
Unakuta mdada mzuri, ameumbika mashaallah na umri umefika wa kuolewa lakini analalamika kuwa kila mwanaume anayekuwa nae kwenye mahusiano hadumu nae, huenda akawa anajitaidi kutimiza majukumu yake kama mwanamke lakini ikifika muda anaachwa.
Usihudhunike ndugu yangu, ndio maana Mwenyezi Mungu akawaleta manabii na mitume sambamba na vitabu vitakatifu kuweza kumaliza changamoto hizi, ingawa vipo vitu vingi vinavyochangia mwanamke kuchelewa kuolewa.