USIPOKUBALI UDHAIFU HAMTOPATA FURAHA!
September 20, 2019
Edit
NI matumaini yangu kwamba mpenzi msomaji wangu uko vizuri, na unaendelea salama na mishemishe zako
Siku ya leo, nitazungumzia suala ambalo husababisha mahusiano ya watu wengi kukosa mvuto, furaha na kuwa yenye majuto. Suala lenyewe ni la mpenzi kutokubali udhaifu wa mwenza wake.
HILI NI TATIZO KUBWA
Unajua katika uchunguzi nilioufanya nimegundua mara nyingi katika suala hili watu wengi huwa hawagundui kama wapo kwenye tatizo.
Kwa mfano mdogo tu; Unakuta mpenzi wako anapenda kucheka. Ukizungumza suala lolote hata kama si la kuchekesha, yeye anacheka au kutabasamu.
Hii linaweza kwa namna moja au nyingine likawa linakukera. Ukamwambia mara moja au mbili kwamba hupendi, kwa sababu ni tabia yake au udhaifu wake, anashindwa kujikontroo. Mwisho wa siku linakuwa ni suala la kuwagombanisha.
Mfano mwingine unaweza kuwa ni kwenye masuala ya mapishi. Pengine mwanamke unayempenda si mtu wa kupika vyakula vya kukukosha roho.
Unaumia na kujiuliza unampenzi wa namna gani asiyejua kupika. Inafika wakati badala ya kula kwake unapita sehemu fulani na kujipigilia. Migogoro ndiyo inaanzia hapo anapofahamu.
Ukweli ni kwamba mifano ni mingi, ipo mingine ni mifano ya vitu vidogovidogo, kama uchafu, kuwa na mwenza asiyejali, yeye akifika ndani akivua shati anarusha popote, akishika sahani anaacha popote pale na hata kwenye suala zima la tendo la ndoa. Unaweza kuwa na mpenzi mwenye udhaifu katika sehemu fulani ambayo wewe ndiyo inakufurahisha.
Kutokana na udhaifu wake huo, inasababisha mnafikia hatua mnakuwa hamna furaha na raha kwenye uhusiano wenu.
UFANYEJE LINAPOTOKEA SUALA HILI?
Jibu ni kwamba kwanza kubaliana na udhaifu wa mpenzi wako.
Baada ya kukubali taratibu mwambie kinachokupa furaha kupitia tatizo hilo badala ya kumfokea au kumweleza maneno ya kukasirisha.
Kwa mfano; “Mpenzi ninapenda sana unavyonijali, lakini hiyo haitoshi pale unapokuwa hujali vitu vyako. Si vizuri kuacha soksi mezani. Ukivua viatu v i w e k e m o j a k w a moja kwenye henga.”
K w a l u g h a kama hii hakuna
ambaye atachukia kwa hicho ulichomwambia. Lakini vuta picha ukimwambia hivi;
“Hivi wewe mwanaume mbona huko hivyo, yaani uchafu umekuzidi kha! Mpaka soksi unaacha popote kiukweli umenishinda tabia.”
Kwa maneno haya hata kama kile unachoeleza ni sahihi lakini kwa uwasilishaji huu utakuwa unatengeneza jipu. Kwanza huyo mwanaume akilini mwake atafikiri humuheshimu, unaongea sana au hujafunzwa.
Wapo wengine ukimwambia hivyo atakurudia kwa maneno; “Kwani nikiweka kitu vibaya huwezi kutoa, kazi yako ni nini sasa hapa?”
Wewe utajibu; “Kwa hiyo kazi yangu ni kuokota soksi zako?”
Kwa hiyo mtajikuta mnajibishana maneno mwisho wa siku kila mmoja anakasirika na kunakuwa hakuna furaha tena. Kwa hiyo kukabiliana na changamoto ya udhaifu wa mpenzi wako, kwanza halafu tumia lugha nzuri kuitatua, kwa kumfundisha au kumuelekeza.