Victor Wanyama ashtaki kampuni ya Menengai kwa kutumia picha zake kimakosa - RAHA ZA KITANDANI

Victor Wanyama ashtaki kampuni ya Menengai kwa kutumia picha zake kimakosa

-Kampuni ya Menengai Oil Refineries iliweka picha za Wanyama kwenye mtandao wake wa Twitter wakati wa mashindano ya AFCON 2019
- Wanyama anadai kuwa kampuni hiyo ya Nakuru ilienda kinyume cha hadhi zake
Nahodha wa Harambee StarsVictor Wanyama, anaripotiwa kuishtaki kampuni ya mafuta ya Menengai kwa madai ya kutumia picha zake kwa matangazo yake.
Nyota huyo wa Tottenham anaaminika kufungua mashtaka dhidi ya kampuni hiyo katika mahakama ya Milimani mnamo Jumatano, Agosti 7, huku akitaka kulipwa fidia baada ya picha zake kutumika bila idhini yake.

Kampuni hiyo inasemekana kutumia picha za kiungo huyo wa kati pamoja na mvamizi hatari Michael Olunga na Ovella Ochieng kupitia mtandao wa Twitter wakati wa michuano ya AFCON nchini Misri.
“Kama unaamini unaweza basi sisi kama Menengai tungependa kuwatakia vijana wetu ufanisi katika mashindano ya AFCON," ilisoma taarifa ya kampuni hiyo kwenye Twitter.
If you believe it, you can do it. We at Menengai would like to wish our boys all the best in the . From , we believe in you!
View image on Twitter
22 people are talking about this
Katika ujumbe mwingine wa kampuni hiyo kwenye mtandao jamii, Menengai iliweka picha ya Wanyama na Olunga wakimkumbatia nyota mwingine wa Ligi Kuu huku akiwa amebeba mpira.
Hata hivyo, Wanyama anateta kuwa picha hizo zilitumiwa bila ya idhini yake, kwa hivyo ilikuwa kinyume cha hadhi zake.
Pia alidai kuwa ujumbe huo haukuwa wa kuitakia Harambee Stars ufanisi katika mtanange huo wa bara, bali kutangaza bidhaa za kampuni hiyo.