Kuchukuliwa Mume na ‘House Girl’ ni udhaifu wetu! - RAHA ZA KITANDANI

Kuchukuliwa Mume na ‘House Girl’ ni udhaifu wetu!



Leo nimekuja na mada inayohusu watu watatu wakuu kwenye nyumba zetu tunazoishi, dada wa kazi ‘house girl’, baba mwenye nyumba na mke.Somo hili moja kwa moja linamuangukia mke ambaye ni mamamwenye nyumba kwani yeye ndiye mwenye majukumu mazitio zaidi.Kutokana na majukumu hayo, hata kunwgi wako alipokuwa akikufunda alitaka uwe na uwezo wa kujituma kwenye ndoa yako.Najua umefundwa mengi lakini hili la kujituma unatakiwa ulipe kipaumbele.Kungwi wako wala hakukosea kwa sababu hilo ndilo moja ya mafunzo anayotakiwa kufundwa mke wa anayeenda kuitawala nyumba.Mke, hata kama ukiwa na dada wa kazi, unatakiwa kuishi naye kama ndugu yako, akiwa na kazi nyingi msaidie lakini usimpe kazi zinazomhusu mumeo, hizo unatakiwauzifanye kwa nguvu zako.Mwari wangu hata kama unafanya kazi jipange kwa ajili ya kazi za mumeo, hakikisha unasafisha viatu, nguo na vitu vingine vinavyomhusu mumeo, usimuachie dada wa kazi hata kidogo.Kuna wake za watu wanaoshindwa kupika, hili jamani ni balaa kubwa kwani si vyema kila siku kumuacha dada wa kazi ampikie mumeo.Ashakhumu si matusi, mke aliyeolewahawezi kumuacha dada wa kazi akafua nguo za ndani za mumewe.Tobaaa! Hivi wewe mwanamke unajuakama jasho la mumeo ni kivutio kikubwa kwa mtu anayefua nguo hizo?Hivyo unatakiwa kuchunga sana kwani msichana wa kazi naye ni binadamu, anaweza kuingiwa na shetani na kulitamani jasho la mumeo, sijui utamlaumu nani?Hebu vuta picha, mumeo anarudi kutoka kazini halafu anamkuta msichana wa ndani anafua nguo zake za nani, unadhani atajisikiaje, ataachakumtamani? Jamani wanawake wenzangu huko si kujisahau ni kuziangamiza ndoa zetu wenyewe.Jipange mwanamke mwenzangu hakikisha unafanya yale uliyofundishwa na kungwi wako, utajisikiaje msichana akisifiwa na mumeo kwa kupika chakula kizuri?Leo anasifiwa kwa mapishi kesho na keshokutwa atasifiwa kwa kingine, shauri yako wewe lalilia masikio tu.Jamani sijawaruhusu wasichana wa kazi kuwachukua waume za watu, la hasha, bali kuwataka wake kuwa makini na waume zao kwani kinga ni bora kuliko tiba.Mwanamke mwenzangu zingatia hayoniliyokueleza leo wanawake wengi wameshaachika kwa sababu ya wasaidizi wa ndani.Amka mwari wangu kumekucha mumeo atabebwa na msaidizi wa kazi, wee hayaaa weee.