SEHEMU 4 za Mwili Usizopaswa Kumshika Mkeo Nyakati Hizi
April 15, 2019
Edit
Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa na waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero au kuwakwaza wake zao.
Kama tunavyofahamu, wanawake ni viumbe wenya mlango mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya tendo anaweza asizingatie sana anataka kukidhi haja yake.
Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake, utabaini kuwa ni rahisi sana kufahamu kwani mwanamke katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana wakati anataka kuguswa.
1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani
Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’ kuendelea na zoezi la kushiriki tendo.
2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho kabla ya kuoga
Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi japo sio wengi. Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa jasho.
3. Sehemu za siri kabla ya kuoga
Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kulalamikia waume zao. Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu, hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.
Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni wasafi.
4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba
Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa wewe.
Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema mtaharibiana ‘mood’.
Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mmewe.