HIVI NDIO VYAKULA 10 VINAVYONENEPESHA ZAIDI NA KULETA VITAMBI.. - RAHA ZA KITANDANI

HIVI NDIO VYAKULA 10 VINAVYONENEPESHA ZAIDI NA KULETA VITAMBI..



kumekua na tafiti nyingi zinzoonyesha vyakula vipi vinanenepesha watu zaidi duniani, japokua kila chakula kinategemea na kiasi unachokula lakini baadhi ya vyakula hunenepesha sana vinapoliwa na ni hatari kwa afya kwani huleta magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo na saratani ambayo yanaongoza kuua watu wengi zaidi duniani kila mwaka. kama wewe ni mnene unataka kupungua, kama wewe ni mwembamba unataka kubaki hivyohivyo basi kaa mbali na hivi.
chipsi; hiki ni chakula kinacholiwa sana na watu duniani, kwani ni rahisi kuandaa na kukiuza na ukiwachunguza walaji wa chakula hichi  hua wana vitambi sana  au ni wanene..chips husababisha mazoea yaani addiction ambayo humfanya mlaji atamani kuzila kila siku na kunenepa zaidi kwani ukizila husikii kushiba na kula nyingi zaidi..
vinywaji vitamu; unywaji wa vinywaji vitamu sana kama soda na ice cream au kuweka sukari nyingi sana kwenye chai au juisi husababisha homoni ya insulini kutengenezwa nyingi sana, baada ya muda homoni hii inakua nyingi muda wote kwenye damu na kubadili sukari kua mafuta na kuiingiza ndani ya seli badala ya kuiacha itumike kwa kazi za kuupa nguvu mwili.
                                                        
nyama; ulaji wa nyama nyingi hasa  nyekundu yaani nyama za nguruwe, mbuzi na ngombe husababisha kuhifadhika kwa mafuta mengi sana mwilini na kuongezeka kwa lehemu au cholestrol ambayo ndio chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo.kitaalamu mtu anatakiwa ale 70 gram ya nyama tu kwa siku sawa na finyango tatu tu ndogo lakini pia nyama hukaa masaa 20 kwenye mfumo wa chakula kabla ya kutolewa nje kama kinyesi.

viazi; viazi vitamu au viazi vya kawaida vinanenepesha sana bila kujali kwamba unavichemsha au unavikaanga kwani vina kiasi kikubwa sana cha nguvu au calories ambazo baadae hugeuka kua mafuta ndani ya mwili hivyo ulaji wake unatakiwa ue mdogo sana..
                                                                
                                                                
vyakula vya kukaangwa; vyakula vyote vya kukaangwa kama maandazi, vitumbua, chapati,sambusa, soseji,  nyama na mikaango yote unayofahamu hua na mafuta mengi ambayo mafuta hayo huingia mwilini na kumfanya muhusika awe mnene sana.
                                                        
juisi za viwandani na kuandaa nyumbani; hizi mara nyingi hua zina sukari nyingi sana ambazo kama nilivyoelezea hapo juu, sukari hii ni hatari sana na itakunenepesha tu. hakikisha unaandaa juice yako nyumbani na kuweka sukari kidogo na usinunue juice za viwandani au zinazouzwa vijiweni na mama ntilie kwani zina sukari nyingi sana.

mafuta ya kuganda; haya ni mafuta yanayoandaliwa na kua kama ya mgando...ulaji wa mafuta haya kwa mfumo wowote ule kama blue band, mayonise, kimbo au siagi hunenepesha na kuongeza kiasi cha lehemu au cholestrol  mwilini, mafuta hayo yakiingia mwilini huganda kama yalivyokua nje kabla haujayala...ni vizuri kuyaepuka na kutumia mafuta ya maji kama alizeti, korie na kadhalika..
pipi, biskuti, keki na chocolate; hivi ni vyakula ambavyo vinaonekana vina umbo dogo sana lakini vina kiasi kikubwa cha sukari na nguvu[calories] kiasi kwamba ukila inabidi ufanye mazoezi makali sana kuondoa mafuta yanayoingizwa mwilini na vyakula hivi.
                                                  
wali; wali unaopita kiwandani kurekebishwa na kuonekana mweupe zaidi, ni moja ya vyanzo vikuu vya unene na unaliwa sana dunia nzima na bei yake ni rahisi lakini hata huu wali wa kawaida tunaochukua mashambani unatakiwa uliwe kwa kiasi kidogo sana, angalau kikombe kimoja kidogo  cha wali uliopikwa kwa mlo mmoja...ukila zaidi ya hapo kitambi na unene huwezi kukwepa.
                                                          
tambi; ulaji wa tambi angalau mara moja au mbili kwa wiki hauna shida, tatizo linakuja pale mtu anapoamua kuzila kila siku..hapo unene hauwezi kukwepeka kwa mlaji huu kwani zenyewe zina wanga mwingi na pia huongezewa chumvi au sukari na kufanya vinenepeshe zaidi..
                                                                


mwisho; vyakula vya wanga ni chanzo kikuu cha unene ulipindukia duniani na ni vyakula vikuu vinavyoliwa na watu...ni vizuri kujenga tabia za kutokula wanga kila siku yaani sio lazima kila siku ule wali, ugali au viazi na mboga...unaweza ukala mboga tu kama dagaa, samaki,bamia, mboga za majani,matunda siku nzima bila kula wanga kabisa.

HIVI NDIO VYAKULA 11 VINAVYOPUNGUZA UNENE NA KUTOA KITAMBI.

                                    
                                 
makala iliyopita nilizungumzia vyakula vinavyoweza kusababisha mtu kunenepa sana... kama hukuona makala hiyo soma hapa  katika vyakula hivyo nilivyozungumzia kuna ambavyo ni muhimu kuepuka kabisa kama soda, biskuti, ice cream na kadhalika kwani havina umuhimu kabisa mwilini na kuna vingine vya wanga kama wali,ugali,tambi,viazi,mihogo huwezi kuacha kabisa ila ni muhimu kupunguza na kula kwa kiasi kidogo sana kulingana na shughuli zako. kupunguza uzito kunataka nidhamu sana ndio maana watu wengi wameshindwa kupungua na kukata tamaa  lakini sheria kuu ni moja, mazoezi sana na kula kidogo..bila kubadilisha mfumo wako wa maisha na kula kidogo huku ukifanya mazoezi kwa nusu saa angalau mara tatu kwa wiki hata ule dawa gani unaweza ukapungua baadae ukarudi palepale. lakini pamoja na hayo kuna vyakula ambavyo ni muhimu sana kuvila wakati unapunguza uzito kwani vinasaidia kuchoma mafuta ya mwili lakini vyenyewe pia vina nguvu au calorie kidogo sana kiasi kwamba hata vikiliwa kwa kiasi kikubwa sio rahisi kunenepesha.
mayai; mayai ya protini nyingi sana ambazo zinamtosha kifaranga kutoka ndani ya yai hilo akiwa mzima. kawaida protini hujenga misuli ikiliwa kwa kiasi kinachotakiwa.utafiti unaonyesha binadamu wa kawaida anatakiwa ale mayai angalau matatu kwa siku kuondoa uwezekano wa kuongeza cholestrol ambazo ni hatari kwa moyo. ukiamka asubuhi ukala mayai kama sehemu ya kifungua kinywa chako utakaa muda mrefu bila njaa..mayai nayozungumzia hapa ni yale anayotaga kuku mwenyewe hasa ya kienyeji.
mboga za majani; hizi ni kama mchicha, bamia, nyanya chungu,kabichi, spinachi, kisamvu, msusa na zingine nyingi...mboga hizi zina vitamini nyingi, fibres au nyuzi nyingi na  wanga kidogo hivyo zinaweza kuliwa kwa kiasi kukubwa na kujaza tumbo bila kusababisha unene lakini pia zinaitwa kitaalamu kama antioxidant yaani zinaweza kuondoa sumu mwilini.
samaki; samaki wana kiasi kidogo sana cha mafuta, wana protein nyingi ambayo itakuacha muda mrefu ukiwa umeshiba na kukufanya usile sana...lakini pia samaki wana kemikali ya omega 3 ambayo ni muhimu sana kwenye mwili kwani huzuia magonjwa ya moyo na kusaidia kazi ya kuchoma mafuta.
maharage; hichi ni chakula kizuri sana cha asili ambachi kimewakuza watu wengi,  kina protini ya kutosha pamoja na fibre yaani nyuzi ambazo ni muhimu sana. lakini pia nguvu au calorie yake ni kidogo sana.
maparachichi; wakati matunda mengine yana sukari nyingi, parachichi zina mafuta na nyuzi ambazo ni muhimu sana kwa afya ya moyo na kupunguza uzito. maparachichi pia yana mafuta aina ya oleic oil ambayo yanapatikana kwenye mafuta ya mizaituni au olive oil  na hua yana maji mengi na kumfanya mlaji kutoishiwa maji mwilini.
karanga na korosho; japokua vyakula hivi vina mafuta, mafuta yake ni salama sana hayanenepeshi kama mfuta yatokanayo na wanyama...tafiti zinaonyesha kwamba mafuta haya huweza kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta mwilini.
                                                   
matunda; matunda yote unayofahamu yanapunguza uzito isipokua machache yenye sukari nyingi kama ndizi mbivu na zabibu..tafiti zimeonyesha watu wanaokula matunda mengi hua wanakula chakula kidogo sana sababu mafasi kubwa ya tumbo inachukuliwa na matunda ambayo hayaongezi uzito.                                                  
nyama ya kuku; hasa kuku wa kienyeji ambao wanakuzwa kiasilia, huwa na protein nyingi sana ambayo inajenga misuli badala ya kuongeza mafuta mwilini, kuku wa kisasa wana kemikali nyingi sana ambazo zinahusiana na magonjwa hatari kama kansa na kadhalika. kumbuka kama unakula kuku kupunguza uzito usile ngozi yake kwani ina mafuta mengi.
mafuta ya maji; mafuta yanayokuja kwa mfumo wa maji kama korie, mafuta ya nazi na alizeti ni mazuri sana kwani yakiingia mwilini hubaki kwenye mfumo ule ule lakini mafuta yanayokuja kwa mfumo wa kuganda kama kimbo, blueband na siagi sio mazuri kwani yakifika tumboni huganda vilevile.
viazi mviringo vya kuchemsha; japokua watu wengi hawataki viazi hivi na kuamua kuvikaanga kila wakati ili wale kama chips lakini ni chakula kizuri sana kama unataka kupunguza uzito..vina sukari kidogo na kiasi kikubwa cha potassium..
maziwa; tofauti na watu walivyokua wanafikiria zamani kuhusu maziwa kwamba yananenepesha sana, utafiti umeonyesha maziwa yanasaidia kupunguza uzito kwani yana kiasi kikubwa cha calcium ambacho husaidia kuchoma mafuta mwilini.