ZIFAHAMU SABABU KUMI MUHIMU ZINAZO SABABISHA MIMBA KUHARIBIKA... - RAHA ZA KITANDANI

ZIFAHAMU SABABU KUMI MUHIMU ZINAZO SABABISHA MIMBA KUHARIBIKA...



utafiti unaonyesha kati ya mimba 100 zinazobebwa ni 80 tu ndio zinafika kuzaliwa, yaani asilimia
 ishirini ya mimba zinazobebwa huharibika hata kabla ya kufika mezi watatu. kuna sababu nyingi zinazoweza sababisha mimba kutoka lakini leo nteanda kongelea zile muhimu ili kila mtu kama iko ndani ya uwezo wake aweze kuzuia pale anpopata mimba.

matatizo ya vimelea vya urithi: kawaida mbegu za mwanaume huchangia pea 23 za vimelea vya urithi yaani chromosomes na yai la kike hichangia vimelea 23 pia kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa, lakini kwenye hali isiyo ya kawaida namba hiyo ikiongezeka au kushuka husababisha mimba kutoka ndani ya muda mfupi.

magonjwa; kuna magonjwa mengi endapo hayatatbiwa wa muda muafaka husababisha mimba kutoka muda wowote ule yaani inaweza kua mwanzoni au mwishoni.mfano. malaria, kisukari, pressure, kaswende, virusi vya ukimwi, U.T.I, toxplasmosis,rubella, na herpes simplex virus.

matatizo ya kizazi; kuna magonjwa mengi yanayoahiri kizazi moja kwa moja na huweza kuleta kutoa mimba kirahisi sana mfano wa magonjwa hayo ni uvimbe wa ndani ya kizazi,ulegevu wa mlango wa uzazi na kadhalika.

matumizi ya dawa; ukiwa mjamzito hutakiwi kutumia dawa yeyote bila kuandikiwa na daktari, kuna dawa nyingi sana zinaweza kutoa mimba mfano fragile, albendazole,misoprostol, dawa ya mseto ya malaria, doxycline, na nyingine nyingi.
utapiamlo;  mwanamke mwenye upingufu wa madini muhimu mwilini kama calcium, potassium na sodium lakini pia wanga, protini, vitamini na kadhalika. upungufu huu humfanya mwanamke ashindwe kubebeba mimba mpaka kujifungua na hata akijifungua huweza kuzaa mtoto mwenye mapungufu fulani ya kiakili.

matatizo ya homoni; mwanamke ana kiwango maalumu cha homoni za uzazi ambacho anatakiwa awe nacho ili mimba iweze kutungwa na kukua. kiwango hiki kikiwa juu sana au chini sana husababisha mimba kuharibika.

aina ya maisha ya mjamzito; matumizi ya pombe na sigara kipindi cha ujauzito ni hatari sana kwani huingilia mfumo wa homoni na uzazi na kusababisha mimba kuharibika.

umri mkubwa; kubebe mimba kwenye umri mkubwa huchangia sana mimba kuharibika kwani kipindi hiki viungo vya uzazi na mfumo wa homoni unakua umepungua nguvu sana hivyo mimba za ukubwani sana hasa zaidi ya miaka 35 hutoka kirahisi kuliko mimba za vijana wadogo.

mazingira ya kuishi; maeneo mengi karibu na viwanda au huduma za mionzi ya hopitali hua kuna mionzi hatari ambayo huweza kuingia kwa mama na kuharibu mtoto aliyeko tumboni lakini pia uwezo wa kuzaa huko mbele ya safari.

upungufu wa damu; kipindi cha ujauzito akina mama wengi hua na damu chini ya kiwango kutokana na mabadiliko ya kimaumbile, lakini upungufu huo ukizidi zaidi husababisha uchungu kuanza kabla muda na mimba kuharibika.

mwisho; kila mtu anahitaji mtoto katika kipindi fulani cha maisha yake hivyo ni vizuri kujilinda na vyanzo hivyo kabla na baada ya kupata ujauzito kwa kufuata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya na kukaa mbali na mazingira hatarishi ya kuharibu ujauzito. kwa maelezo zaidi bofya maneno hayo ya kijani kusoma