Kwanini Hupungui Uzito Mkubwa Na Kitambi - RAHA ZA KITANDANI

Kwanini Hupungui Uzito Mkubwa Na Kitambi


Kama wewe ni muhanga wa tatizo la uzito mkubwa na kitambi, umejaribu njia nyingi za lishe lakini bado hupungui uzito basi utakuwa na uzoefu kwamba wanaume hupungua uzito kiurahisi zaidi kulinganisha na wanawake. Kuna baadhi ya sababu zinazokwamisha wanawake kupungua uzito kwa haraka. Uzito mkubwa na kitambi kwa mwanamke inaweza kuwa kero sana na kukunyima furaha, utashindwa kufurahia tendo la ndoa na pia kujiachia na marafiki.Makala yetu ya leo itazungumzia kwa upana na kujibu swali lako kwa nini hupungui uzito.

Kwanini Wanawake Hupata Shida Kupungua Uzito.

Unaweza kuwa umejaribu njia nyingi mpaka kukata tamaa kwamba hutaweza tena kupunguza uzito wako na kutengeneza shape nzuri. Kumbuka haupo peke ako, kuna kundi kubwa linateseka na uzito bila mafanikio, ndio maana nimeandika makala ya leo kukupa elimu na point za kutumia ili uondoke kwenye kifungo hichi.
Sasa na tuangalie kwa kina sababu 9 zinazofanya wanawake washindwe kupungua uzito na kuhangaika pasipo mafanikio

Sababu ya kwanza: Unakula Vyakula Visivyotakiwa

Kwa bahati mbaya vyakula vingi vinavyotunzunguka kwenye maduka, supamaketi na migahawani ni vyakula hatarishi kama chips, mikate, mandazi soda na vyakula vilivosindikwa  vinvyoharibu mwili na kukufanya uwe na uzito mkubwa na kitambi.
Usipumbazwe na vyakula vilivyoandikwa low fat au no fat kwani ndani  yake vinakuwa na vimejazwa sukari na viambata vya kuongeza ladha, ili kudanganya ulimi wako na kukufanya uwe mteja wa sukari kila siku.
Sukari ni adui wako mkuu kwenye swala la uzito na kitambi, vyakula vingi kama mtindi na tomato sauce vinakuwa na sukari nyingi  na kukuacha kuwa mteja wa kila siku, kichwa kuuma na kuhangaika kupungua uzito bila mafanikio.

Unajuaje Kwamba Vyakula Unavyokula ni ndio Adui Wako

Tazama kwenye friji lako kama vyakula na vinywaji ni vya makopo, kwenye mabox ama kwenye vifungashio basi muda wa kutupa vyote hivi na kuanza upya.

Nini cha kufanya

Jambo la kwanza ni kufuta vyakula vyote ambavyo vinakupa uzito mkubwa na kitambi kama nilivyoeleza hapo juu. Chagua vyakula asili na halisi, kwa maana ya vaykula unavyopika mwenyewe visivyochakatwa kiwandani.
Kama utanunua snacks na vyakula vingine vya haraka basi hakikisha unasoma maelezo ya viini lishe na kemikali zilizomo. Chukua muda wa weekend  kuaandaa chakula chako nyumbani ambacho unaweza kula week mzima.

Sababu ya pili: Una Matatizo Kwenye Tezi ya Thairodi.

Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo-angalia picha hapa chini.
Kiungo hichi kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti. kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za triiodothronine (T3) na thyroxine (T4), ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili. Kazi za mwili huzorota na kukosekana kwa mpangilio endapo T3 na T4 ni kidogo sana ama inazalishwa kwa wingi kupita kiasi. Homoni hizi zinaweza kuvurugika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo lishe, madini kidogo ya iodine na athari za metali nzito kwenye mwili kama mecury.

Unajuaje Kama Una Tatizo Kwenye Tezi ya Thairodi

Kama kuna shida kwenye utendaji wa tezi ya thairodi basi utakuwa na dalili zifuatazo.
  • Mwili kushtuka na kusisimka kila mara
  • Kukosa usingizi
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio kuliko kawaida
  • Uzito kupungua pasipo kutarajia
  • Kutokwa na jasho jingi kusiko kawaida
  • Misuli kukosa nguvu
  • Mwili kuchoka mara kwa mara
  • Ngozi kuwa kavu
  • Kukosa choo kwa mda mrefu ama kupata choo kigumu
Kama tayari unapata dalili hizi basi hakikisha unaweka apointment na daktari ili kupata vipimo uanzee tiba mapema.


Nini cha kufanya

Kabla ya kuanza tiba ya hormone replacement therapy kwa dawa za kifamasia, hormone za asili kupitia kwa wanyama au upasuaji kwanza kabisa unahitaji kutazama umekosa nini kwenye lishe yako, shirikiana na dactari ili akuweke wazi juu ya tatizo lako, Ukishajua unachopungukiwa basi rekebisha kwanza lishe na utumie virutubishi kutoa sumu mwilini kisha angalia maendeleo ya tatizo lako. kama tatizo litaendelea kusumbua ndipo uanze hizi tiba.

Sababu ya 3: Una Mvurugiko wa Homoni zako

Kuvurugika kwa homoni za kike yaweza kuwa kikwazo kwenye safari yako ya kupungua uzito kama mwanamke. Mfano homoni ya cortisol ambayo hutolewa kwa wingi ukiwa na stress inakufanya uwe na njaa zaidi na uwe mlevi wa sukari na wanga ambavyo vinakuongezea unene.

Unajuaje Kama una Mvurugiko wa Homoni

Mambo Yanayoashiria kwamba una shida kwenye vichocheo/homoni zako
  1. Kupata hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku 7 unatumia zaidi ya pedi 2
  2. Hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana, kichefuchefu na kuharisha
  3. Kuwa na hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
  4. Hedhi ambayo haina mpangilio, Unaweza kuingia mara tatu kwa mwezi mmoja, mara mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi 6 hadi mwaka.
  5. Kuwa na ndevu sehemu za usoni,kifuani nyingi kupita kiasi
  6. Kuwa na kitambi cha tumbo la chini (Abdominal obesity)
  7. Kukosa mtoto kwa muda mrefu
  8. Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama lenye kuambatana na maumivu makali
  9. Mwili kuwa unauma sana hasa misuli bila sababu ya msingi, kuumwa sana na kichwa bila sababu ya msingi.

Nini Cha Kufanya

Punguza msongo wa mawazo ili kurekebisha utolewaji wa homoni ya cortisol.

Sababu ya 5: Dawa Unazotumia Zinakufanya Uwe na Kitambi

Kama unatumia dawa kila mara basi inaweza kuwa ndo kikwazo kwenye safari yako ya kupungua uzito. Baadhi ya dawa zinaweza kusababisha uzito kuongezeka, kupoteza hamu ya kula na kuongeza uzalishaji wa baadhi ya homoni. Moja ya dawa hizi ni vidonge vya kuzuia ujauzito.

Utajuaje Kama Dawa zako Ndo Kikwazo

Kama umetumia dawa kwa muda mrefu na kila ukijaribu njia mbalimbali za kupunguza uzito unakwama, ni muda sasa wa kubadili mwelekezo na kuongea na dactari wako vizuri

Nini cha kufanya:

Kabla hujaanza kumeza dawa mfano vidonge vya kupunguza maumivu na vidonge vya kupunguza athari ya msongo wa mawazo anza na njia za asili zisizo na madhara kwa mwili. Kama ulishaanza kumeza vidonge, ongea na dactari kama inawezekana kusitisha kwa muda kisha tazama uzito wako kama unapungua..

Sababu ya tano: Hupati Usingizi wa Kutosha

Kikawaida unatakiwa kupata masaa kuanzia 8 mpaka 9 ya kulala bila kelele wala mwanga. Matumizi ya mitandao kupita kiasi na msongo wa mawazo unakufanya ukose usingizi mzuri. Unapolala mwili unafanya kazi ya kutoa sumu. Kukosa usizngizi huvuruga homoni  na kukufanya uwe na uzito mkubwa na kitambi.

Utajuaje kama Kukosa Usingizi Ndio Kikwazo.

Tazama muda gani unaenda kulala na muda gani unaamka, kama unalala chini ya masaa 8 basi unahitaji kurekebisha ratiba yako.

Nini cha kufanya

Unapolala hakikisha unazima vifaa vyote vya kielektroniki kama simu, computer na televisheni, usiruhusu kelele kuingilia usingizi wako. Usitumie vinywaji vyenye caffeine kama energy drink, na kahawa karibia na muda wa kulala.

Sababu ya 6: Unakula Vyakula Vingi Kupita Kiasi

Unapokula chakula kila mara unaongeza idadi ya kalori mwilini. Kalori ni kipimo kiachotumika kuonesha nishati inayopatikana baada ya kiasi flani cha chakula kuunguzwa. Kumbe kiujumla kadiri tunavokula vyakula vingi tunaongeza kalori na mwili unatumia kiwango kidogo cha kalori kuzalisha nishati kiwango kinachobaki huhifadhiwa kama mafuta mwilini.

Nini cha Kufanya

kama chakula chako ni Wanga na sukari ni wakati wa kubadili lishe yako na kuanza vyakula vya mafuta. Vyakula vya wanga na sukari huchangia kalori nyingi zaidi kwenye mwili kuliko vyakula vya mafuta na protini.

Sababu ya 8: Una aleji ya Chakula

Kama unajiskia mwili kuchoka, tumbo kujaa gesi, mwili kuvimba, kutapika ama kichefuchefu baada ya kula aina fulani ya chakula ni wazi kwamba una aleji. Kadiri unavokula zaidi vyakula hivi mwili unatutumuka zaidi  na kushindwa kurekebisha uzito.

Unajuaje kama una Aleji ya Chakula

Kama unapata shida kuchakata chakula tumboni, tumbo kujaa gesi mda mwingi, matatizo ya ngozi yasiyoisha au kutapika na kujiskia hali mbaya baada ya kula aina fulani ya chakula basi utambue kwamba una alegi au mwili wako hauna uwezo wa kuchakata hicho chakula.

Nini cha Kufanya.

Ondoa vyakula vyote ambavyo ni adui kwa mwili wako hata kama unavipenda. Usitumie chakula ambacho mwili unakikataa.