ZIFAHAMU DALILI 10 ZA MPENZI ANAYECHEPUKA - RAHA ZA KITANDANI

ZIFAHAMU DALILI 10 ZA MPENZI ANAYECHEPUKA


Miongoni mwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwasumbua watu wengi ni mahusiano, basi nimeona nikuletee kwako baadhi ya dalili za mtu aliyechepuka kwenye mahusiano kama zilivyofanyiwa Utafiti na wataalam Duniani.
  1. Akirudi nyumbani hutumia dakika chache  ambazo haizidi moja toka kusalimia hadi kwenda bafuni kuoga.
  1. Mara nyingi mavazi aliyovaa siku hiyo, akishayavua hukimbilia kwenda kuyasokomeza kwenye kapu la  nguo chafu au chumba cha watoto wakati si kawaida yake.
  1. Ukimkazia macho usoni na kumuangalia , hukwepesha macho usoni na kumuangalia, hukwepesha macho yake kwa aibu dhamira anahisi kama umejua.
  1. Hatapenda kukaa sanjari na wewe muwewe kama kawaida yenu.
  1. Kama hatasingizia kuumwa tumbo saa mbili kabla ya kurudi nyumbani, basi atafanya hivyo akishafika tu.
  1. Mara nyingi akiingia ndani breki ya kwanza bafuni, hata kama alishaoga huko, kuondoa harufu ya sabuni ya gesti. Kisha nguo alova siku hiyo zinalowekwa fasta.
  1. Anabadili Nywila(Password) ya simu mara kwa mara, ukigundua mpenzi wako anabadili nywila mara kwa mara ujue kuna kitu anakuficha
  1. Mkiwa pamoja simu yake anaweka mbali, simu ikiita anapokea haraka na anakimbilia nje au chumba kingine kwa ajili ya mazungumzo, anatoa mlio wa simu, wakati mwingine mkuwa pamoja anageuza ili usione ikiita wala ujumbe.
  1. Baadhi ya wenza ni wajanja, ili kufunika kombe mwanaharamu apite hujifanya wanamahaba sana. Utaona mapenzi yanazidi ghafla tofauti na zamani, lengo ni kukufanya usihisi chochote.
  1. Kwa sababu anafahamu kile anachofanya, anadhani na wewe unafanya. Kutokana na tabia yake atakuwa mlalamishi kwa kitu hata jambo dogo la kuzungumza yeye atalalamika ili kukufanya ujisikie vibaya.
x