ETI....,WAPENZI WAKUTANE KIMWILI MARA NGAPI KWA WIKI, WATOSHEKE?
April 18, 2019
Edit
Kwa wiki nzima nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki tendo la ndoa na kulidhika.
Wengi kati ya hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili watosheke?
Jibu la swali hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini? Katika hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini, hii ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu.
Kwa msingi huo mtu akitaka kutosheka na penzi la mpenzi wake, ni lazima kwanza aitosheleze akili yake na kile anachopata, zoezi ambalo atalifikia kwa kutathimini uwezo wake wa kufanya mapenzi na wa mpenzi wake. Wengi kati ya watu wanaodai hawatosheki kimapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Nikijibu swali la ni mara ngapi wapenzi wakutane kimwili ili watosheke nitasema hivi: KUTOSHEKA HAKUNA IDADI, bali ni kwa kila mmoja kulidhika na mwenza wake kutoka ndani ya akili yake. Kama hapa sikueleweka vizuri katika jibu hilo, maana yangu hasa ni kwamba kutosheka ni namna mtu mwenyewe anavyoyaendesha mawazo yake.
Ukiyaendesha mawazo yako kufanya mapenzi mara kwa mara, hutatosheka hata ukipewa kila saa, kwa sababu fikra zako unazijenga zaidi ya unachopata. Uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao akili zao zimejaa mawazo ya ngono, hawawezi kulala bila kufanya mapenzi, lakini watu hao hao, ukiwapa matatizo yatakayochukua sehemu kubwa ya mawazo yao kwa mfano, kuwafunga jela, kuwafukuza kazi, kupata msiba, utashangaa wanaweza kukata wiki bila kusumbuliwa na tamaa ya ngono.
Hii ina maana kwamba unavyowaza ndivyo unavyotenda. Kitaalamu kinachofanya mapenzi ni mawazo, ndiyo maana wapo wanaojichua wenyewe kwa kutumia mawazo yao na kupata raha. Kila mmoja akijenga heshima juu ya fikra zake na kujali hisia zaidi tutakuwa na watu wengi wanaofurahia tendo la ndoa bila kujali wanalipata mara ngapi kwa wiki.
Uchunguzi wangu umebaini kuwa watu wengi hasa wapenzi wa siku nyingi na wanandoa, wanafanya mapenzi kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini si kwa kuheshimu fikra na hisia zao, jambo ambalo husababisha ladha ya mapenzi kuwa ya asilimia ndogo, ukilinganisha na mahitaji halisi ya mawazo yao.
Upo ushahidi wa kutosha kwa wanandoa wengi kupata msisimko mdogo wanapokuwa na waume/wake zao katika tendo la ndoa tofauti na wanapopata wasaa wa kusaliti ndoa kwa hawara zao.
Watu wa aina hii wasiseme kuwa hawatosheki na tendo la ndoa kwa sababu wanakutana na wapenzi wao mara chache zaidi, bali wanakutana katika mhemko wa chini usioweza kulifanya tendo hilo kuwa na raha ya kutosha.
Labda msomaji wangu utaniuliza, tatizo la kupata msisimko mdogo kwa mtu unayemzoea linachangiwa na nini? Jibu litakuwa ni MAWAZO ya mtu mwenyewe.
Ukichunguza utagundua kuwa, wapenzi wengi hasa wazoefu huwa hawapeani nafasi katika mawazo, kama wanavyotoa nafasi kwa wapenzi wa pembeni, hili ndilo tatizo linalopunguza msisimko wa kimapenzi na kuondoa hali ya kutosheka na penzi. Kama mtu anataka mpenzi wake amtosheleze, basi hana budi kumkuzia mwenza wake hisia kiasi cha kumtamani. Niulize swali, hivi ni mara ngapi wewe unayesema hutosheki na penzi ulishakaa peke yako ukamvutia taswira mpenzi wao kabla hajarudi nyumbani kiasi cha kupata msisimko wa kutana naye kimwili?
Wengi wetu hatufanyi hivyo, hatuna vitu vinavyotuvutia kwa wake/waume zetu, jambo ambalo hutufanya tukikutana nao kimwili kwa kutimiza desturi tu na kubaki na kiu zetu za penzi. Lakini uweli unabaki kuwa wapenzi wakikutana kipindi cha msisimko mkubwa na kupeana mahaba kwa usahihi hata ikiwa ni mara moja kwa wiki watatosheka.
Jambo kubwa la kuzingatia hapa ni kwamba wakati mwingine msisimko huo huwa hauwatokei wapenzi kwa wakati mmoja, hivyo ni jukumu lao kushirikiana pindi mmoja anapokuwa katika hali hiyo.