Mke wangu kaniambia hanipendi - ushauri tafadhali - RAHA ZA KITANDANI

Mke wangu kaniambia hanipendi - ushauri tafadhali



mhn! sijui hata nianzaje najiona kama sina mchango wa maana wa kutoa japo nafikiri nibora nijaribu kadri vidole vinavyojituma kuandika kwa kuwa naamini kwa kufanya hivi pia ni kuongeza uwezo wa akili zetu kufanya vizuri na kuwaza mawazo mengine magumu na mazuri ya maisha yanayotusumbua. hivyo tusimpite bila chochot anaweza kujumlisha na kupata kitu.


mleta mada hajatueleza kuwa mlalamikiwa kabla ya kuumwa alikuwaje? hii hali ilianza baada ya kuumwa au kabla? nafikiri kama ni baada na kipindi anaumwa kuna uwezekano mkubwa hajapona bado na anahitaji matibabu zaidi na ni ushauri zaidi kuliko dawa.
ki ukweli anampenda mme wake na ndo mana haondoki ila kunadhamira ipo ndani yake inamlazimisha aondoke hapo na sivinginevyo.
wakati mwingie hivi vitu kwa akili zetu hatuwezi kwakuwa wakati mwingine kuna mazingira ya kishirikina na uchawi (mume bado mdogo na anaonekana wanawake wengi wangevutiwa kuwa naye na kama haitoshi fedha hana lakini anajali familia sasa unategemea nini?) hebu fikiria katika mazingira ya kawaida mdada tena mzuri anakuja anakwambia wewe hurogeki nishajaribu kukutoa kwa mkeo hautoki basi japo uwe day waka bado mbishi na cc wengine tushakuw wazee inakuwaje kwa mtoto kama huyu mwenye verosa ambayo kila mdada mdogo wa arusha anapenda awe nayo?
hivyo anahitaji ushauri lakini ili anayewashauri aweze kuwasaidia ni vizuri akapata maisha ya mwanamke ya nyuma kwa kuanza kwa wazazi wake kuanzia kuzaliwa kwake ,kukua kwake usichana wake na maisha yake kabla ya ndoa na hapa mama mzazi anatakiwa awe mkweli hata kama alishawahi kwenda kwa mganga ni vizuri hivi vitu vikawa wazi katika kutafuta kumaliza tatizo. lakini pia familia yake itazamwe tatizo hili halipo katika familia yake huko nyuma?
pia mtazamo huo utazamwe kwa mwanaume pia kwanini mwanamke anamkataa huwenda ana roho ya kukataliwa? 
kwa hiyo wote wanahitaji ushauri alimpaaje huyu mwanamke?
kingine tofauti ya elimu kati ya mwanamke na mwanaume inawezekana ikawa sababu ya mwanamke anajisikia unyonge na kunauwezekana anahisi mwanume wake anaweza kumwacha sasa ili asiumie anatafuta njia ya kujifariji ili likitokea jamii ielewe kuwa mwanamke mwenyewe alishamchoka mme wake. hivyo anahitaji kurudi shule tena na asiachwe akajisikia mnyonge.
tofauti ya maisha kati ya familia ya mwanaume na mwanamke inaweza kuwa sababu pia inayomuumiza mwanamke na kusababisha kutojiamini kwa kuwa na mwanume kama huyo msomi anapesa huku akiangalia kuna wanawake wa nguvu na shule zao nafedha zao hawana hivyo ajaimini.
lakini mwisho wa siku wanaume ndoa zetu (na maisha yetu tumeyafanya kama tamthilia hayapo kihalisia hii ni changamoto nyingine mpya katika maisha ya ndoa ) hatuendeshi familia kwa misingi ya malezi ya taratibu zetu. sisemi kuwa tuwe na ndoa za kizee kama za wazazi wetu bali tuziboreshe kutokana na mazingira yetu. mfano mtoto wa mvuvi anatakiwa aendelee kuvua lakin safari hii asitumie mtubwi bali boti iyendayo kasi yenye uwezo wa kubeba samaki wengi na yenye jokofu la kupozea. kwa kuwa ndio kazi aliyokulia. hivyo wanaume tunatatikiwa wakati mwingine tulee ndoa zetu kadri wazazi wetu walivyo kuwa wanaishi ila tukiacha mambo mabaya tuakongeza mazuri zaidi.
hebu fikiria una mume anabaki makalio wazi unategemea nini hapa au mechi haziwezi kila akija yeye na laptop wakati mwanamke ni mdogo anahitaji mechi na misisimko ya nguvu we umebaki unaita dear ,darling mechi za kuvizia na hasileti hamasa unategemea nini? unabaki kumlambalamba kama kama mbwa.
nisiwachoshe ngoja niishie hapa