Si Kila Mtu Ni Wakumueleza Matatizo Yako. - RAHA ZA KITANDANI

Si Kila Mtu Ni Wakumueleza Matatizo Yako.

Related image
….Hivi unafikiri unapomwambia mtu matatizo yako hivi unahisi ataumia kama wewe unavyoumia?…. Unahisi atapata uchungu kama unaoupata wewe?…..Unahisi atakuonea Huruma kama unavyojionea huruma wewe huruma?…….Ngoja nikwambie Wala haiko ivyo unavyodhani, mtu uyo unaemwambia matatizo yako hawezi kufikia kiwango cha uchungu unaoupata au maumivu yako unayoyahisi.
Rafiki yangu acha kutafuta kuonewa huruma, utajiumiza bure na kuwapa watu faida ya kukufahamu undani wako pasipo na msaada utakaofikia maumivu yako.
Wengi unaowaambia matatizo yako uishia kukutangaza kwa watu wengine kuwa wewe ni mdhaifu wa jambo fulani. Si wengi watoa msaada katika yale yanayokusumbua, kuwa makini sana unapokuwa unafikisha mambo yako kwa wengine……..
Embu kaa chini na Utumie utaratibu wa KUJISEMESHA MWENYEWE na kuifikia akili yako ya ndani ambayo itakupa faraja na kukutia nguvu na kuamka na nguvu mpya tena.
Jisemeshe na ujiambie matatizo yako mwenyewe kwanza kabla hujaenda kuwauzia watu gazeti la yenye maandishi yanayokuhusu wewe. Wewe ni wewe mwenyewe……..