Sehemu ya pili: Kwanini mwanaume anahamu zaidi ya kufanya mapenzi kuliko mwanamke!
August 27, 2019
Edit
Masaa yaliyopita nilianza kuzungumzia mada iliyokuwa na kichwa cha habari hicho hapo juu lakini hii yote ilitokana na malalamiko ambayo nimekuwa nikiyapata mara kwa mara kutoka kwa baadhi ya wanawake juu ya usumbufu wanaoupata kutoka kwa waume zao katika ishu ya tendo la ndoa.
Siyo siri hili ni tatizo ‘sirias’ na wanaume wasipokuwa makini nalo wanaweza kujikuta wanakimbiwa na wake zao. Jamani, mapenzi ni starehe lakini tufahamu kwamba, yakifanywa bila mpangilio yanaweza kuwa kero kwa wengine. Ni sawa na pombe, pombe ikinywewa kistaarabu ni starehe tosha lakini ikizidishwa kipimo ni matatizo.
Kama wewe ni mwanaume na umeoa au una mpenzi, tendo la ndoa lifanywe kwa mpangilio, kila mtu awe anajisikia kufanya hivyo ndipo lifanyike. Mwenza wako akiwa hajisikii na akakupa sababu za msingi, muelewe kwani huyo ni wako, baadaye ama kesho utakula vitu vyako.
Lakini sasa hii isiwe sababu ya wanawake kuwabania waume zao pale wanapojisikia kuwa nao faragha kwa kutoa visingizio vya hapa na pale. Tambua kwamba, kitendo cha mume wako ama mpenzi wako kujisikia kuwa na wewe faragha halafu akawa ni mtu wa kutoa sababu ili tu usimpe, yaweza kuwa sababu ya kumfanya atoke nje na kwenda kukusaliti.
Ndiyo! Atatoka nje na yawezekana akienda na akaonjeshwa vitamu zaidi huko asitamani kurudi tena kwako. Utabaki ukilia kwa penzi lako kumegwa na wajanja lakini chanzo ni wewe mwenyewe.
Ndiyo maana nasema licha ya utafiti kuonesha kwamba mume ana hamu zaidi ya kufanya mapenzi kuliko mke, kuna kila sababu ya wanandoa kuangalia njia sahihi za kukabiliana na hali hiyo ili isije ikatokea licha ya kupendana kwenu kwa dhati, tendo la ndoa likawatenganisha.
NINI KIFANYIKE?
Wenye hamu kubwa ya kufanya mapenzi ni sawa na wale wanaovuta sigara ama kutumia dawa za kulevya. Wapo ambao wasipotumia vitu hivyo kabisa huumwa na kukosa raha katika maisha yao. Watu kama hawa huwawia vigumu sana kuacha, lakini wapo ambao wamefanikiwa kuachana na vilevi hivyo kwa kuweka nia.

Kama wewe una hamu kubwa ya kufanya mapenzi labda kila siku mara nne au zaidi, waweza kujitahidi kupunguza na kufanya hivyo mara mbili kwa siku au mara moja tu.
Hali hiyo itakufanya ujizoeshe na kadri siku zinavyokwenda utajikuta ukiwa na hamu ya kawaida ya kufanya mapenzi ambayo haiwezi kuwa kero kwa mwenza wako.
Ila kama wanandoa watakuwa wakijikuta katika hali mbaya kuhusiana na hili ni vyema wakamuona daktari ili waweze kupatiwa msaada wa kitaalamu zaidi.

Tukumbuke tu kwamba, kufanya tendo la ndoa ni kitu cha furaha na cha msingi katika maisha ya ndoa, lakini inapotokea mwenza wako akasema anakupenda sana na angefurahi kufanya mapenzi ila kwa siku hiyo hajisikii vizuri, mwanandoa mwingine hapaswi kujuta, kulaumu ama kutishia kwenda nje ya ndoa, kama atafanya hivyo basi huyu atakuwa hatambui nini maisha ya ndoa na hatakuwa na busara.
Nimalizie kwa kusema kwamba, kuwepo na mwanandoa mmoja ambaye ana hamu kubwa ya kufanya mapenzi hakuwezi kuvuruga ndoa kama tu wanandoa watakuwa wana uelewa wa mambo.
Ila sasa tufahamu pia kwamba kufanya kitendo hiki ni lazima kuwepo na makubaliano, hakuna kulazimishana. Ni vizuri wakati mwingine kujaribu kuzizuia hisia zetu kwani kuendekeza kufanya mapenzi kila wakati ni kero ndani ya ndoa.