Long Distance relationship maswali ya kujiuliza! - RAHA ZA KITANDANI

Long Distance relationship maswali ya kujiuliza!


Umbali unaweza kuleta masikitiko. Lakini wakati mwingine  masikitiko hayo yanaweza  kupima utamu uliopo Na kuna maumivu ya moyo pia.
Huchukii mahusiano ya mbali . Ukweli ni kwamba, Unajikuta katika hali  ambayo unakutana na mtu sahihi kwa wakati mbaya.
Umbali huleta udhaifu, ndio kitu ambacho kinasababisha mahusiano yako yakose balance. Utajikuta unajiuliza, hii inafaa kweli?
Jiulize na mwenza wako ajiulize  maswali haya muhimu kama kweli mahusiano yenu yanaweza kupona  kutokana na umbali huu.
1.Wote mnakubaliana kujicommit?
Lazima wote mkubaliane . sio mmoja anavumilia na mwingine anaanzisha mahusiano  ya wazi upande mwingine. Matatizo yanaweza kutokea. Kwa sababu ya mmoja kuvumilia na mwingine kuendelea na mahusiano mengine. Mtasababisha  mfarakano.
2.Wote Mnaaminiana?
Siku za leo ambazo zina magonjwa mengi , unatakiwa kuaminiana na kuwa wakweli kwa nia moja  bila ya kufanya makosa. Na hio ni kwa ajili ya usalama wenu. Wivu ni sumu .
Matatizo yanaweza kutokea.Kama uaminifu utapotea na mwenza kuanza kuuliza uko wapi, unafanya nini, uko na nani. Na kama unasema ukweli kutokana na maswaili haya . kama anahisi kuwa huaminiki. Inawezekana kuna kitu unakifanya ambacho sio sahihi na sio salama ..
3.Wote mnawasiliana Vizuri?
Unaweza ukawa unaongea wazi na huru kwa mwenza wako ,  bila ya kuogopa tabia zako mbaya . utakuwa  unazoea  hisia mbaya  wakati ukiwa mbali. Ni vizuri kama mtaweza kuliongelea hilo.
Matatizo yanaweza kutokea. Mazungumzo yanaweza kuwa mafupi, na hutaweza kupata kitu cha kuongea na mwenza wako. Utaanza kuhisi kuwa mwenza wako hahusiki na kitu unachokifanya au hali iliopo. Kwa hio hamuongelee hayo.  Unatengeneza umbali.
Kwa sababu hio kutatokea wivu, kukosekana kwa usalama, na kukosa hisia kwa mwenza.
4.Mnakubaliana kutoa ulinzi ili kumsaidia mwenza?
Ina maana gani hapa?
Nguvu yako na uaminifu kwa mwenza unakuwa kwenye mazingira magumu sana kwa muda  huo wa majaribu. Wataweza kuhitaji  ulinzi zaidi kutoka kwako, ili kufahamu kama unajali kweli. Unahitaji kupata muda wa kuwasurprise , kumualika au kurudi kwake  mara panapohitajika  msaada huo.
Japo kwa mwezi mara mbili au moja. kama ni mbali sana hata kila baada ya miezi kadhaa  sio mbaya, kwa sababu ya commitment mliojiwekea.

# SHARE KWA WASHIKAJI