Unapendwa, Unaachwa tatizo ni nini? - RAHA ZA KITANDANI

Unapendwa, Unaachwa tatizo ni nini?


KUACHWA au kuachana kwa wapenzi si jambo la ajabu sana katika jamii, lakini inapotokea wewe unakuwa wa kuachwa kila siku, hapo ndipo kwenyetatizo. Ndiyo zao la mada hii. Kwa nini uingie kwenye uhusiano na kuachwa kila mara?Msingi wa mada hii ni wanawake, ingawa hata wanaume kuna wakati wanaachwa na wenzi wao. Rafiki zangu, pamoja na ugumu wa jambo hili, lakini inakupasa ukubali kwamba wewe ni tatizo.Kuufanya ubongo wako kukubali kuwawewe ni tatizo, utakuwa mwanzo mzuri wa kutafuta dawa. Ni jambo gumu kidogo kupata hekima ya kugundua jambo hili, lakini waliobahatika wanafanya maamuzi ambayo hayawaumizi mioyo yao.Haya mambo yanawezekana rafiki zangu. Kwanza ni kukubali kujifunza, kuangalia wapi ulikosea, ni kipindi gani wenzi unaochana nao wanapatwa zaidi na hisia za kukuachan.k. Baada ya hapo ni rahisi kusogea mbele zaidi katika kujua jinsi ya kutatua tatizo ulilonalo.Wapo wanawake wengi sana ambao wanahangaika kwa sababu ya kuachwa kila siku. Kila mwanaume anayekuwa naye, baada ya muda mfupi tu, anamuacha! Hajui tatizo, badala yake anaishia kulia tu.Kulia kwako hakutakusaidia lolote kama hutakaa chini na kujiuliza ni wapi kwenye matatizo, ni sehemu gani huwa unakosea.Una miaka ishirini na nne tu, lakini umeshakuwa na wanaume tisa! Hili ni tatizo, tena kubwa ambalo linahitaji dawa ya kuponya na siyo ya kutuliza maumivu. Twende darasani…
KUJIRAHISISHA…Kwanza jaribu kujichunguza kama una tabia ya kujirahisisha. Ni kweli umekuwa na tabia ya kujishusha thamani na kuona kama wewe ni kuonewa? Kuchezewa? Mwanaume mwenye ndoto na mwanamke wa baadaye wa maisha yake hahitaji mwanamke wa aina hii.Anapenda zaidi awe na mwanamke mwenye msimamo anayetambua thamani yake yeye mwenyewe na maisha yake kwa ujumla. Hapendi mwanamke mwepesi kuingilika. Kamautakuwa wa aina hii, hata kama atakuwa amekupenda, ataishia kukutumia na kukuacha, kwani wewe mwenyewe umejionesha wa namna hiyo.Mwanaume anapenda mwanamke wa kumsumbua kidogo, angalau baadayeapate stori za kusema; “Lakini mama nanilii ulinisumbua!”Huu ni ukweli ambao baadhi ya watu wanaukwepa. Acha kujirahisisha. Kujirahisisha huku ni pamoja na sualazima la kufanya mapenzi. Usiwe na haraka na tendo hilo, usiulizie juu ya kufanya mapenzi, lakini kama ikitokea jamaa akataka, usikubali haraka. Onyesha msimamo wako, ukiainisha usivyotaka kuchezewa.
JICHUNGUZE MWENYEWEWakati mwingine mambo yako yasiyotamanika yanaweza kuwa chanzo cha wewe kuachwa na wenzi wako kila wakati. Angalia tabia zako, tizama mienendo yako, marafiki, kauli na kila kitu ambacho unadhani kinaweza kuwa tatizo.Mwanaume hapendi kuwa na mwanamke ambaye ana kampani mbaya, kwani anaamini na wewe pia inawezekana ukawa na tabia chafu kama rafiki zako, lakini kauli nzuri kwa mwenzi pia ni kati ya mambo ambayo mwanaume mwenye nia ya kuoa atavutiwa navyo. Jichunguze!
VIPI, UNAJALI?Kujiona wewe ni bora kuliko wanawake wote hakukusaidii, sana sana kunazidi kukurudisha kwenye matatizo yale yale kila siku. Mwanamke ambaye hajali na haoneshi umakini wakati akizungumza na mpenzi wake, hana sifa ya kuwa mke.Kama ni kweli unataka kuwa mke, lazima uwe makini, uoneshe kujali kwako na kumuona mwenzi wako kila kitu. Mheshimu, mpe nafasi ya kwanza, hiyo inaweza kuwa safari nzuri ya kuelekea kwenye mafakio.Jifunze unyenyekevu, ukikosea kuwa wa kwanza kuomba msamaha, kubali kusamehe na hakikisha kwamba unakubali kufundishwa unapokosea. Usiwe mtu usiyejali, ambaye upo tayari kwa lolote, hata kama ni kuachana na mwenzi wako. Hii ni kati ya sumu hatari zitakazokufanya uishiekuachika kila siku.
UNASHAURIKA?Tabia ya kung’ang’ania mambo ambayo mpenzi wako hapendi ni kati ya sababu zinazotosha kabisa kukufanya uachike. Inawezekana mpenzi hapendi aina fulani ya mavazi,tabia fulani mbaya na amekuambia kwa nini hapendi lakini wewe ukaendelea kung’ang’ania. Hili ni tatizo.Acha uking’ang’anizi, jaribu kuwa muelewa. Mwenzi wako anapokataa kitu na kukueleza sababu za msingi, msikilize na kama unaona anachokuambia hakifai basi mjibu kwa hoja na siyo kumuwekea kiburi.
DHARAUWanawake wenye dharau wapo katikanafasi kubwa zaidi ya kuachwa na wapenzi wao. Utakuta mwingine dharau zake zinazidi mipaka mpaka kwa ndugu wa mpenzi wake. Wakigombana kidogo, anaweza kutajahata wazazi au ndugu wa karibu na mpenzi wake.Ni mwanaume gani anayependa kuishi na mwanamke mwenye mdomo mchafu? Mwenye dharau? Anayeamini kila kitu anaweza mwenyewe? Sifa ya kwanza ya mwanamke ni heshima, kama mwanamke huna heshima basi fahamu kwamba huwezi kuishi na mwanaume hata siku moja.Katika maisha ya ndoa kati ya mamboya msingi ambayo huzingatiwa na wengi ni pamoja na kila mmoja kukubalika na ndugu wa pande zote, sasa itawezekana vipi wewe kuolewa ikiwa hata hao ndugu wenyewe unawadharau? Unawadhalilisha kwa maneno makali? Itawezekana vipi?Mwanamke lazima uwe na heshima, uwe na haiba ya kike, siyo unaishi mradi siku zinakwenda. Kama huwa unaachwa kila wakati, chunguza tabiahii nayo inaweza kuwa chanzo cha wewe kuachwa!
UNAITAMBUA NAFASI YAKO?Baadhi ya wanawake huwa hawataki kutambua na kutumikia nafasi zao, mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanaume kwa kila kitu. Hata kama kwa bahati mbaya mmetofautina, kama mwanamke ambaye anatarajiwampenzi wako aje kuwa ‘kichwa cha nyumba’ yako, lazima uonyeshe unyenyekevu.Tulia, msikilize kwa makini, hata kamani yeye amekosea, usitumie kauli chafu ambazo zitamuudhi. Zungumzanaye kwa staha ukitambua nafasi yake. Wakati mwingine wanawake wenyewe wanasababisha waachike. Usikubali kuwa hivyo!
KURUDIA MAKOSAHakuna binadamu ambaye hakosei. Inaelezwa kwamba, kukosea ni sehemu ya ukamilifu wa mtu. Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema: “Ni vizuri watu wakosee ili wajifunze, huwezi kujua kitu bila kukosea, lakini unaruhusiwa kukosea mara moja tu!”Kama ukichambua neno moja baada ya lingine la Mwanasaikolojia huyo, utaweza kuona jinsi sentesi yake fupi ilivyo na maana kubwa. Kwa mantiki hiyo hata kama utakosea mara mia moja, hakuna tatizo, lakini yawe makosa mapya. Kosea kila siku, lakini kitu kipya, hii inamaanisha kwamba, kwa sababu kukosea ni kujifunza, basikama utakosea mara mia, utakuwa umejifunza pia mara mia moja. Upo hapo?Sasa wanaume wengi hawapendi wanawake ambao wanakosea na kusahau! Jenga utaratibu wa kuheshimu unachoambiwa; Ukielezwahakifai, usikaidi, huna sababu ya kurudia tena.Kurudia kwako mara nyingi ni kuzidi kumkera mwezi wako ambaye lengo lako hasa ni kuishi naye hapo baadaye.
BADILIKAKama hayo yote hapo juu yanakuhusuni wazi kwamba unatakiwa kufanya mabadiliko ya haraka sana katika maisha yako, kama ni kweli unataka kuolewa. Siyo rahisi mwanaume ambaye anatafuta mke akakubali kuwa katika uhusiano na mwanamke mwenye tabia zako.Anza taratibu, rekebisha moja baada ya lingine, halafu kuwa makini katika kila jambo, mwisho wake utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupata mwenziwa maisha.-GPL