SABABU ZINAZOPLEKEA WANAUM KUTOKA NJE YA NDOA ZAO - RAHA ZA KITANDANI

SABABU ZINAZOPLEKEA WANAUM KUTOKA NJE YA NDOA ZAO



Wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kutoka nje ya ndoa ambapo kwa zamani ilikuwa si kitu cha kawaida  na hata walipokuwa wanafanya ilikuwa inafanyika kwa siri sana, lakini  sasa hivi imekuwa ni jambo la kawaida na inawezekana kila mtu akajua na hata mke wake  anapojua kwa mwanaume anaona ni kitu cha kawaida tu.
Inawezekana kuwa mwanaume anafanya makusudi kufanya bila kuwa na sababu ya kufanya hivyo.unaweza usimuelewe mtu anapokwambia sababu za yeye kuchepuka lakini kitu chochote kinapozidi ufanya mtu kuchoka na kutafuta mbadala.
mapenzi.
Inatokea kuwa mwanaume anaona mwanamke wake amtoshelezi kimapenzi kabisa na kila akijitahidi kumrekebisha ni kama vile hamuelewi kabisa.kwenye mapenzi kuna ubunifu na vitu vingi vinavyoitajika ili kumridhisha mwenzi wako hivyo pale mwanaume anapoona kuwa kila siku wewe ni yuleyule ndipo anapotafuta kupya.
kisasi
Mwanaume mwingine sio msemaji kama mwingine, anapohisi kuwa mwanamke aliyenae anamahusiano ya nje anachofanya  yeye ni kulipiza bila kuwa na uchunguzi , na hata kama itakuwa ni uongo kwa mwanamke endapo mwanaume atajaribu nje na kuona utofauti basi ujue mwanaume huyo tayari ameshapotea.
mabishano ya kila siku.
wanaume wengi sio waongeaji kama wanawake, linapotokea jambo dogo ni vigumu mwanamke kulinyamazia tofauti na mwanaume ambae huweza kukaa nalo muda mwingi kwa sabau tu hataki kuongea sana, hivyo inapotokea kuwa kila baba akirudi nyumbani basi lazima kesi zianze ni lazima atatafuta ambapo akienda anakaribishwa na utulivu na mahaba tele.
mapishi.
Hii pia huwa ni sababu kubwa sana wanaume uwafanya kuhama nyumba zao,baba anakuwa anachika kula mapishi yale yake kila siku.Mara nyingine chakula kinakosa radha, muda mwingi jikoni anashinda dada wa kazi, mwanaume anaamua kula hotelini na siku akichoka akaonja mapishi tofauti tu basi shoga baba unampoteza.
kubadilika na kuwa sio kama zamani.
Nadhani kuna muda unafika mwanamke anakuwa namzoea sana mumewe kiasi kwamba kuna vitu alikuwa anafanya mara ya kwanza anabadilika na kuacha kuvifanya tena.Anaweza kuwa sio msafi kama zamani, lugha zake sio nzuri tena, hamjali tena mwanaume wake , hii itamfanya mwanaume kwenda kutafuta mambo hayo sehemu nyingine.