Jinsi Ya Kuishi Katika Mahusiano Marefu Na Mpenzi Wako
July 27, 2019
Edit
Read More
- Kuwa na nafasi binafsi.Katika mahusiano, yawe mapya ama ambayo yameshamiri, lazima uwe na nafasi yako binafsi. Hii inatumika kwa yeyote ambaye hayuko single. Kama mnaishi pamoja basi unahitaji kuwa na nafasi ya kuwa kivyako. Hakikisha kuwa unameet na marafiki zako, nenda kafanye mazoezi, soma vitabu ili mradi tu unakuwa na uhuru wa kufanya mambo kivyako.2. Chagua vitu vya kupigania.Kama mmekuwa mkiishi pamoja na mpenzi wako, kufikia sasa najua kuna mambo mengi ambayo unayajua kumhusu mpenzi wako unayoweza kuyatumia dhidi yake, jambo ambalo si zuri.So badala ya kugombana kila wakati kuhusu mambo madogo madogo, ni bora kurudi nyuma na kufikiria ni mambo gani muhimu ambayo yanahitaji kupiganiwa.3. Mazungumzo yaendelee kunawiri. Wengi katika mahusiano huchukulia kuwa wamekuwa katika mahusiano muda mrefu na wapenzi wao hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kuwasiliana na wapenzi wao. Unachohitajika nikuendeleza kiwango cha mawasiliano na mpenzi wako muda wote. Usibahatishe hata mara moja.4. Tokeni deti. Kutoka deti kuna umuhimu kwa kuwa mnapata kukumbana na mambo mapya. Mpenzi wako atafurahia kwa kuwa unaleta misisimiko mipya katika maisha yenu. Hivyo kumtoa mpenzi wako deti kuangalia sinema, mkahawa ama kwenda katika sehemu za kujipumbaza kunafungua maisha mapya kati yenu.
- Usitarajie chochote.Ukimsapraize mpenzi wako na ua ama zawadi yoyote hupaswi kutarajia chochote kutoka kwake. Kuwa katika mahusiano hakumaanishi kuwa ukitoa unapaswa kunufaika, la. Wewe unapaswa kutoa ili umfurahishe mpenzi wako. Inaonyesha kuwa unamkubali mpenzi wako, na watafurahi katika mahusiano yenu.