Fahamu siri hizi ili kusaidia uhusiano wako kuwa bora zaidi - RAHA ZA KITANDANI

Fahamu siri hizi ili kusaidia uhusiano wako kuwa bora zaidi




Kuna watu hutumia muda mwingi kutafakari namna ya kuboresha uhusiano wao na wenzi wao, hii sio kwa uhusiano uliovunjika tu (kutengana), hata ambao bado uhusiano wao ni imara itawasaidia pia.                 Inawezekana hata wewe ni mmoja kati ya watu wanaojiuliza kuhusu wanandoa wengine, “kwanini wao wanakuwa na furaha muda wote”? Ondoa wasiwasi sababu hapa nimekuandalia siri za uhusiano wenye furaha daima ili kukusaidia nawe kuwa katika uhusiano imara na kuwa na furaha muda wote.

1. Kuwa na muda mwingi wa kuwa pamoja

Jaribu kutenga muda wako kwaajili ya kuwa nae. huna budi kupanga tarehe nzuri na mahali mtakapokwenda, unatakiwa kufanya hivyo ili kuhakikisha kila mmoja wenu anafikiria kuhusu muda huo ili isitokee shida ya kuvunjwa kwa ahadi.

2.Wasiliana nae wakati wowote

Kutokana na utandawazi na tekinolojia kurahisishwa siku hizi ni rahisi kuwasiliana, iwe kwa kumpigia simu au kumuandikia ujumbe mfupi wa maneno (text) mara moja moja hata akiwa kazini mkumbushe kuwa unampenda.

3. Shirikiana nae bega kwa bega wakati wote

Ni rahisi sana kama kweli unampenda, kushirikiana nae katika wakati mgumu na nyakati za furaha hufanya uhusiano wa karibu kati yenu wawili.

4. Mkumbatie (kumbatianeni) mara tu mnapoonana

Hakuna haja ya kuficha hisia zako pale tu unapokutana na mwenzi wako baada ya kutomuona kwa muda.

5.Jipende wewe binafsi kwanza

Unahitaji jinsi ya kujua kujipenda wewe mwenyewe kwanza kabla ya kuanza kuwapenda wengine, na usisahau kuwa mkweli kwako mwenyewe.

6.Tengeneza kumbukumbu zenu za pamoja

Hii itakusaidia unapoangalia kumbukumbu za nyuma mlipokuwa pamoja unaweza kukumbuka kumbukumbu nzuri badala ya kuzingatia nyakati mbaya au ubaya anaokufanyia.

7.Usiruhusu mwenzi wako asahau wewe ni nani kwake

Mwandikie barua, na ujitahidi kumpa au kumuandalia zawadi ndogo ndogo mara kwa mara ili kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo pamoja nae. Vile vile itasaidia awe na uwezo wa kukutofautisha wewe na watu wengine.

8.Kila mmoja kuwa na furaha na mwenzie

Kufanya kitu kizuri pamoja kunaongeza furaha kwenye uhusiano. Jaribu.

9.Mfurahie mwenzi wako

Maisha ni mafupi sana, kitu muhimu ni kufurahia uwepo wa kila mmoja katika maisha. Kuliko kupoteza muda wako usifurahi wakati wowote.