ETI MKEO NI KAMA GOGO MUWAPO KITANDANI, KWA HIYO? KWA NINI UMTANGAZE? HEBU SOMA HAPA UJIFUNZE - RAHA ZA KITANDANI

ETI MKEO NI KAMA GOGO MUWAPO KITANDANI, KWA HIYO? KWA NINI UMTANGAZE? HEBU SOMA HAPA UJIFUNZE



Wiki hii nataka kuzungumzia tabia f’lani ambayo imejengeka kwa baadhi ya wanaume ambayo kimsingi ni mbaya na haileti picha nzuri lakini naamini kwa kuandika kupitia safu hii, itasaidia kuwafanya wahusika wabadilike.


Natambua umuhimu wa watu kukutana sehemu mbalimbali na kubadilishana mawazo, haijalishi ni eneo gani ambalo litatumika. Wapo ambao stori zao huzipigia baa na wengine maskani tu.Hukondiko tunakojadili mambo kadha wa kadhayanayogusa maisha yetu ya kila siku. Miminadhani ni jambo la msingi sana kwani naamini watu zaidi ya mmoja wanapokutana na yanayozungumzwa yakawa ni yenye maana, ni lazima yatakuwepo mabadiliko chanya kwa wahusika.
Lakini pamoja na yote hayo, nimegundua kuna baadhi ya wanaume wanapokuwa kwenye mazungumzo kama hayo huingia pia katika kuzungumzia maisha yao ya kimapenzi na baya zaidi ni kwamba, badalaya kuzungumzia mambo mazuri huingia kwenye kuzianika kasoro walizonazo wapenzi wao. Jamani huu si ulimbukeni uliopitiliza?Yaani wanafanya hivyo wakiwa na imani kwamba eti kwa kuzieleza kasoro hizo, wenzao watawasaidia katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao. Unaweza kumsikia jamaa akisema mbele za watu; “Unajua kuna kitu kinaniumiza kichwa sana washikaji, mpenzi wangu hayajui kabisa mapenzi, yaani nikiwa naye faragha naona kama niko na gogo vile!” Labda nikuulize wewe msomaji, kwa mtu mwenyebusara anaweza kweli kuanika kasoro hiyo kwa wenzake?
Mimi mwenyewe naamini katika ushauri nikitambua kuwa, kupitia ushauri ninaoweza kuupata kutoka kwa watu wangu wa karibu naweza kupata mwanga wa kufanya maamuzi sahihi lakini siamini kama kupitia vikundi vyenye mchanganyiko wa watu naweza kupata ushauri mzuri hasa ninapokuwa na matatizo yanayohusu maisha yangu ya kimapenzi.Jamani, mapenzi ni mambo ya siri hivyo ni vema yakaheshimiwa na ifike wakati basi tuchuje yale ambayo tunastahili kuyanadi mbele za watu kuhusu wapenzi wetu na mengine yabaki kuwa siri ya wewe na mpenzi wako. Hapo ndipo heshima ya penzi inapopatikana.
Yako mambo mengi ya mpenzi wako yasiyostahili kusemwa mbele za watu, lakini muhimu kabisa ni masuala yote yanayohusu tendo la ndoa, kasoro za kimaumbile hasa za mwili, uwezo wa kuelewa mambo na elimu hasa inapokuwa ya chini. Migogoro ya ndani, hitilafu za kitabia na dhiki mnazokabiliana nazo hazitakiwi kabisa kutoka nje ya kuta za chumba chenu.
Athari za kutoa siri za ndani zipo nyingi kwani uchunguzi unaonesha kwamba sababu nyingi za kusalitiana na kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi hutokana na kuvuja kwa siri za ndani za wapenzi. Ikiwa mwanaume atatangaza jinsi mpenzi wake asivyotosheka na tendo la ndoa au namna mkewe anavyoongoza kwa usaliti sina shaka wafitini watapata pa’ kuanzia.Hivi kuwaambia washikaji zako kwamba mpenzi wako hajui mapenzi unataka wao wamfundishe au anataka wakushauri uachane naye? Ukishamuacha je? Labda nikufahamishe tu kwamba, wapo marafiki zako ambao wanaweza kukushauri uachane na mpenzi wako lakini baada ya kumuacha wao wakamchukua.Niseme tu kwamba, kama mpenzi wako si mtundu wala mbunifu suluhisho si kumtangaza kwa wenzako bali wewe ndiyoutakuwa na jukumu la kumuelekeza katika hili na lile na mwisho wa siku naamini atakuwa bora zaidi.