Hakuna maana moja ya kumuelezea mwanaume, ila kwa aliye mwanaume nadhani anaelewa nini maana ya kuitwa mwanaume, mara nyingi wanawake huwa wanaonekana wao ndio wanaonewa sana na wanaume na ni vigumu sana kujua manyanyaso ya wanaume sababu wengi huwa hawayaongelei, wanawake wengi huwaongelea wanaume kwa ujumla yaani kuwafananisha wote katika kundi moja. lakini kuna mtu na mtu kila mtu ana tabia zake na wanaume wana tofautiana, sina maana ya kutetea haki za wanaume ila kuna fikira potofu kuhusu wanaume ambazo watu wanatakiwa kuzitoa akilini.
Mwanaume halii.
Mwanaume akionekana analia ataitwa dhaifu, ama hajakuwa bado mtoto, lakini ukweli ni kwamba hata wanaume wana hisia wana umia na wana mioyo kama wanawake, wao sio maroboti japokuwa inachukuliwa kuwa mwanaume anayaeweza kuvumilia maumivu ndio jasiri bila kujua sio kila anaye lia kwa machozi ni mnyonge. Kuna usemi wa mwandishi Malorie Blackman alisema “Boys don’t cry, but men do.” katika kitabu chake cha Boys Don’t Cry.
Wanaume Wakorofi.
Wapo wanawake wengi wameumizwa na vitendo vya kikatili kutoka kwa wanaume zao, ndugu zao na marafiki, kupigwa na kuteswa na wanaume zao, lakini si kweli wanaume wote wakorofi na wanadharau wanawake au watoto, wapo wanaume wanaojali na kuheshimu wanawake pia.kuna mtu alisema ukitaka kujua mwanaume mwenye hekima tazama heshima yake na mapenzi yake kwa mama yake.
Wanaume hawafanyi Kazi za Nyumbani.
Kazi za nyumbani sikuzote huonekana ni za wanawake tu,ni mara chache usikie baba anaandaa chakula kwa ajili ya familia yake hata kama baba huyo amesomea Mapishi na ana Degree, lakini wapo wanaume wanaosaidia wake/wapenzi wao wakiwa nyumbani, kama ni kufua kupika na kuosha vyombo wapo wanaojua nini maana ya kusaidia kazi za nyumbani.
Mwanaume ndiye Anaepanga Maamuzi juu ya Mwanamke.
Sikataii wapo wanaume wa aina hii, wao wanapanga kila kitu, yeye ndo atakwambia fanya hivi na usifanye hivi kitu ambacho si kila mwanaume anafanya, wapo wanaojali maamuzi ya wenza wao na kuheshimu mambo yao, tusiishi kwa mazoea.
Wanaume Wanapenda Michezo.
Hapa sanasana mpira wa miguu, nilishangaa siku moja nilimuuliza mshikaji mmoja anapenda timu gani ya mpira wa miguu alinijibu kirahisi tu ye si mpenzi wa mpira wa mguu , nilishangaa lakini ukweli wapo wanaume ambao sio wapenzi wa mpira wa miguu, ni kawaida kukutana na watu tofauti.