Nimfanyeje Huyu Mwanamke wa Kiarabu, Hebu Nishaurini Wakuu
June 28, 2019
Edit
Mwenye uzoefu ni mkubwa kuliko wewe, hata kama umri umemzidi. Haya basi nishauri wewe mwenye uzoefu.
Ni hivi, niliwahi kuishi mkoa fulani miaka 3 iliyopita na mwaka jana nilihamia Dar es Salaam kikazi na makazi ya kudumu kabisa. Huko nilikutana na mwanamke 1 wa Kiarabu tukaanzisha mahusiano na yakadumu kwa muda mrefu. Aliniambia yeye ni single mother kwa mtoto 1 wa kike na kwamba aliolewa lakini ndoa haikudumu. Nilimuamini.
A short while later kuna bwana 1 ambaye alikua anamfahamu sana yule mwanamke akanitonya kuwa ni mke wa mtu!!! nilishtuka sana...mana hakuwa na dalili zozote na kila nilipomuhitaji alifika bila kukosa na hata simu niliweza kumpigia muda wowote na anapokea wala tabu hakuna. Wanawake wana siri hawa...haki ya Mungu! Yule jamaa aliniambia mpaka sehemu mumewe anapofanyia kazi. Ni mwarabu mzee kidogo., mtu mzima kama 50+ hivi. Umri wa mzee wangu kabisa.
Ilibidi nimwite bidada na kumhoji vizuri ndipo akafunguka ana mume na watoto 2, badala ya yule msichana ninayemjua mimi there is a boy, first born, miaka kama 8 hivi anaishi Dar. N kwamba mumewe ana wake 2 na yeye ndio bimdogo. Niliishiwa pozi kabisa. Roho iliniuma as if mi ndio nagongewa mke wangu. Lakini sikuilaumu nafsi yangu, nilimlaumu yeye. Nikajisemea huyu anaweza kuniuwa huyu. Niliazimia kumuacha.
Sasa bidada huyu amekuwa akinisumbua kila mara akitaka turudiane. Eti nimtoroshe kwa mumewe nikamfiche kokote kule yuko radhi. Nimekomaa aniache mimi hataki. Ever since sijamla tena na sitaki hata kumuona. Akija Dar mara nyingi anaforce tuonane, I refuse. Nimekuwa nikifuta namba yake lakini yeye atanitafuta tu hata iweje. Anaweza kukaa hata miezi 6 lakini kuna siku atanitafuta tu. Na story zake ni kuwa amenimiss. Mwezi wa 6 nilimsema sana na kumponda mno anavyotaka kusaliti ndoa yake na kumpa maneno ya MUNGU nikijua atanichukia na kushika njia yake, but in vain.
Leo jioni hii kanipigia, anasema sasa hana ndoa ameachika rasmi na kwamba yuko Morogoro tangu October so kama vipi tuendelee na yetu! Imani naye sina.....nikiri tu ni mzuri na sijawahi kuona mwanamke msafi kule maeneo yetu kama yeye. Na sina namna yoyote ya kuprove maneno yake....
Nikijicheck niko lonely kinyama nyama. Hivi ushawahi ng'ang'aniwa na mwanamke kama hivi?
Huyu ananipenda au kitu gani?