Jinsi Ya Kumuapproach Mwanamke Katika Gari La Abiria
June 29, 2019
Edit
Najua kuna baadhi ya watu ambao washawahi hujaribu na kufaulu (kawaida unafaulu asilimia 100 kila wakati), so somo lenyewe ni kuapproach mwanamke katika gari la usafiri la abiria.
Ok, hebu tuanze hivi, ni mara ngapi ushawahi kuingia katika basi ukakutana na mwanamke mrembo ukamtamani? Ama ni mara ngapi ukiwa ndani ya gari ushawahi kumwona mwanamke mrembo ameingia na kukaa mbele yako? Ni mara nyingi. Mambo kama haya hutokezea kila siku. Mwanzo kila siku unapoabiri basi huwa unakutana na wanawake tofauti tofauti na warembo. Na je, unajua mbinu ya kuwaaproach uanze mazungumzo? Somo letu litafafanua kwa upana.
Wanawake wakiwa ndani ya magari ya usafiri huwa rahisi kuwaaproach tofauti na sehemu nyingine unazozijua. Hii ni kwa sababu ya mambo haya:
1. Kinga zake ameziweka chini. Katika gari za usafiri mwanamke huwa hayuko katika hali ya kutangamana, so hatakuwa na mawazo katika akili yake kama vile anavyokuwa katika kilabu. Mfano hafikirii mbinu za kukabiliana na wanaume wanaoudhi ama kuwa na wasiwasi wa kwanini hakuna mtu mpaka sahizi amemuaproach. Nguvu zake zote katika gari la usafiri huwa zimetulia ukilinganisha na wakati ameenda kula bata na marafiki zake usiku. Katika hali hii huwa ni rahisi kumuaproach na anaweza kuungana na wewe kirahisi bila matatizo.
2. Gemu huwa ya juu. Katika magari ya usafiri wanawake ni wengi mno. Kila siku ukisafiri utakutana na wanawake tofauti. Wale ambao utakutana nao leo, si wale ambao utakutana nao kesho. Hii inamaanisha kuwa kadri utakapokuwa ukisafiri ndipo utakapokuwa na nafasi nzuri ya kuchagua mwanamke unayetaka wewe.
3. Una mstari ambao unafanya kazi kila wakati. Kuanza mazungumzo na mwanamke ni rahisi katika magari ya usafiri. Sentensi kama, "Unasafiri ukielekea wapi?" Tayari inaweza kuamsha mazungumzo yasiyokuwa na mwisho.
Ok. Hapo juu tumeonyesha sababu muhimu ambazo zinafanya kuapproach mwanamke katika gari la usafiri kuwa rahisi kuliko zote.
Kuna aina tatu za kumtambua mwanamke abiria. Nazo ni kama zifuatazo:
Hali #1 Mumesimama nje ya gari la usafiri unangojea kuingia ndani ukamwona mwanamke unayempenda. Katika hali hii mara nyingi hutokea katika basi. Abiria wote wako nje wanangojea kuabiri basi, halafu ghafla ukakutana na mwanamke unayevutiwa. Hatua ya kufanya hapa ni rahisi. Unachotakiwa kuanza ni kwenda hadi pale alipo, simama karibu yake halafu umwambie, "Waah, leo abiria ni wengi/wachache. Hivi unaelekea wapi?" Hapa atakujibu bila wasiwasi wowote sababu kinga zake zote ameziweka chini (sababu tumeeleza hapo juu).
Sasa mazungumzo yenu hayaishi hapo nje, lazima uingie ndani ya gari. Sasa hapa kuna changamoto kidogo. Kama unaingia ndani ya gari ambalo kiti unajichagulia mwenyewe utakuwa umefaulu kumnasa. Kama tayari mumepewa tiketi ambayo kila mtu ameandikiwa kiti chake itakuwa vigumu kuendelea na appraoch kwa huyu mwanamke kama kiti chako ni nambari 12 na yeye ni 35.
Turudi kwa kujichagulia kiti mwenyewe; Wakati mnapoingia kwa basi, unamwambia maneno kama, "Mi hupenda kuketi katika viti ya katikati, ingekuwa bora tukae katika viti vya nambari 23 na 24." Ukimwambia maneno kama haya hawezi kupinga. Mwanzo ushajitokeza kama mwanaume alpha, jambo ambalo wanawake wanapenda.
Ama unaweza kutumia mbinu nyingine nzuri ya kumwonyesha sehemu ya kuketi kwa kutumia ishara. Mfano wakati mnaingia ndani ya basi, elekeza sehemu unayotaka akae, mwambie, "kaa hapa sehemu ya dirisha." Akishaketi sasa wewe unafuatilia. Hii ni mbinu nyingine rahisi ya kufuatilia.
Hali #2 Unaingia ndani ya gari la abiria halafu unamwona mwanamke amekaa pembeni akiwa pekeake. Hapa moja kwa moja unaenda kukaa sehemu alipo. Anza na mstari wa, "Unaelekea sehemu gani?" halafu mazungumzo yaanze na hapo.
Hali #3 Umekaa nyuma ya gari, ghafla mwanamke mrembo akaingia na kukaa viti vya mbele pekeake. Hatua kama hii unapaswa kuwa mjanja. Jambo la kufanya ni kuhakikisha kuwa mwanamke aina hii hakukuona. Hakikisha hajaona sura yako. Akishaenda kukaa kwa kiti sasa unaweza kubeba ujasiri wako na kuaproach sehemu alipo. Hapa lazima ufahamu mambo mawili. Kwanza ni kuwa ukienda kukaa sehemu yake lazima atajua kuwa ulikuwa ndani ya gari so lazima uwe na sababu za kwa nini umeenda kukaa na yeye. Pili ni kuwa usipojieleza ukaeleweka unaweza kumfanya mwanamke kama huyu kuziamsha kinga zake hivyo ukakosa kila kitu. So hivi ndivyo unavyopaswa kusema wakati umekaa na yeye, "Kule nyuma kuna joto na unarushwarushwa kila wakati, nimekuja hapa mbele angalau nafeel kibaridi na hewa safi." ama "Nimekuona ukiingia kwa hili gari nikaona si vizuri kumwacha mwanamke nadhifu kama wewe ukae pekeako, waendeleaje lakini?"
Mazungumzo ukiwa katika gari la abiria ni rahisi sana. Mwanzo unazungumzia kuhusu gari lenyewe na kampuni inayomiliki, unazungumza kila kitu kuanza mwenendo hadi mwishio, unaongea kuhusu sehemu unayoenda na uliyotoka, vitu mnavyokumbana navyo barabarani nk, yaani mazungumzo hayana mwisho.