Je Wanawake ni Mabingwa wa Kuzuga Kitandani? - RAHA ZA KITANDANI

Je Wanawake ni Mabingwa wa Kuzuga Kitandani?

Image result for kelele kitandani

Kama wewe nimwanaume, basi bila shaka unafahamu ile milio na miguno ya wanawake wakati wakujamiiana, na kama wewe ni mwanamke pia unafahamu kwamba huwa unatoa milio namiguno hiyo. Ni nini basi kinachopelekea milio na miguno hii kutolewa? Je miliona miguno hii ni ya kweli au ni zuga tu, ili kumfanya mwanaume ajisikie "kijogoo"?

Baadhi ya wataalamuwa masuala ya kujamiiana na mapenzi walijiuliza pia maswali hayo. Mwaka jana,Gayle Brewer wa Chuo Kikuu cha Central Lancashire na Colin Hendrie, wa ChuoKikuu cha Leeds waliibuka na utafiti wao waliouita "Copulatory Vocalization"(kwa tafsiri nyepesi-"Milio/sauti za kujamiiana"). Katika utafiti huo,waliuliza wanawake 71 ambao wanashiriki tendo hilo mara kwa mara (sexuallyactive) kati ya umri wa miaka 18 na 48 kwa ajili ya kupata undani zaidi wasuala hili la kutoa milio wakati wa kujamiiana.


Wataalamu haowaliweza kubaini kwamba wengi wa wanawake hao walikuwa wanatoa milio, lakinisio tu wakati wanafika kileleni (orgasm), bali 66% walisema walitoa milio, ilikuharakisha wanaume zao kufika kileleni, na 87% walisema kwamba walitoa milio,ili kumfanya wanaume ajisikie "Kijogoo" (boost his self-esteem).

Wataalamu haowaliongeza kusema kwamba "Wakati mwanamke kwa kawaida hufika kileleni wakati wakutomasana, mara nyingi milio ya kujamiiana imeripotiwa kutokea mara kwa marakabla au sambamba na wakati ambao mwanaume anafika kileleni". Walisema pia katikautafiti wao imebainika kwamba wakati mwingine wanawake walitoa milio na miguno,ili kukabiliana na kuboheka, uchovu, na maumivu wakati wa tendo la ndo, kwahiyobasi wanaume inabidi kuwa makini kwani wakati mwengine kumbe mtoto wa watu anaumia! Au pengine yupo kwenye zile harakati za kukuzuga, ili ujione "Kijogoo"?

Wataalamuwanaendelea kusema kwamba tatizo kubwa ni kwamba jamii imefanywa kuamini kwambamilio wakati wa tendo la kujamiiana huusishwa na mwanamke kufika kileleni au kufurahia tendo hilo, kiasi kwamba imefikiawanawake kuona ni busara kudanganya (fake) kwamba wamefika kileleni (wakijuafika kwamba mwanaume tayari ana amini hivyo) wakati kumbe hawajafika popote.

Wataalamu wanaonyakwamba sio busara kwa wanawake kudanganya kwamba wamefika kileleni, kwanikufanya hivyo kunapelekea wanaume kufikiri kwamba wanafanya kila kitu sawawakati wa mapigo, wakati kumbe sio. Mwalimu wa elimu ya kujamiiana, PattyBrisben, anashauri kwamba wanawake watumie 
miguno/miliokama "njia ya kuonyesha kwamba wanafurahia tendo, lakini sio njia ya kufichakama tendo hawalifurahii."


Kuficha au kutokuficha, wataalamuwanasema kwamba suala la kutoa milio/miguno wakati wa tendo la kujamiiana siosuala la binaadamu peke yao, utafiti kwa wanyama umebaini kwamba hata manyanijike (baboons) hutoa milio fulani kabla au wakati wa tendo hilo. Nyani jikehutoa milio fulani kuhashiria kwa nyani dume kwamba yupo tayari kwa tendo hilona pia manyani jike huongeza milio wakati wanajamiiana na nyani dume, ambae anacheo katika kundi lao (higher-ranked male baboon). Zaidi ya hayo, nyani jikeaina ya "Macaque" amebainika pia kutoa milio/miguno wakati wa tendo hili nyeti,ili kumfikisha mwenza wake kileleni haraka!


Mwisho wa yote wataalamuwanamalizia kusema kwamba suala la kuridhishana kimapenzi (tuite "ukijogoo" wamwanaume au vinginevyo), ni suala muhimu kwa pande zote mbili, yaaani mwanaumena mwanamke. Kwahiyo basi, suala la kutoa milio sio tu suala la mwanamke kudanganyaau kufanya mambo asiyotaka, bali ni suala la kuwepo "hai" (sexually present)(mara ngani umeshasikia wanaume wa kitanzania wakilalamika kuhusu wanawakewanaokaa kama "gogo" au "kusoma gazeti" wakati wa kujamiiana??) wakati wa tendohilo na kubadilishana mahaba na mwenza wake. 


Mwisho kabisa, wanasema, "wote(wanaume na wanawake) tutoe milio!" 

Je unakubaliana na utafiti huu?