CHANZO CHA USALITI KATIKA MAPENZI
June 22, 2019
Edit
1;TAMAA YA MTU MWENYEWE Kuna watu wana hulka tu binafsi ya kutoweza kuwa na mpenzi mmoja hivyo ni vema kufahamiana zaidi kabla ya kuamua kuingia katika mahusiano. Wanasayansi pia wamethibitisha kuwa inawezekana kabisa mtoto kurithi tabia mojawapo toka kwa mzazi. 2;SIFA AU UMAARUFU Hii hutokea kwa aina ya watu ambao huona sifa kuwa na wapenzi tofauti na wanaume kutaka kuonyesha ana nguvu na hata mamlaka juu ya wengine. Utasikia mimi pale tayari na hamna kitu akihadofthia wenzake. Na pia wanawake hona fahari kuwa na watu maarufu,wenye fedha,cheo na yeye kujigamba khwa mtu flan maarufu kamuweka mfukoni. 3;KUTORIDHISHWA KIMAPENZI Hali hii hutokea zaidi kwa wanawake kwa sababu ya maumbile yao kiasili ingawa pia wanaume pia hutokea. Katika hili wote mnatakiwa kuwa wabunifu na kujua mpenzi wako anapendelea nini,mjitahidi kuwa wasafi na mkiwa mnataka kukutana basi muwe wote na utulivu wa akili na bila kusahau kula vyakula vya kuongeza nguvu mwilini. 4;TAMAA Hapa tunaongelea mahitaji mbalimbali ya kimaisha kama fedha,nguo,chakula,cheo nk. 5;KULIPIZA KISASI Hili hutokea mmoja wa wapenzi anapogundua mwenzi wake kamsaliti basi naye huamua kama moja ya njia ya kupunguza machungu ni kutoka nje ya mahusiano na hapa utakuta anaweza fanya mapenzi na hata rafiki wa karibu kwa lengo la kumkomoa