๐Ÿ’๐ŸŒบNDOA๐ŸŒบ๐Ÿ’ Usitarajie Raha Katika Ndoa Bila Karaha. - RAHA ZA KITANDANI

๐Ÿ’๐ŸŒบNDOA๐ŸŒบ๐Ÿ’ Usitarajie Raha Katika Ndoa Bila Karaha.

Read More

๐Ÿ’๐ŸŒบNDOA๐ŸŒบ๐Ÿ’ Usitarajie Raha Katika Ndoa Bila Karaha.

Usitarajie Kila Kitu Kiwe Shwari Katika NDOA  bila Misukosuko.

Usitarajie Kushiba,Kuvaa,Kuoga Bila ya Kukosa cha Kutia Kinywani Au Kuvaa Mwilini ni jambo la Kawaida Katika NDOA.

Usitarajie Aliyekuoa au Uliyemuoa Awe Mkamilifu Utakavyo Wewe! Bila  Shaka Utie Akilini Kwamba Chochote Kizuri kina Ubaya Na Kinyume Chake.

Usitarajie Kubembelezwa katika Ndoa Bila maneno Makali Bila Manung'uniko katika Ndoa. Bila Shaka Kuna Kusutwa,Kupigwa,Kufukuzwa na Hata Kuchukiwa.

Usitarajie Vyote Katika NDOA Ni vyenye Kukufurahisha kuna Vile Vya  Kuhuzunisha Kukutia Majonzi Kukupa Mihangaiko Mfadhaiko na Kukutupa Katika Lindi La Mawazo.

Usitarajie Kupata Mzuri Safi,Mwenye Hekima Na Busara Katika Ndoa. Kuna Wenye Hasira  Bila Busara Wenye Midomo Mikali Mno Wenye Kupungukiwa Kwa Uwezo WaKutafakari.

Ndo Maana NDOA ni Chuo Ni Ibaada Na Kila Ibaada Inataka Uvumilivu Wa Hali Ya Juu Mno.

*Sote Tuvumilie Katika NDOA zetu. ALLAAH๏ทป  atupe Moyo Wenye Kusubiri.*


Related Posts