SIMULIZI FUPI: CHOZI LA MILELE
September 03, 2019
Edit
MTUNZI : IDDI SIRAJ
Binadamu unapozaliwa tu uhai wako na amani yako huishi kwenye mikono ya mama alie kuzaa japo mungu anakuwa ndio mlizi mkuu wa maisha yako.
Mama anapo amua kukufupishia uhai wako anaweza kutimiza kwa dakika chache haijalishi kwa kukupa sumu au kuziba pumzi kwa muda mrefu hii itategemea ni jinsi gani amekusudia kukufupishia uhai .
Wasichana wengi huchukua jukumu la kuharibu na kuzitoa mimba zao zinapokuwa changa kwa msukumo wa mazingira yaliyo mpelekea kupata mimba ile ama kwa sababu ya ugumu wa maisha na mazingira magumu anayo ishi,.
Wasichana wengine huenda mbali na kufanya maamuzi magumu pale anapo ilea mimba miezi tisa na kujifungua salama baada ya hapo humtupa mtoto na kumuacha katika mazingira hatarishi nae anaondoka na kutokomea, hufumba macho na kuyasahau mateso ya kutunza mimba ndani ya miezi tisa na yale machungu ya kujifungua .
Sijui ni ujasiri gani wanao utumia akina mama au ni roho mbaya kiasi gani wanayo kuwa nayo wakati ule wanapo watupa watoto walio wazaa wenyewe tena kwa uchungu....na sikitika sana kwani hata mama yangu alinitupa nikiwa mtoto mdogo mchanga akiniacha mazingira hatarishi .
Mungu msamehe mama yangu na wanawake wote wanao toa mimba na kuwatupa watoto....
Mimi ni Baraka matata. mwandishi na mtunzi wa simulizi hii ni ndugu Iddi Siraji na imehaririwa na Lizbertha Maseke.
sasa isome na ujifunze.
Jina la baraka nilipewa na yule mama mgumba baada ya kuniokota nikiwa mtoto mchanga na kunifanya kuwa mwanawe mpendwa wa pekee na kwa hakika alinipa upendo ambao ulipindukia na alinipa malezi ambayo yalistahiki kwa kila mtoto japo alikuwa na maisha duni akijishughulisha na kilimo akiwa na mumewe mzee matata.
Yalikuwa ni maisha duni ya kutegemea kilimo cha mkono lakini baba na mama yule walijitahidi kunisomesha kwa kidogo kilicho patikana huku nami nikifanya bidii kwenye masoma na kuwasaidia kilimo kila nilipo rudi kutoka shule,.
Siku zote mama alinihimiza nisome kwa bidii kwani elimu ni urithi wa milele.
"Mwanangu nipo tayari kuuza hata mashamba ili mradi tu usome na ufike mbali...unadhani nisipo kupa elimu utapata urithi gani wa thamani pindi nikifumba macho" aliongea kwa kunisisitizia na kunifanya niwe makini sana ninapo kuwa darasani.
Mbali na kuwa saidia kulima wazazi wangu nilikuwa nina bustani zangu za mboga ambazo kila jumapili nilienda kuuza sokoni na kujipatia pesa ndogo zilizo niwezesha kununua vifaa vya shule na mafuta ya taa ya kibatali changu cha kusomea usiku.
Hatimae juhudi zangu zilizaa matunda ni pale tu nilipo faulu kwa kishindo kutoka la saba kwenda kidato nilikuwa mwanafunzi wa pili kati ya wanafunzi sita wa kwanza akiwa ni mtoto wa kike wa mwalimu mkuu wa shule ile ilio kuwa chini ki elimu na uhaba wa walimu.
Mama na baba mzee matata walifurahi kupita kiasi nina uhakika furaha yao ilizidi ya kwangu, waliuza mazao yaliyo patikana msimu ule kisha pesa iliyo patikana walininunulia vifaa vya shule na kunilipia ada ya shule kwani kipindi hicho cha mwaka 2005 elimu haikuwa bure kama sasa.
Hatimae siku zilifika nikajiunga na wenzangu katika shule ile ya sekondary....Bado mama alinisisitizia kuhusu swala la kujituma katika elimu huku safari hii akinisihi sana nijiepushe na makundi ya vijana wasio na maadili , nami nilizingatia hayo, siku zika songa nikijituma kwenye masomo pamoja na kazi za nyumbani.
***--**
Kama ilivyotokea mwaka 2005 basi ndivyo ilivyo jirudia mnamo 2009 kwani kwa mara nyingine nilifanikiwa kuziweka ndoto zangu mahala pazuri kwa kufaulu kutoka kidato cha nne kwenda cha tano.
Safari hii furaha yangu haikudumu sana kwani iliyayuka baada ya kujua kwamba kulikuwa na uwezekano wa kutoendelea na masomo kwa sababu ya ada kubwa na shule niliyopangiwa ilikuwa mbali sana.
Wazazi wangu wapendwa hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama zile, nilijikuta nikikata tamaa machozi yakinitoka kila siku zilivyo karibia za kujiunga na kidato cha tano.
Siku moja baba aliniletea karatasi kadhaa na kuniambia ni chukue kalamu kisha nijaze ma swali ya form ile kisha niambatanishe na cheti changu cha kidato cha nne,
nami nilifanya vile nikajaza karatasi ile ilio sheheni maswali yalio nihusu mimi na elimu yangu , baada ya kufanya hivyo baba aliichukua barua ile na cheti changu na kuuondoka navyo bila kuniambia anapeleka wapi hii ni kawaida yake mzee matata huwa haweki mipango yake wazi hivyo sikutaka kujisumbua kumuuliza.
Baada ya siku sita tangu nijaze barua ile tulipokea ugeni wa watu ambao hakika walitoka serekalini tukawakaribisha,
"naona mmekuja mabwana...kijana mwenyewe ndio huyu" mzee matata aliongea baada ya kusalimiana na watu wale huku akinielekezea kidole mimi.
watu wale waliniuliza maswali kadhaa yenye misingi ya elimu wakijenga maada ya juu ya masomo ambayo huwa naya fanya vyema .
Nami niliwajibu kadri nilivyo weza.
walipo ridhishwa walitazamana na kuafiki
"Ok mzee matata mwanao atajiunga kwenye hiyo shule kwa msaada wa kitengo chetu hivyo aanze maandalizi" aliongea mmoja wa watu hao na hapo nilishindwa kuivumilia ile furaha iliyo ripuka ghafla kwenye moyo wangu.
Mzee matata alikuwa amefanya jitahada kubwa sana kwa kwenda kuomba msaada wa mimi kusomeshwa na alifanikiwa watu wale niliohisi wa serekalini walimkubalia nami nilitakiwa nikajiunge na wenzangu kwenye ile high school tena nilitakiwa nikaishi bweni.
Huo ndio ulikuwa msaada mwisho wa mzee matata!! msaada katika mafanikio yangu kwani nikiwa nipo shule miezi tisa tangu niondoke nyumbani nililetewa taarifa mbaya yenye kuumiza moyo wangu mzee matata alikuwa kapata ajali ya kugongwa na gari ! maskini mzee matata aliaga dunia na kumuacha mama mjane huku akiniachia kilio cha aina yake.
Nililia sana baada ya kupokea habari ile na uongozi wa shule ukanifanyia msaada wa usafiri wa haraka ili niwahi mazishi.
Hayati mzee matata tulimzika katika hali ya udhuni iliopindukia huku akimuachia mama kilio kisicho bembelezeka.
Baada ya kumzika baba yangu mpendwa sasa macho yangu yalimuangalia mama yangu mpendwa ambaye nae hali yake kiafya haikuwa nzuri alikuwa kanyongea sana tena alidhohofika, hali ile ilinifanya nisitamami kurudi shule nikae kumuuguza mama yangu mpendwa, lakini mama alilipinga hilo na kuniamuru nirudi shule niendelee na masomo huku akidai udhoofu ule alionao ni sehemu ya ukiwa wa kufiwa na sio ugonjwa
Maskini mama kipenzi alipenda sana nisome kuliko kitu kingine , sikuwa na pingamizi kwani mitihani ilikuwa imekaribia ikanilazimu nirudi shule na kumuacha mama akilelewa na wanakijiji.
Wakati nikiendelea na mitihani shuleni nililetewa taarifa kuwa hali ya mama sio nzuri amelazwa hosptal hii ikanilazimu kumalizia mitihani haraka kisha nikarudi kijijini kwenye hospital aliyo lazwa mama.
Hali ya mama haikuwa nzuri hata kidogo alikuwa taabani akisumbuliwa na maradhi ya moyo bila shaka ni kutokana na kifo cha baba.
Nikiwa na muuguza mama hospitalini pale siku moja alfajiri iliniita jina langu nami haraka nikaitika.
"Mwanangu baraka kunakitu nataka ni kujuuze leo hii" aliongea ni kauliza ni kitugani mama ?
"Unajua nilimpenda sana baba yako mzee matata na nilimkabidhi moyo wangu wote kwani ni wazi yeye pia alinipenda sana pengine kupita mimi kwani alikubali kuhama na mimi na kuondoka mkoa alio zaliwa akiepuka maneno ya ndugu zake walio mshawishi aniache na aoe mwanamke mwingine kwani mimi nilikuwa ni mgumba nisie weza kushika mimba" mama aliongea na kunyamaza kidogo kisha akaendelea"
"mzee matata hakukubaliana nao kabisa akahama nami kutoka mkoa aliozaliwa, ndugu zake wasijue tume hamia wapi .baba yako alinipenda sana kufikia hatua ya kukubali kuishi nami bila kupata mtoto lah! mzee matata alikuwa na upendo wa kweli kwangu.
siku moja usiku nilitoka nje kukojoa kukiwa na hali ya mvua, na wakati narudi ndani nilisikia sauti ya mbwa akiunguruma huku akiburaza kitu nilipuuzia na kutaka kurudi ndani lakini hapo nikasikia chafya ya mtoto mchanga haraka nikawasha kurunzi yangu yenye mwanga hafifu nikasogea upande huo ! masikini nilikuta kuna mtoto mchaga akisukwa sukwa na mbwa akiwa katupwa nilimfukuza mbwa huyo kisha nikamuita mzee matata tukamchukua huyo mtoto na kuingia nae ndani kwani mvua ilikuwa imeanza kunyesha bila ya mimi mvua ile ingechukua uhai wa mtoto au mbwa ange mdhuru mtoto huyo tukampa jina la BARAKA na kukufanya kuwa mwanetu mpendwa ukiwa ni baraka kutoka kwa mungu" Moyo wangu ulipata mshtuko mkubwa sana na kukumbwa na simanzi mara dufu baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa mama na muda huo mama aliendelea kunisimulia
"mama yako alikuzaa akakutupa akiwa anaona hufai ila sisi ulitufaa japo hatuku kuzaa ila tulikufanya kuwa mwanetu ....baraka mimi sio mama yako ila nakupenda sana"
kufikia hapo nilikuwa na lia tu huku nikiwa siamini kuwa yule sio mama yangu kilio kile kilichukua takribani dakika ishirini
"HAPANA MAMA WEWE NA MZEE MATATA NDIO MLIO NIZAA HAYO MANENO SIYAAMINI NAKUPENDA MAMA" niliongea huku nikilia lakini mama alikuwa kimya... naaam kimya cha milele!! alikuwa amesha iaga dunia akiniacha na chozi la milele.
Tayari mama alikuwa amefariki.
Mama yangu alitangulia mbele za haki akiniacha kwenye kilio kikubwa nililia sana zaidi ya unavyo fikiri msomaji, mbaya zaidi mama alikuwa amefichuwa siri nzito kuwa mimi waliniokota , swala lile liliniumiza sana ni bora asingeniambia kwani mimi nawajua wao ndio wazazi wangu na mpaka leo hii naandika haya moyo wangu una kiri kuwa wale ni wazazi wema japo hawakunizaa.
Ulikuwa ni msiba mkubwa sana kijijini pale , nae mama tulimzika karibu na kaburi la mumewe mpendwa mzee matata.
Baada ya mazishi yaliyo hudhuliwa na watu wengi huku waalimu kadhaa walio nipenda wakishiliki mazishi yale kisha nikarudishwa shuleni ili nika pumzike bwenini kwani pale kijijini sikuwa na ndugu mwingine tofauti na wazazi wangu walio tangulia.
Hapo shuleni nilipewa wiki tatu za kupumzika kabla ya kurudi kwenye masomo...sikuwahi kuwaza kumtafuta mama yangu alie nizaa na kunitupa ila mara nyingi nilijiuliza ni kwanini alinitupa na kuniacha mazingira hatarishi .
Nilirudi tena kwenye masomo huku hali yangu kiafya ikiwa sio nzuri lakini nilijikaza kuushinda wakati ule wa majonzi
nilifanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha tano na sita na nilifaulu kwa matokeo mazuri kwenda chuo kikuu cha dar es salaam.
Jiji la dar nilikuwa nalisikia tu kwenye vyombo vya habari lakini sasa nilipata nafasi ya kwenda kimasomo huku gharama zote zikisimamiwa na watu wale walio tafutwa na hayati mzee matata .
Miaka mitatu ya chuo ilinitosha kuhitimu vyema masomo yangu na kufikia hatuwa ya kuajiriwa kwenye kampuni ya wale wadhamini walio ni somesha huku asilimia ishirini na tano ya mshahara wangu wakichukuwa wao kama fidia .
Yalikuwa ni mafanikio ya haraka sana kwani watu wengi huhitimu chuo kisha hupata tabu kwenye swala la kuajiriwa , nilishukuru sana kwa mungu huku nikiukumbuka msaada wa mzee matata , nilisikitika sana kwani wazazi wale walio nilea vyema walikufa bila kuyaona mafanikio yale.
mshahara wangu wa kwanza niliuchukua na kwenda kijijini kujenga makaburi ya wazazi wangu wa pendwa na kuyaacha katika hali nzuri kisha pesa ilio bakia nikawagawia majirani ambao walikuwa bega kwa bega kwa mama yangu hadi umauti ulipo mfika, baada ya hapo nilirudi mjini ili kundelea na kazi.
Tayari nilikuwa nimesha fanikiwa kujenga nyumba kubwa na kuna msichana nilikuwa nime muoa, msichana huyo nilimkuta katika maisha ya kifukara akiishi na mama yake kwenye nyumba waliopanga baba yake akiwa alisha kufa. yeye na mama yake walikuwa kwenye maisha magumu lakini moyo wangu ulipendezwa na binti yule nika muoa na kufanga nae pingu za maisha.
kama wasemavyo wahenga ukipenda boga penda na ua lake, basi nilipo muoa binti yule nilimchukua na mama yake nikaishi nao nyumbani kwangu .
Msichana yule aliyeitwa joyce alikuwa mke mwema kwangu aliniheshimu na alinipenda sana .tulifanikiwa kupata mtoto wa kiume nae nikamuita MATATA ,
Siku moja tukiwa wote mama mkwe na mimi na mke wangu niliamua kuwasimulia juu ya maisha yangu kwani walijua mimi ni yatima lakini hawakujua mengi ya maisha yangu.
Siku hiyo niliwasimulia tangu nilipo tupwa na mama alie nizaa nyuma ya ua wa mzee matata kisha nikaokotwa na wazee wale wakanilea.
stori ile ili wahudhunisha sana wakanipa pole, lakini nilikuwa nimefanya kosa kubwa kuwasimulia!!!!
Ilikuwa ni siku ya pili tangu familia yangu niisimulie kuhusu maisha yangu , siku hiyo niliwahi sana kutoka kazini nikanunua zawadi za mwanangu na mahitaji ya mama watoto. lakini nilipo fika nyumbani furaha yangu ili yayuka na kuzitupa chini zawadi zile , kwanza nyumba ilikuwa kimya kabisa tofauti na siku zote na nilipoingia ndani nikakutana na balaa.
Kwanza nili muona mke wangu akiwa kalala sakafuni na mama mkwe alikuwa kalala kwenye kochi mwanangu matata akiwa kalala pembeni yake.
Loh! hii sijawahi kuona usingizi namna ile itawezekana vipi wasinzie fofofo muda ule wa saa kumi za jioni!
Haraka nikamsogelea mke wangu na nikamgusa kujaribu kumuamsha lakini hakuamka kabisa na mwili wake ulikuwa wa baridi!! , hata mama mkwe nae ile vile vile hadi mtoto wangu na wote wale hawakuwa wao ila ilikuwa ni miili yao tayari wamesha fariki.!!!!
Nilichanganyikiwa sikujua nini kimetokea ila niliona karatasi ikiwa mkonomi mwa mama mkwe nikaichukua ilikuwa ni barua haraka nikaifungua na kuisoma.
Ndani ya barua ile nilikutana na jambo zito tena ilikuwa ngumu kuliamini na kulikubali kwani aliye iandika barua ile alikuwa ni mama wa mke wangu, aliandika kwamba yeye ndie yule msichana alie mtupa mtoto nje ya ua wa mzee matata !!!!!!, " Mwanangu kweli malipo ni hapa hapa duniani naona hata aibu kukutazama mwana nilie kutupa kisa ulikanwa na baba yako, jana ulipo simulia stori ya maisha yako nimejihakikishia kuwa wewe ndiwe nilie kutupa kisha nikakimbilia dar es salaam kuishi na mwanaume ambae na tulizaa huyu joyce ulie muoa naweza sema umemuoa dada yako ila wakulaaniwa ni mimi ...nisamehe kwa maamuzi nilio yachukua ya kuondoka na familia yako lakini nimefanya haya kwa kujiepushia aibu kwani wewe na mke wako ni mtu na dada yake japo baba tofauti ...nisamehe sana mwanangu ama hakika aibu kubwa imenikuta"
LA haullah! yule ndie alikuwa mama yangu. kwa mara nyingine niliangusha kilio kizito cha kuipoteza familia yangu machozi yalinitililika naam MACHOZI YA MILELE ama hakika hili ni CHOZI LA MILELE.
MWISHO....