Pesa! Pesa! Ndani ya mahusiano.
September 07, 2019
Edit
Upendo ni hisia halisi za hiari toka ndani ya moyo wa mtu kwa mtu ampendaye mbali napesa. Natambua kuwa unatambua jinsi ambavyo ni vigumu kuulinda upendo ili udumu kuwa hai. Usipokuwa makini hatua zote za mwanzo na juhudi zote ulizotumia kuupata zaweza kuwa ni bure, kama utakubali pesa iingilie upendo wako kwa umpendaye. Waweza kujiuliza mwenyewe utafanya nini wakati pesa itakapo ingila upendo wako?.
Wakati matatizo yanapo ibuka kwa mara ya kwanza ni lazima ujiulize “kuna uhusiano gani kati yangu na pesa?” pesa yaweza kuwa na maana tofauti tofauti kwa watu wengi na hivyo hupelekea kwenye mada ngumu saana kuhusu pesa. Usipokuwa na pesa kabisa ni lazima uwe na hofu kubwa saana. Ukiwa na pesa saana napo ni taabu, je pesa humaanisha nini kwako?.
Pesa haiwezi kabisa kununua upendo nafahamu hata wewe unalitambua hilo, pesa na chombo cha biashara, unapo ingiza pesa kwenye upendo maana yake ni kwamba unafanya upendo wako kuwa biashara. Ni kweli kwamba pesa ni muhimu katika maisha yetu, huchukua nafasi kwenye mifuko yetu, hutusaidia tuwe na afya njema lakini haina nafasi yoyote katika mioyo yetu.
Katika kila mahusiano, kuna uwiano kati ya majukumu na nguvu ama uwezo. Mmoja wenu anaweza kuwa ana nguvu saana kuliko mwingine katika kutoa maamuzi au mwingine akawa ndiye mnyonge saana katika mahusiano yenu katika mahusiano yenu. Uwiano sahihi katika mahusiano ni jambo muhimu saana ni kama tu mzani. Ikitokea mwingine amemzidi mwingine katika uwiano wenu hapo shida huenda ikatokea.
Changamoto za kiuchumi ni kitu kibaya saana katika mahusiano, madeni, uoga, ukaidi ni miongoni mwa vitu vinavyo haribu saana uwiano huu katika mahusiano yenu na hatimaye hali ya amani yaweza kutoweshwa. Hali ya kutoaminiana yaweza kuanza kuibuka. Kukatishana tama kunaweza kufunika upendo wenu wa dhati. Hofu na uoga ni sumu mbaya saana katika kuaminiana kwa wapenzi
Pesa ni kitu ambacho husuluhusha matatizo yote ambayo mwanadamu aweza kuyapata nje ya yale ambayo ni ya moyoni. Pesa ukiipata hata namna ya kufikiri hubadilika. Lakini changamoto za kifedha hutowesha kabisa hata amani katka mahusiano, pesa hufunika kabisa changamoto za ndani kabisa za mtu, hutowesha kabisa upweke na aibu. Kukosekana kwa pesa hupelekea kila mtu katika mahusiano kupambana na hali ngumu ya maisha na hivyo pesa huathiri hata mfumo na uwiano sahihi katika mahusiano.
Katika siku hizi mahangaiko ya kutafuta pesa na hali ya kutokuwa na kazi vina athiri saana uwiano sahihi na upendo halisi kwa wapendanao. Hivyo zinahitajika juhudi nyingi saana ili kurudisha nguvu inayoshikilia upendo wenu, la sivyo hali yaweza kuwa mbaya katika mahusiano yenu.
Yatafakarini maisha mnayoyaishi kwa mtazamo mpana saana. Pesa yaweza kuwafanya mtengane, lakini ki msingi ni kitu cha kupita tu. Angalieni maisha yenu ya baadaye! Na wala si ya leo na kesho tu. Kumbushaneni kwa pamoja malengo yenu na maamuzi yenu mliyojiwekea.
Malengo ya baadaye mliyojiwekea ndiyo yatawapa mwanga wa kupambana na changamoto ambazo zinawapata kwa muda tu, malengo hayo yatawafanya mpate suluhisho la changamoto mzipatazo. Songeni mbele huku mkiangalia malengo yenu.
Kwa pamoja, ongeeni kwa upole na upendo kuhusu hofu inayowapata juu pesa mkitumia uwezo mlionao kwa wakati huu. Furahini kwa kuwa pamoja katika wakati huu mnao upitia, chekeni pamoja maana kicheko hubadili giza kuwa mwanga, mshike kwa upendo mwenzi wako kila wakati wote kama ishara ya mapenzi ya dhati katika kipindi kigumu mnachopitia.
Ifanye ahadi ya upendo wako kwa mwenzi wako kuwa mpya kila wiki au kila siku. Kama wewe umeolewa au umeoa ahadi yako uliyo itoa siku ya harusi yako endelea kuifanya kuwa mpya. Kama bado unamtafuta na bado hamja oana, endelea kumuonesha kuwa umpendaye kuwa yeye ni wathamani kuliko chochote kile.
Mara nyingi saana pesa humomonyoa na huweka kutu katika chuma cha upendo, pesa ni changamoto kubwa saana ya upendo wa dhati. Pia pesa ni nguvu ambayo yaweza kuleta hali ya kutoelewana katika mahusiano kama hatutaweza kuitumia vizuri.
Wapenzi wapya au wale walio wachanga katika mahusiano ni rahisi saana kupatwa na changamoto hii ya pesa katika mahusiano yao kuliko wale waliyo na uzoefu au wale waliyo ishi pamoja kwa muda mrefu. Changamoto ni kitu cha kawaida. Uchumba au kuchunguzana ni kama mtu ambaye anachagua bidhaa dukani, kujaribu na kumchunguza mwenzi ambaye anafaa ni jambo la muhimu saana kabla ya kuoa au kuolewa. Chunguza jinsi mchumba wako huyo anavyo tumia pesa, itakusaidia saana kutambua jinsi ambavyo mchumba wako huyo atakavyo kuwa baadaye, kuwa mwangalifu saana. Je anatumia pesa kwa uangalifu?. Je anaweka akiba kwa ajili ya baadaye au ndiyo anazitumia na zinaisha?
Leo ni kawaida kabisa kuwa na hofu juu ya Hali ya kiuchumi katika familia nyingi, hili haliepukiki. Kila mmoja ana mzigo wa kufanya pesa nayo haitoshi, dunia nayo haijiwezi kila siku tunashuhudia hali ya kutokuwa imara kiuchumi je hali hii katika mahusiano yako unaichukuliaje?