Mambo 10 Muhimu ya kufahamu kwa Mwanamke kabla hujaamua kupoteza Bikira yako
August 07, 2019
Edit
Tafsiri ya bikira inatofautiana kwa kila mtu.
Jambo la kwanza kufahamu kwa wewe mwanamke mwenye bikira ni kwamba maana ya bikira inatofautiana inategemea na mtu husika kwa mfano, wengine bikira humaanisha kutoingiliwa kingono kwa mwanamke, wengine humaanisha kutojihisha na mapenzi kwa namna yoyote either njia ya uke au mdomo (oral sex). Kwa vyovyote ambavyo unaweza kuelezea bikira basi yapaswa kufahamu kwamba una maamumuzi ya kupanga lini uvunje bikira yako. Na pia kumbuka kwamba siyo kitu kibaya kuvunja bikira maana inakufungulia mwonekano mpya wa maisha ya kuanza kujihusisha na ngono ambapo mwanzo haikuwa hivo.Utando laini kwenye uke haupasuki kwa ngono pekee.
Naamini kama wewe ni bikira ama hujawahi kujihusisha na vitendo vya ngono basi umewahi kusikia kuhusu utando laini unaoziba uke, Kwamba utando huu hupasuka wakati uume unapoingia kwenye uke kwa mara ya kwanza. Ukweli ni kwamba tishu hii haipasuki wakati wa tendo pekee bali hata kwenye shuguli zingine za kawaida kama mazoezi na kazi znto.Kwahivo usipate mawazo pale ambapo hujaona damu ikitoka wakati unafanya tendo la ndoa kwa mara ya kwanza.Mwili hautabadilika baada ya kupoteza bikira yako
Baada ya kufanya ngono kwa mara ya kwanza basi kumbuka mwili wako hautabadilika kwahivo usipate hofu. Japo kutawepo na mabadiliko kidogo ya kisaikolojia kwa upande wa hisia za kimapenzi kama- Mashavu ya uke kuongezeka
- Wakati fulani kasi ya kupumua kuongezeka
- Ngozi kuwa ya moto
- Kupata jasho sana
- Kumbuka dalili hizi ni za muda mfupi tu kutokanana na hisia za kimapenzi unazokuwa nazo kwa wakati husika na zitapotea baada ya muda flani.
Huwezi kutambulika na watu kwamba umetoka kufanya ngono
Baada ya kumaliza kufanya ngono aidha kwa mara ya kwanza kutokana na kwamba siyo kawaida yako basi unaweza kuwa na hofu labda watu watajua kwamba umepoteza bikira yako kwa kukutazama machoni. Jibu ni hapana, watu hawawezi kukujua kwenye macho kwamba umepoteza bikira yako labda uwaambie, kwa maana ingine hakuna mtu atajua kwamba wewe sio bikira tena.Kufanya ngono haitakuwa kama vile unavyoangalia kwenye tv ama pono
Wanawake wenye bikira hufikiri kwamba siku ya kwanza wanapoanza ngono basi ufanyaji wake utakuwa kama kwenye TV wanavyoangalia au video za ngono hapana. Kila mmoja hufanya tendo hili kwa namna yake. Kwahivo usidangaywe na vido unazoona kwenye mtandao ama kwenye TV. mengi huwa ni maigizo.Tendo lako la kwanza hutafurahia lakini halitakuumiza.
Ni kawaida kwa mwanamke kutofurahia tendo pale anapofanya kwa mara ya kwanza. Msuguano hutokea pale uume unapoingia kwenye uke wako kwa mara ya kwanza na inaweza kukupelekea kutojiskia vizuri. Kama ukipata maumivu wa tendo la kwanza basi ni wazi kwamba hukuandaliwa vizuri ama uke wako ni mkavu hauna majimaji. Kama maumivu yakiwa ya mara kwa mara inaweza kuwa una uvimbe kwenye kizazi na unatakiwa kumwona dactari.Utahitaji kuandaliwa kabla ya tendo na uke wako utaloa
Kwa mwanamke pale unavonja bikira fahamu kwamba kwenye kila tendo utakalofanya baada ya hapo uke wako utalowa majimaji ambayo kazi yake ni kulainisha njia ili uume upite kiurahisi, na pia fahamu kwamba utahitaji kuandaliwa kwanza kabla ya kufanya ngono.Magonjwa ya zinaa huambukizwa kupitia aina yoyote ya ngono
Kwasababu tayari umeanza kujihusisha na vitendo vya ngono basi fahamu kwamba unaweza kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa endapo hutakuwa mwagalifu kwenye mahusiano yako. Magonjwa ya zinaa husambaa kwa aina yoyote ya ngono iwe kupitia uke, njia ya haja kubwa, au ngono kwa mdomo. Inashauriwa kutumia condom kwa kila tendo ili kujikinga na maambukizi haya.Unaweza usifike kileleni siku ya kwanza
Naamini umekuwa ukisoma na kuambiwa na wenzako kuhusu swala la kufika kileleni. Kitendo ni hali ya mwanamke kutosheka kimapenzi baada ya tendo la ndoa. Kutokana na kwamba siku ya kwanza utakuwa na woga na pia kuhisi maumivu wakati wa tendo, hutaweza kufurahia ngono kwahivoo hutaonja ile ladha ya kutosheka kimapenzi ama kufika kileleni. Lakini usohofu maana kadri unavoshiriki zaidi ngono ndivyo utakavokuwa mzoefu na utaweza kujua mbinu mbalimbali za kimapenzi. Fahamu pia kadri unavorelax na kuweka akili itulie ndipo itarahisisha kufika kwako kileleni.Kama hukufurahia tendo siku ya kwanza, unaweza kufanya vizuri siku zijazo.
Kwa mwanamke amabaye amevunja bikira yake siku ya kwanza unaweza kutofurahia tendo kama ambavyo ulisimuliwa na marafiki zako. Kama ulicholipata kwenye tendo siyo kile ulichotarajia basi fahamu kwamba unaweza kujaribu tena na tena siku zijazo na ukafurahia ngono. Kadri unavofanya ndivyo unakuwa mzoefu na kuwa fundi kwenye tendo la ndoa.