Zifahamu sifa kumi za Mpenzi au Rafiki wa kweli - RAHA ZA KITANDANI

Zifahamu sifa kumi za Mpenzi au Rafiki wa kweli


Nivigumu kumtambua kuwa ni Mpenzi au Rafiki wa kweli, Japokuwa kuna tabia ambazo hazijifichi maishani kwa mtu mkweli na mwongo. Ndio maana nikaona nivyema ku share na wewe Sifa kumi ambazo zinaonekana mara kwa mara kwa Mpenzi au Rafiki wa kweli.
  1. Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo asaidie au atoe. 
  2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .
  3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri .
  4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuacha mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
  5. Mpenzi/rafiki wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa nyuma na kukuacha bila msaada .
  6. Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule atakayekupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)
  7. Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine 
  8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli .
  9. Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .
  10. Atakuwa tayari kuvumilia hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu au ubabe. Ni hayo tu jipeme na umpime umpendaye!