Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 9)
July 04, 2019
Edit
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 9
Ilipoishia...
"Mjinga mkubwa shusha Silaha yako haraka kabla sijamwaga ubongo wako, huna mtu wa kumtisha hapa, uko peke yako tuko zaid ya kumi teremsha bastola yako kwa usalama.
" Mnaweza kuwa zaid ya kumi na bado mkawa mabwana wadogo tu kwangu,endapo utathubutu kushut na mimi naondoka na huyu mwenzenu kwa sababu sishindwi kumshut kabla yenu hamjanishut. Alisema.
Songa nayo.....
Askari waliendelea kumsogelea, Mwalifu bado hakuonekana kutetemeka japo tayari alikuwa amezungukwa, aliombwa ateremshe silaha yake chini lakini aligoma na kusema
"kabla ya kunimaliza mimi sishindwi kummaliza kinyago mwenzenu huyu..
Kiongozi wa mapolice waliokuwa eneo hilo, alijiuliza wafanyeje na anatakiwa akiwa mzima ili aweze kumtaja aliemtuma. Alimuangalia vizuri namna alivyosimama, kwa kuwa yeye na mhalifu walikuwa wamekaliana kipembe pembe aliibinya bastola yake taratibu bila woga wowote, moyoni akisema endapo akimripua huyo askari mmoja aliemuweka chini ya ulinzi sawa tu lakini lengo lao litakuwa limekamilika, na huyo atae uawa atakuwa amekufa kishujaa vitani.
Risasi iliitika kwenye mkono wa mhalifu, hakuwa na balansi tena ya kushika silaha akaiangusha chini, maaskari wengine hapo hapo wakapata nafasi ya kusogea zaidi na kumzingira ili asije kupata nafasi yoyote ya kutoa silaha nyengine mwilini mwake kama anayo.
" Pumbavu wewe ndo umesababisha tutoke jasho sisi namna hii si ndio!?. Aliuliza mmoja.
Askari mwingine alichukua kitambaa cheupe na kuiweka silaha kisha kuitumbukiza ndani ya gari. Hazikupita dakika tano baada ya kufanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mtuhumiwa waandishi wa habari kutoka kituo cha tv Z.B.C walifika pamoja na watangazi watatu waliokuwa wanaongoza kituo kimoja cha Radio.
Police walijiuliza waandishi wametoka wapi kwa muda ule mfupi. Muhalifu bado hakutolewa kitambaa chake cha usoni mpaka pale atapofikishwa kituo cha police mjini znz.
Akiwa anaugulia maumivu yake ya kupigwa Risasi karibu na kiganja chake, askari hawakujali hilo, walimpiga pingu na kumuingiza ndani ya gari, waandishi wa habari waliitaji kupata mawili matatu kutoka kwa maaskari ili wayarushe kwenye vipindi vyao vya breaking newz za jioni hiyo.
Baada ya kuwahoji baadhi ya maaskari, walichukua picha na kushuti video fupi fupi za mazingira, wakaingia kwenye magari yao na kuanza kurudi mjini huku maaskari wote na wao wakifanya utaratibu wa kuelekea mjini kumpeleka mtu aliesumbua ndani ya muda mfupi.
Kipindi wanaanza kutoka eneo la tukio waliwasiliana na vijana ambao wako na hamad, wakawaomba ikiwa hawajafika mjini waende haraka mtuhumiwa ashapatikana na usalama upo sawa.
Ticha alifikishwa hospitalini na matibabu kuanza mara moja ili kuangalia kama uwezekano wa kupona upo, madaktari walimfanyia huduma ya kwanza kumzuia eneo la risasi lisivuje damu ili asije kupoteza damu nyingi zaid, kisha kuanza mpango wa kuitoa risasi.
" Mh huyu aliempiga risasi inaonekana anajua vizuri kutumia silaha na alikuwa amelenga kwenye mshipa maalum lakini haijafanikiwa, mpigeni sindano ya fahamu kisha tuendelee na matibabu. Aliongea mganga mkuu ambaye aliingia kwenye wodi akiwa na nesi wake wawili kwa ajili ya kumwangalia Ticha, aliwaambia Nesi wake wampige sindano ya masaa huku akitoka kwenda ofisini kwake kuchukua baadhi ya vifaa ambavyo aliviacha.
Kipindi anatoka kwenye chumba hicho alichowekwa Ticha alisikia msafara wa magari yanaingizana kwenye geti la hospital m/mmoja, alisogea dirishani na kuchungulia akafanikiwa kumuona Mzee shaibu anashuka moja ya magari matano yaliyoingia kwenye hospital hiyo.
Alitoka kwenye dirisha na kwenda moja kwa moja ofisini kwake, akijua mzee shaibu atapanda juu hospitalini.
Aliingia ofisini kwake akachukua vifaa alivyokuwa anaviitaji kisha kugeuza kuanza kurudi kwenye wodi aliyolazwa ticha, akiwa anafunga mlango alitabasam baada ya kumuona mzee shaibu akipanda ngazi kuja alipo yeye, alisimama mpaka alipofika karibu nae.
"Karibu sana mzee shaibu. Alimkaribisha.
" Asante Dokta. Vipi hali. walishikana mikono.
" Hali yangu ni njema, sijui wewe?
" Mimi namshukuru Mungu mpaka sasa salama. Walianza kutembea taratibu wakifatisha njia iliyokuwa imenyooka.
" Nimepata habari zinazoendelea kwa sasa huko shamba shamba. Kuna salama?
" Salama ipo mzee wangu, si kuhusu habari zaa mwalimu na kijana wako.
" Ndio, ndio, ndio.
" Salama ipo kabisa, Ticha tu kapigwa risasi bahati nzuri haijalenga eneo la hatari, ndio nafanya haraka kwenda kumtibia. Alisema dokta, ghafla nesi alitoka kwenye chumba alichowekwa ticha mbio.
"Dokta mgonjwa mapigo ya moyo yamekata. Aliongea kumwambia dokta wake huku akiwa anahema.
Ilibidi Docta amuache mzee shaibu na kumuomba akae sehemu, alitembea haraka haraka mpaka chumbani, alipofika alianza kumfanyia vipimo Ticha ili kuangalia tatizo gani limepelekea mapigo ya moyo kukata ghafla..
*****
Seid na mama yake bado walikuwa hawajapata taarifa yoyote kuhusu Ticha na Hamad. Walipokuwa tayari wamemaliza kula, Seid alimuita mama yake aliekuwa anakusanya vyombo huku seid akiokota mifupa ya chini.
" Mama!
" Ee! ,,
" Kipindi naenda kununua vitu sokoni, nimeziona difenda mbili zikitimua mbio sijui wahalifu wametokea wapi tena!.
" Heee Zina mapolice au ziko tupu nyuma?
" Tupu!?, wapo wazee wa kazi pamoja na FFU, bora wangekuwa tupu sasa, bunduki nje nje.
" Ee! kiukweli sasa hivi Znz tumeingiliwa sana mwanangu, juzi tu hapo karibia yule mama makame agongwe na gari la majambazi waliovamia mjini kule benk!.
" Na hali hii yote inasababishwa na watu kutoka bara. Alidakia seid.
" Usiseme hivyo, ni sisi sisi hakuna cha bara wala wapi.
" Um mama yangu ngoja ninyamaze tu ila zile sura! za wabara kabisaa.
" Tuyaache hayo, muda uliokuwa unaenda kununua vitu ilipita dakika 20 tu tokea Hamad na mwenzake waondoke, Ebu mpigie cm uulize usalama kwanza isije ikawa wamekumbana na hiyo gharika. Alisema bi najma, akili za kiutu uzima za kuangalia mbali alizokuwa nazo, zilimpelekea kuhisi kitu tofauti ndani ya moyo wake.
"Uenda ni kweli mama ee!. Alisema seid kwa mshangao huku akitoa cm mfukoni.
Aliangalia kwenye call log na kuipiga namba ya Hamad.
Cm ilifanikiwa kuita.
" Rafiki yangu!, alisema hamad baada ya kuona cm ya rafiki yake inaingia na yeye kupokea.
" Vipi hali!
" Hali sio nzuri sana ndugu yangu.
"Sio nzuri sana!?. Umefanikiwa kufika mjini au bado na kwa nini hali haiko vizuri kwa upande wako?. Aliuliza seid.
Kabla ya kujibiwa swali lake Cm nyingine iliingia katika cm ya hamad, alitoa cm sikioni kuangalia anaepiga nani akakuta my fatha, ikabidi amuweke seid hold ampokee baba yake.
Seid baada ya kuwekwa hold alikata cm uso wake ukibadilika kidogo, akiyakumbuka maneno aliyoambiwa alipouliza hali, bi najma akauliza.
"Vipi!.
"Ngoja nimpigie Tena ebu. Alisema seid. Aliipiga tena akakuta inatumika.
"vipi amefika? ,, Bi Najma aliuliza tena.
"Hajanjibu zaid ya kuniweka hold. kibaya naona anaongea kama mtu mwenye wasi wasi.
" ukijaribu kumpigia sasa hivi?
" inatumika!!.
" Eh.
" Baba. Hamad alimuita baba yake baada ya kupokea.
" Uko wapi kijana wangu!!?, aliuliza kwa kuamasika mzee shaibu.
" Niko salama mzee wangu usiwe na wasi wasi wowote.
" Sasa hivi uko wapi!? mama yako yuko katika hali mbaya huko kwa ajili yako!. Anakuulizia sana.
" Ngoja nimpigie nimtulize usijali baba niko salama. Alikata cm haraka akampigia mama yake, alimpata na kumwambia asijali yeye yuko vizuri, wawaze na kuomba juu ya Ticha na sii yeye.
Alipoelewana na wazee wake wote wawili Cm ya rafiki yake seid aliiona inaingia akamuomba mama yake akate kuna mtu anampigia.
" Naona cm imakatika swahiba, niliitaji kujua kama umefika mjini tayari au laa kwa sababu kuna difenda nliziona zinapita huku kwetu, nikadhani kuna uhalifu tayari ushafanyika na uenda umekukumba. Alisema seid.
" Yeah mawazo yako si mabaya na hizo difenda zilikuwa zinatuhusu sisi nadhani. Alisema hamad. Seid akashtuka.
" Kivipi?. Aliuliza kwa mshangao.
" Ticha kapigwa risasi bhana, Kipindi tunatoka huko tulikutana na gari kati kati ya bara bara, tukiwa tunashangaa akatokea mtu akampiga Risasi.
" Mungu wangu!. na wewe uko wapi sasa?.
" Mimi niko kwenye gari nakaribia mfenensini sasa kuelekea mjini.
" Sasa hivi nakuja!. Alisema Seid na kukata cm, tayari alishachanganyikiwa alipoambiwa ticha kapigwa risasi, alivaa nguo zake haraka haraka na kumwambia mama yake wataongea badae.
Bi najma alijaribu kuuliza kimetokea nini seid hakujibu, akatoka na kuanza kutembea mbio mbio kutafuta dala dala kwa ajili ya kwenda mjini kumuona Ticha....
Difenda zilizokuwa zimeuongoza msafara wa mhalifu kumpeleka katika kituo cha malindi mjini zilizidi kukanyaga mafuta ili waweze kumfikisha mapema akiwa chini ya ulinzi mkali mno, pamoja na zile zilizokuwa zinamsindikiza hamad, huku seid nae akiwa tayari amepata gari kutoka shamba kwa ajili ya kufatilia kuhusu Ticha.
Dokta aliekabidhiwa kazi ya kumtibia ticha alihakikisha anatumia uganga wake wote na utaalam wa hali ya juu kumkarabati, alipomaliza alienda kuzungumza na mzee shaibu ambae badae waliagana baada ya kupigiwa cm na kuambiwa mwalifu analetwa katika kituo cha police malindi.
Robo saa magari yote ya police yalikuwa katika kituo hicho kikubwa mjini zanzibar, huku wana usalama na baadhi ya mapolice waliokuwa wanalitumikia jeshi kupitia hicho kituo wakiwa nje kusubiria kumuona mualifu kwa hamu.
Msafara wa magari matano likiwemo gari lililombeba Mzee shaibu nao uliingia katika kituo hicho, Huku gari la hamad pamoja na la vijana watatu waliokuwa nyuma yake nayo yakiingia.
Mzee shaibu alipoona gari la kijana wake kwa mbali alianza kulifata taratibu, baada ya kushuka alimkumbatia huku hamad akisema "I'm the geniass father siwezi kufa kirahisi namna hiyo.
Waliachia tabasam wote wawili mtu na mtoto wake, Wakaongozana mpaka ndani ya kituo ili kumuona mtu aliejitahidi kulitoa jasho jeshi la police na kufanya wananchi wakae roho juu juu kwa risasi zilizokuwa zikimiminwa.
Mhalifu alikalichwa kwenye kiti ndani ya kituo cha police mara tu aliposhushwa kwenye gari, alitolewa kitambaa usoni. Kila mmoja alitoa macho na kukaa katika hali ya siamini kuwa sura anayoiyona mbele yake ndiyo sura iliyofanya unyama wa kumpiga ticha risasi, na kuwaangaisha watu kiasi chote hicho cha kuwaangaisha.