Riwaya: MSAMAHA WA MAMA Mwandishi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA 12 Mzunguko wa kutangazwa habari za kurudiwa kwa matokeo ya kidato cha sita ndani ya muda mfupi ziliwashtua wengi, maradio mengi yalitangaza habari hiyo, huku Tv ya Z B C nayo ikitangaza habari za matokeo hayo na kupata fununu za chini kwa chini za waziri wa elimu kupiga cm kwa kijakazi wake na kuitaji ajiuzulu kazi ndani ya masaa 24 bila kujulikana chanzo chake nini. Nini kiliendelea?. SONGA NAYO... Seid bado alikuwa njiani kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi na mama yake, Cm yake ya simen ilianza kuita, akazima mziki akaitoa mfukoni na kupokea haraka baada ya kuangalia kwenye screen na kukuta jina ni Hamad. " Nambie rafiki yangu. " Vipi ushafika? " Bado ndio kwanza naiacha bububu. " Ok!, habari zishaenea za kurudiwa matokeo. " Usinambie! " tayari vyombo vya habari vishatangaza kila kitu. " Furaha kwangu hiyo rafiki yangu. Alisema kwa tabasam zito lililosheheni vizuri mdomoni mwake. Waliongea zaid na zaid kisha hamad alikata cm, Seid alipiga mayoe ya furaha akaachia ngoma na kwendelea kudundika ndani ya gari, aliona dunia yote ameitawala yeye ndani ya muda mfupi, baada ya kupita sehemu iliyokuwa na msongamano kidogo wa magari alikanya mafuta speed ikasomeka 100 kamili, aliviangalia vitu vinavyowaka kwenye gari akasema akitabasam peke yake " Haya ndio maisha sasa, yani mtu upo kwenye chombo raha yake utafikiri tayari uko peponi manina, hadi moyo unacheka ndani kwa ndani, ukonde kwa lipi sasa!? na nikizipata mie, Eheeeeee! mbona wajiandae!, haiwezekani nilie shida miaka yote kisha nije kuzipata nishindwe kula bata kwanza, Lazima niwapige shenzi time alaaa!. Ni taa tu zilikuwa zinaonekana kutokana na mwendo kasi wa gari, ndani ya nusu saa alifanikiwa kufika nyumbani kwao, alipaki gari nje akigonga honi za mfurulizo, Bi Najma alikuwa amekaa ndani ikabidi atoke nje kuangalia honi za nini usiku huo. Alishangaa alipokuwa tayari ametoka nje kuona gari zuri limepaki, Seid alishuka kwa mbwembwe zote akamkimbilia mama yake aliekuwa amesimama mlangoni. " Shikamoo mama. " Maraaba. "Mama haya ndio maisha yangu ya badae. Alimsogelea mama yake na kumwambia hivyo mara alipomaliza kumsalimia. " Wewe mtoto, hili gari umelitoa wapi?. " Rafiki yangu kanipatia nirudi nyumbani bila kutumia usafiri wa dala dala akijua utanisumbua, Ila Haya ndo yatakuwa maisha yangu ya mbele mama yani ni gud time tu hadi raha. " Na vipi kuhusu matokeo yako, mmefanikiwa? " Tuingie ndani kwanza mama yangu mengine yatafata. Waliingia ndani wakafunga mlango, Waliongea mengi seid akimueleza kila kitu mama yake, walipomaliza kuongea kama kawaida ilishushwa pazia kisha kila mmoja akalala. Asubuhi na mapema bi najma aliamka akaingia shambani, Seid nae alipoamka alifata nyayo za mama yake, walipariria baadhi ya viazi na mazao mengine yaliyokuwemo shambani, saa nne walitoka wakaandaa chai ya kunywa wakiwa na uhakika wa vitafunio hata chakula cha mchana kutokana na pesa waliopatiwa na hamad kuwa bado ipo. Seid alipotoka shambani ilibidi aende sokoni kununua mandazi au chapati pamoja na vitu vingine, aliporudi tayari alikuta chai nzuri ya asilia imeandaliwa na mama yake, walianza kunywa wakiongea maneno ya kutaniana yaliyowafanya wacheke na kufurahi. Walimaliza Seid akachukua maji akaenda bafuni kuoga, Baada ya kumaliza alikuta cm yake inaita, akapangusa maji maji yaliyokuwa katika kiganja akapokea haraka. Alikuwa ni rafiki yake ambaye alimpigia kwa ajili ya kumwambia awahi mjini aone mambo mazuri kuhusu matokeo na ticha kiujumla. Seid alijiandaa chap chap akamuaga mama yake kwa ajili ya kuondoka. " Hivi mama, ungesikia raha gani kama ningekuwa nimepaki gari kama hili alafu la kwangu. Alimuuliza mama yake akiwa mbele ya gari. " Ningejisikia furaha sana, ila usijali mwanangu yote ni majaliwa utapata tu lako babaangu mi nakuombea dua, nina hakika Mungu atasikia kilio changu siku moja. Seid hakuongea chochote kuongezea kile alichokiongea bi najma, alitembea hadi kwenye mlango wa gari akiwa anatikisa kichwa chake, alibinya funguo, gari ikawaka, alifungua mlango akaingia ndani. " Na nikiingia chuo watanikoma mimi Akyamungu, kwa sababu mambo kama haya ndio yananipa hasira za kusoma, naishi kwa tabu, shida, njaa wenzangu wanamiliki vitu vikubwa kama hivi, malaptop, ma ipad ma nini sijui dah yote maisha tu poa. Aliongea peke yake ndani ya gari, aliwasha taratibu akaanza kurudi nyuma kutafuta upenyo wa kugeuzia, Bi najma muda wote alimuangalia mwanae anavyoendesha, japo alikuwa hamuoni kutokana na vioo kuwa vyeusi. Aliachia tabasam akanyoosha mikono juu na kumuomba Mungu amuongoze mwanae ili nae siku moja afanikiwe apate vya kwakwe. Baada ya kugeuza gari alikanyaga mafuta mpaka mjini, alifika eneo la chuo kila mmoja akishangaa kuona Seid anaendesha gari wakati haijawai kutokea, alimkumbatia rafiki yake hamad aliekuwa tayari yuko eneo hilo, alisogea ubaoni kuangalia matokeo ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa wanafunzi wengi, Alipoyaona alijikuta akiachia meno yote mdomoni nje kwa furaha, Machozi yalianza kumlenga lenga akainua mikono juu na kumshukuru Mungu. Hamad alimuomba waende pembeni kwa ajili ya kuzungumza, kabla ya yote seid alimpigia mama yake cm akamwambia amepata matokeo mazuri ya kuingia moja kwa moja chuo. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa bi najma. Hamad na seid walisogea pembeni kuongea huku wote wakionekana kufurahi sana kwa kuwa bado wataendelea kuwa darasa moja hata watakapokuwa chuoni. " Rafiki yangu Niliwahi kukuambia siku moja haki ya mtu Haipotei, na bora aibu kuliko fedheha waswahili wanasema, ila hawa watu wamekubali fedheha wakaogopa aibu niulize kwa nini. Hamad aliongea kwa kutumia mdomo na vitendo vya mkono. "Kwa nini ,, Seid alisema kama alivyoambiwa aseme. "Vizuri, Michael Jamseh anasema katika kitabu chake kizuri cha kifaransa ambacho mpaka kesho hakupatikana mwingereza wa kutia neno lake hata moja. " Mtu anathamini chake kuliko cha mwenzake, waliowengi wanafurahi kuona vya kwao vinafanikiwa ila vya wengine vinafeli, mtu wa aina hii yuko tayari akuone unachomwa mshale yeye akacheka akijua hupati uchungu, ila endapo ule mshale utamgeukia uso wake hubadilika na kuwa kama uso wa chatu mwenye njaa kali, ambae hana huruma na mwanadam pindi anapotaka kummeza. Huyu jamaa rafiki yangu alikuwa na akili sana kuyaongea haya maneno, Mr Zubeir aliitaji kutumia pesa ili mwanae apite, akasahau msemo wa wahindi usemao my Opena, Mungu alivyo mkubwa, akamuonesha kuwa haki ya mnyonge miaka yote hailiki hivi hivi, aibu aliyoipata sasa hivi katimkia marekani, kijana wake kampeleka wapi sijui huko ndio maana humuoni hapa, Watu baada ya kutumia akili zao za kuzaliwa kupata matokeo mazuri anategemea kuhonga, si upuuzi uliopindukia huo?, Kizuri zaid soma hili gazeti ukurasa wa nne uone mambo. Alisema hamad. Seid alipatiwa gazeti la Zanzibar Leo, lililokuwa lina habari za kijakazi wa Waziri wa Elimu profesa Sharif kujiuzulu kazi asubuhi ya saa mbili, pamoja na ukweli wote kubainika kuhusu kupigwa risasi kwa ticha, Pia kutangazwa kiongozi huyo kuwa miongoni mwa watu wajuu walioshiriki kuuza matokeo ambao wengine hawakujulikana. Seid alishangaa zaid baada ya kuiona picha yake kwenye gazeti na maelezo yasemayo. "Huyu ndio kijana aliewaburuza watoto wa vigogo katika matokeo, matokeo yake ndio yaliyokuwa yameuzwa. Alifunika gazeti akamuangalia Hamad. " Hiyo ndio habari nzima iliyopo. Furaha aliyokuwa nayo Seid hakuweza kuijua mtu yoyote zaid yake na Mungu wake, alimshukuru sana Hamad aliefanya juu chini mpaka kueneza habari za kuuzwa matokeo ya mitihani yake, walitoka eneo walilokuwa wamesimama, wakaenda kwenye ofisi ya waziri baada ya hamad kupigiwa cm na waziri wa Elimu akiwaitaji waende. Walipofika kwa waziri, waziri alimpongeza seid na kumpa pole pia juu ya usumbufu uliojitokeza, waliongea mambo kadhaa yaliyohusu matokeo na mipangilio mipya ya chuo. Waziri alimuahidi seid kumpatia Laptop na vitabu vyote vitavyoitajika akiwa chuo ili asije kusumbuka tena, Alishukuru sana Seid juu ya msaada huo wa Waziri, japo matokeo yake ya kuingia chuo yalipatikana lakini bado hakujua vifaa vyote vya kusomea atavipata wapi. Cm yake ilianza kuita, Baada ya kuiangalia jina lilikuwa Ticha, Alipokea na kuanza kuongea nae, alifurahi sana baada ya kusikia sauti ya Ticha wake ikiwa katika hali ya furaha, mwisho Seid aliomba wakutane kwa ajili ya maongezi kabla hajarudi shamba. Hawakuwa na cha zaid cha kuongea na waziri kwa muda huo, Waliitaji kumuaga wamuache aendelee na kazi za kiofisi zilizoko mbele yake, na wao warudi makwao kupumzisha akili kwani hakukuwa na chengine cha kuwafanya wazunguke mjini. " Kijana kabla hamjaondoka, Naomba siku moja kabla ya kuingia chuo, uje ofisini kwangu, tutaongozana hadi wizarani nikakupatie vitabu, na kuhusu Laptop tufanye hivi. Alisema waziri. Alifungua droo akatoa kiasi cha pesa laki tano na nusu Akampatia Seid, Seid alipokea kwa mikono miwili " Asante sana Waziri wangu asante sana kiukweli sina la kukulipa zaid ya kukuombea dua Ili mungu akuzidishie. " Usijali kijana, Hiyo ni kazi yangu kiongozi wa vijana kama nyie wenye hali za chini na kuonesha nia ya kufika mbali, maana najua miaka mitatu au minne mbele utakuja kuwa mtu mkubwa serikalini au Tanzania, pita mjini ununue laptop ikusaidie katika masomo yako. " Mimi ndio maana huwa nasema, kama wakipatikana viongozi kumi tu wakawa kama wewe, hii Tanzania yetu inanyooka. Hamad aliongea akimuangalia waziri, Waziri hakuwa na la kuongea zaid ya kucheka, walimuaga wakatoka nje, waliingia kwenye gari na kuanza safari ya kwenda mjini wakipiga stori za hapa na pale kuondoa hali ya kusababisha ukimya. " Seid hiyo pesa usinunulie laptop, iweke itakusaidia kwenye mambo mengine, kwa sababu nadhani tukishaingia chuo kuna vitu vingi sana itabidi ukabiliane navyo na vinaitaji pesa. Mimi nina laptop mbili, nitakupatia moja utumie mpaka pale utapo maliza. Wakiwa kati kati ya maongezi Hamad aliongea maneno hayo yaliyokuwa kama lulu kwa seid.. " Dah, kiukweli wewe ni zaid ya rafiki kwangu, huwa unapenda kumwambia waziri kuwa kama wangepatikana kumi kama yeye, lakini hata kwako kaka, wakipatikana marafiki kumi kama wewe lazima mtu uendelee. Walipofika mjini waliongea kidogo, Wakafanikiwa kukutana na Ticha wakaongea nae ndani ya muda mfupi, kisha Seid akapata dala dala na kurudi shamba. Hamad alienda moja kwa moja hadi nyumbani anakoishi, akamkuta baba yake na mama yake bi Suria wakiwa wamekaa sebleni wanapata Tangawizi. " Assalam alaykum. Alisalimia alipoingia ndani na kukaa kwenye sofa, Wazee wake walimuitikia kwa furaha, kisha kumuuliza kuhusu matokeo mapya na hali ya hewa ilivyo huko mjini mjini. " Kiukweli namshukuru Mungu, hali ya hewa imetulia inaridhisha. " Na vipi kuhusu Ticha? ,,Mzee shaibu aliuliza. " Ticha ashapona, tumetoka kuonana nae muda si mrefu bado amelazwa lakini, hakuumia mno ilikuwa ni mshtuko tu. " Mpigie cm niweze kuongea naye kama tayari anaweza kuongea, Na vipi kuhusu yule mwenzako?. " Seid?. " Ndio. " Karudi kwao sasa hivi. " Na matokeo alikuwa amepata vipi. " Aaaah baba yule mtu si mtu mzuri, katuburuza wote kidato cha sits achana nae kabisa. "Aisseeee. Hamad alimpigia cm ticha na kumuambia mzee wake anamsalimia anataka kuongea na yeye, kwa bahati mbaya salio halikuwepo la kutosha, kabla ya kumpatia mzee shaibu cm ilikatika.. Baada ya kukata ukimya kidogo ulipita, Mzee shaibu ndo alianzisha mazungumzo upya alipouliza tarehe ya kuingilia chuo, Alijibu hamad na kuendelea kuongea na wazazi wake, huku akiwaelezea namna ambavyo hatoweza kulisahau tukio hilo lililotokea la Ticha kutandikwa risasi na kamanda wa jeshi la police mr Richad, ambaye kesi yake imeishia juu juu na haikusikika tena mara tu alipofika dar kutokana na mkono wa pesa uliokuwa umemzunguka. Seid alifika nyumbani kwao akakuta mlango umefungwa, Aliushika akautikisa na kushangaa sana baada ya kugundua umefungwa kwa ndani, alimuita mama yake bila kufanikiwa kuitikiwa, aliita tena na tena kwa nguvu bila mtu kuitika, ikabidi azunguke mpaka nyuma kuliko kuwa na dirisha, akaita mama! mama, mama Seid lakini wapi!, alirudi mbele akauangalia vizuri na kuhakikisha haujafungwa kwa nje. " Um mbona mlango haujafungwa kwa nje huu na mama haitiki?, Mama!, Mamaa! Alimuita tena bila kuitikia " jamani ina maana mama hayumo ndani au vipi ? Tukutane Sehemu ya Kumi na Tatu. - RAHA ZA KITANDANI

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA Mwandishi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA 12 Mzunguko wa kutangazwa habari za kurudiwa kwa matokeo ya kidato cha sita ndani ya muda mfupi ziliwashtua wengi, maradio mengi yalitangaza habari hiyo, huku Tv ya Z B C nayo ikitangaza habari za matokeo hayo na kupata fununu za chini kwa chini za waziri wa elimu kupiga cm kwa kijakazi wake na kuitaji ajiuzulu kazi ndani ya masaa 24 bila kujulikana chanzo chake nini. Nini kiliendelea?. SONGA NAYO... Seid bado alikuwa njiani kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi na mama yake, Cm yake ya simen ilianza kuita, akazima mziki akaitoa mfukoni na kupokea haraka baada ya kuangalia kwenye screen na kukuta jina ni Hamad. " Nambie rafiki yangu. " Vipi ushafika? " Bado ndio kwanza naiacha bububu. " Ok!, habari zishaenea za kurudiwa matokeo. " Usinambie! " tayari vyombo vya habari vishatangaza kila kitu. " Furaha kwangu hiyo rafiki yangu. Alisema kwa tabasam zito lililosheheni vizuri mdomoni mwake. Waliongea zaid na zaid kisha hamad alikata cm, Seid alipiga mayoe ya furaha akaachia ngoma na kwendelea kudundika ndani ya gari, aliona dunia yote ameitawala yeye ndani ya muda mfupi, baada ya kupita sehemu iliyokuwa na msongamano kidogo wa magari alikanya mafuta speed ikasomeka 100 kamili, aliviangalia vitu vinavyowaka kwenye gari akasema akitabasam peke yake " Haya ndio maisha sasa, yani mtu upo kwenye chombo raha yake utafikiri tayari uko peponi manina, hadi moyo unacheka ndani kwa ndani, ukonde kwa lipi sasa!? na nikizipata mie, Eheeeeee! mbona wajiandae!, haiwezekani nilie shida miaka yote kisha nije kuzipata nishindwe kula bata kwanza, Lazima niwapige shenzi time alaaa!. Ni taa tu zilikuwa zinaonekana kutokana na mwendo kasi wa gari, ndani ya nusu saa alifanikiwa kufika nyumbani kwao, alipaki gari nje akigonga honi za mfurulizo, Bi Najma alikuwa amekaa ndani ikabidi atoke nje kuangalia honi za nini usiku huo. Alishangaa alipokuwa tayari ametoka nje kuona gari zuri limepaki, Seid alishuka kwa mbwembwe zote akamkimbilia mama yake aliekuwa amesimama mlangoni. " Shikamoo mama. " Maraaba. "Mama haya ndio maisha yangu ya badae. Alimsogelea mama yake na kumwambia hivyo mara alipomaliza kumsalimia. " Wewe mtoto, hili gari umelitoa wapi?. " Rafiki yangu kanipatia nirudi nyumbani bila kutumia usafiri wa dala dala akijua utanisumbua, Ila Haya ndo yatakuwa maisha yangu ya mbele mama yani ni gud time tu hadi raha. " Na vipi kuhusu matokeo yako, mmefanikiwa? " Tuingie ndani kwanza mama yangu mengine yatafata. Waliingia ndani wakafunga mlango, Waliongea mengi seid akimueleza kila kitu mama yake, walipomaliza kuongea kama kawaida ilishushwa pazia kisha kila mmoja akalala. Asubuhi na mapema bi najma aliamka akaingia shambani, Seid nae alipoamka alifata nyayo za mama yake, walipariria baadhi ya viazi na mazao mengine yaliyokuwemo shambani, saa nne walitoka wakaandaa chai ya kunywa wakiwa na uhakika wa vitafunio hata chakula cha mchana kutokana na pesa waliopatiwa na hamad kuwa bado ipo. Seid alipotoka shambani ilibidi aende sokoni kununua mandazi au chapati pamoja na vitu vingine, aliporudi tayari alikuta chai nzuri ya asilia imeandaliwa na mama yake, walianza kunywa wakiongea maneno ya kutaniana yaliyowafanya wacheke na kufurahi. Walimaliza Seid akachukua maji akaenda bafuni kuoga, Baada ya kumaliza alikuta cm yake inaita, akapangusa maji maji yaliyokuwa katika kiganja akapokea haraka. Alikuwa ni rafiki yake ambaye alimpigia kwa ajili ya kumwambia awahi mjini aone mambo mazuri kuhusu matokeo na ticha kiujumla. Seid alijiandaa chap chap akamuaga mama yake kwa ajili ya kuondoka. " Hivi mama, ungesikia raha gani kama ningekuwa nimepaki gari kama hili alafu la kwangu. Alimuuliza mama yake akiwa mbele ya gari. " Ningejisikia furaha sana, ila usijali mwanangu yote ni majaliwa utapata tu lako babaangu mi nakuombea dua, nina hakika Mungu atasikia kilio changu siku moja. Seid hakuongea chochote kuongezea kile alichokiongea bi najma, alitembea hadi kwenye mlango wa gari akiwa anatikisa kichwa chake, alibinya funguo, gari ikawaka, alifungua mlango akaingia ndani. " Na nikiingia chuo watanikoma mimi Akyamungu, kwa sababu mambo kama haya ndio yananipa hasira za kusoma, naishi kwa tabu, shida, njaa wenzangu wanamiliki vitu vikubwa kama hivi, malaptop, ma ipad ma nini sijui dah yote maisha tu poa. Aliongea peke yake ndani ya gari, aliwasha taratibu akaanza kurudi nyuma kutafuta upenyo wa kugeuzia, Bi najma muda wote alimuangalia mwanae anavyoendesha, japo alikuwa hamuoni kutokana na vioo kuwa vyeusi. Aliachia tabasam akanyoosha mikono juu na kumuomba Mungu amuongoze mwanae ili nae siku moja afanikiwe apate vya kwakwe. Baada ya kugeuza gari alikanyaga mafuta mpaka mjini, alifika eneo la chuo kila mmoja akishangaa kuona Seid anaendesha gari wakati haijawai kutokea, alimkumbatia rafiki yake hamad aliekuwa tayari yuko eneo hilo, alisogea ubaoni kuangalia matokeo ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa wanafunzi wengi, Alipoyaona alijikuta akiachia meno yote mdomoni nje kwa furaha, Machozi yalianza kumlenga lenga akainua mikono juu na kumshukuru Mungu. Hamad alimuomba waende pembeni kwa ajili ya kuzungumza, kabla ya yote seid alimpigia mama yake cm akamwambia amepata matokeo mazuri ya kuingia moja kwa moja chuo. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa bi najma. Hamad na seid walisogea pembeni kuongea huku wote wakionekana kufurahi sana kwa kuwa bado wataendelea kuwa darasa moja hata watakapokuwa chuoni. " Rafiki yangu Niliwahi kukuambia siku moja haki ya mtu Haipotei, na bora aibu kuliko fedheha waswahili wanasema, ila hawa watu wamekubali fedheha wakaogopa aibu niulize kwa nini. Hamad aliongea kwa kutumia mdomo na vitendo vya mkono. "Kwa nini ,, Seid alisema kama alivyoambiwa aseme. "Vizuri, Michael Jamseh anasema katika kitabu chake kizuri cha kifaransa ambacho mpaka kesho hakupatikana mwingereza wa kutia neno lake hata moja. " Mtu anathamini chake kuliko cha mwenzake, waliowengi wanafurahi kuona vya kwao vinafanikiwa ila vya wengine vinafeli, mtu wa aina hii yuko tayari akuone unachomwa mshale yeye akacheka akijua hupati uchungu, ila endapo ule mshale utamgeukia uso wake hubadilika na kuwa kama uso wa chatu mwenye njaa kali, ambae hana huruma na mwanadam pindi anapotaka kummeza. Huyu jamaa rafiki yangu alikuwa na akili sana kuyaongea haya maneno, Mr Zubeir aliitaji kutumia pesa ili mwanae apite, akasahau msemo wa wahindi usemao my Opena, Mungu alivyo mkubwa, akamuonesha kuwa haki ya mnyonge miaka yote hailiki hivi hivi, aibu aliyoipata sasa hivi katimkia marekani, kijana wake kampeleka wapi sijui huko ndio maana humuoni hapa, Watu baada ya kutumia akili zao za kuzaliwa kupata matokeo mazuri anategemea kuhonga, si upuuzi uliopindukia huo?, Kizuri zaid soma hili gazeti ukurasa wa nne uone mambo. Alisema hamad. Seid alipatiwa gazeti la Zanzibar Leo, lililokuwa lina habari za kijakazi wa Waziri wa Elimu profesa Sharif kujiuzulu kazi asubuhi ya saa mbili, pamoja na ukweli wote kubainika kuhusu kupigwa risasi kwa ticha, Pia kutangazwa kiongozi huyo kuwa miongoni mwa watu wajuu walioshiriki kuuza matokeo ambao wengine hawakujulikana. Seid alishangaa zaid baada ya kuiona picha yake kwenye gazeti na maelezo yasemayo. "Huyu ndio kijana aliewaburuza watoto wa vigogo katika matokeo, matokeo yake ndio yaliyokuwa yameuzwa. Alifunika gazeti akamuangalia Hamad. " Hiyo ndio habari nzima iliyopo. Furaha aliyokuwa nayo Seid hakuweza kuijua mtu yoyote zaid yake na Mungu wake, alimshukuru sana Hamad aliefanya juu chini mpaka kueneza habari za kuuzwa matokeo ya mitihani yake, walitoka eneo walilokuwa wamesimama, wakaenda kwenye ofisi ya waziri baada ya hamad kupigiwa cm na waziri wa Elimu akiwaitaji waende. Walipofika kwa waziri, waziri alimpongeza seid na kumpa pole pia juu ya usumbufu uliojitokeza, waliongea mambo kadhaa yaliyohusu matokeo na mipangilio mipya ya chuo. Waziri alimuahidi seid kumpatia Laptop na vitabu vyote vitavyoitajika akiwa chuo ili asije kusumbuka tena, Alishukuru sana Seid juu ya msaada huo wa Waziri, japo matokeo yake ya kuingia chuo yalipatikana lakini bado hakujua vifaa vyote vya kusomea atavipata wapi. Cm yake ilianza kuita, Baada ya kuiangalia jina lilikuwa Ticha, Alipokea na kuanza kuongea nae, alifurahi sana baada ya kusikia sauti ya Ticha wake ikiwa katika hali ya furaha, mwisho Seid aliomba wakutane kwa ajili ya maongezi kabla hajarudi shamba. Hawakuwa na cha zaid cha kuongea na waziri kwa muda huo, Waliitaji kumuaga wamuache aendelee na kazi za kiofisi zilizoko mbele yake, na wao warudi makwao kupumzisha akili kwani hakukuwa na chengine cha kuwafanya wazunguke mjini. " Kijana kabla hamjaondoka, Naomba siku moja kabla ya kuingia chuo, uje ofisini kwangu, tutaongozana hadi wizarani nikakupatie vitabu, na kuhusu Laptop tufanye hivi. Alisema waziri. Alifungua droo akatoa kiasi cha pesa laki tano na nusu Akampatia Seid, Seid alipokea kwa mikono miwili " Asante sana Waziri wangu asante sana kiukweli sina la kukulipa zaid ya kukuombea dua Ili mungu akuzidishie. " Usijali kijana, Hiyo ni kazi yangu kiongozi wa vijana kama nyie wenye hali za chini na kuonesha nia ya kufika mbali, maana najua miaka mitatu au minne mbele utakuja kuwa mtu mkubwa serikalini au Tanzania, pita mjini ununue laptop ikusaidie katika masomo yako. " Mimi ndio maana huwa nasema, kama wakipatikana viongozi kumi tu wakawa kama wewe, hii Tanzania yetu inanyooka. Hamad aliongea akimuangalia waziri, Waziri hakuwa na la kuongea zaid ya kucheka, walimuaga wakatoka nje, waliingia kwenye gari na kuanza safari ya kwenda mjini wakipiga stori za hapa na pale kuondoa hali ya kusababisha ukimya. " Seid hiyo pesa usinunulie laptop, iweke itakusaidia kwenye mambo mengine, kwa sababu nadhani tukishaingia chuo kuna vitu vingi sana itabidi ukabiliane navyo na vinaitaji pesa. Mimi nina laptop mbili, nitakupatia moja utumie mpaka pale utapo maliza. Wakiwa kati kati ya maongezi Hamad aliongea maneno hayo yaliyokuwa kama lulu kwa seid.. " Dah, kiukweli wewe ni zaid ya rafiki kwangu, huwa unapenda kumwambia waziri kuwa kama wangepatikana kumi kama yeye, lakini hata kwako kaka, wakipatikana marafiki kumi kama wewe lazima mtu uendelee. Walipofika mjini waliongea kidogo, Wakafanikiwa kukutana na Ticha wakaongea nae ndani ya muda mfupi, kisha Seid akapata dala dala na kurudi shamba. Hamad alienda moja kwa moja hadi nyumbani anakoishi, akamkuta baba yake na mama yake bi Suria wakiwa wamekaa sebleni wanapata Tangawizi. " Assalam alaykum. Alisalimia alipoingia ndani na kukaa kwenye sofa, Wazee wake walimuitikia kwa furaha, kisha kumuuliza kuhusu matokeo mapya na hali ya hewa ilivyo huko mjini mjini. " Kiukweli namshukuru Mungu, hali ya hewa imetulia inaridhisha. " Na vipi kuhusu Ticha? ,,Mzee shaibu aliuliza. " Ticha ashapona, tumetoka kuonana nae muda si mrefu bado amelazwa lakini, hakuumia mno ilikuwa ni mshtuko tu. " Mpigie cm niweze kuongea naye kama tayari anaweza kuongea, Na vipi kuhusu yule mwenzako?. " Seid?. " Ndio. " Karudi kwao sasa hivi. " Na matokeo alikuwa amepata vipi. " Aaaah baba yule mtu si mtu mzuri, katuburuza wote kidato cha sits achana nae kabisa. "Aisseeee. Hamad alimpigia cm ticha na kumuambia mzee wake anamsalimia anataka kuongea na yeye, kwa bahati mbaya salio halikuwepo la kutosha, kabla ya kumpatia mzee shaibu cm ilikatika.. Baada ya kukata ukimya kidogo ulipita, Mzee shaibu ndo alianzisha mazungumzo upya alipouliza tarehe ya kuingilia chuo, Alijibu hamad na kuendelea kuongea na wazazi wake, huku akiwaelezea namna ambavyo hatoweza kulisahau tukio hilo lililotokea la Ticha kutandikwa risasi na kamanda wa jeshi la police mr Richad, ambaye kesi yake imeishia juu juu na haikusikika tena mara tu alipofika dar kutokana na mkono wa pesa uliokuwa umemzunguka. Seid alifika nyumbani kwao akakuta mlango umefungwa, Aliushika akautikisa na kushangaa sana baada ya kugundua umefungwa kwa ndani, alimuita mama yake bila kufanikiwa kuitikiwa, aliita tena na tena kwa nguvu bila mtu kuitika, ikabidi azunguke mpaka nyuma kuliko kuwa na dirisha, akaita mama! mama, mama Seid lakini wapi!, alirudi mbele akauangalia vizuri na kuhakikisha haujafungwa kwa nje. " Um mbona mlango haujafungwa kwa nje huu na mama haitiki?, Mama!, Mamaa! Alimuita tena bila kuitikia " jamani ina maana mama hayumo ndani au vipi ? Tukutane Sehemu ya Kumi na Tatu.


Ilipoishia……
“Um mbona mlango haujafungwa kwa nje huu na mama haitiki?, Mama!, Mamaa!
Alimuita tena bila kuitikia.
” jamani ina maana mama hayumo ndani au vipi?
Songa nayo:
Baada ya kuona kimya alitoka eneo la mlangoni akaingia shambani kumtafuta akidhani uenda umefungwa tofauti na alivyozoea, shambani bado hakumkuta akarudi tena mlangoni na kwendelea kuita upya, Baada ya kuona haitikiwi, maneno yalimtoka akiwa tayari amekunja uso wake.
” Dah, hii ndo shida ya umasikini ninayoisemea mimi kila siku, hapa mama angekuwa na cm si ningempigia tu nikajua yuko wapi!?. Mama! Mama yangu! aliita akigonga mlango kwa nguvu.
” Abee.. ni sauti iliyotokea ndani.
Alishangaa sana kusikia mama yake anaitika baada ya kugonga zaid ya mara tano kwa nguvu, bi najma alifungua mlango akiwa katika hali ya uchovu hali ya usingizi, seid alimuangalia mama yake bila kummaliza mwisho akaachia tabasam na kusema.
” Tatizo nini mama yangu!, nimeita mpaka nimekata tamaa, nikawa na wasi wasi juu yako tatizo nini?
” Ina maana umekuja muda mrefu!?. Aliuliza bi najma.
” hadi nimezunguka nyuma kwenye dirisha nikaenda shambani sikuoni mama yangu!, tatizo nini?. Aliongea kwa sauti ya chini kama mtu anaesikitika.
” Ah! kweli usingizi ni nusu ya kifo, sikusikia kabisaa kiukweli kama umeita, karibu.
Alimpokea mwanae akaingia nae ndani huku akimwambia amsamehe ni uchovu wa usingizi aliokuwa nao siku nyingi, kutokana na kila siku kuamka mapema kufanya kazi nyingi na kukosa muda wa kulala mchana.
” Vipi hali za mjini huko wanasemaje?. Alimuuliza baada ya kuingia ndani, Seid akiwa amekaa kwenye kigoda mama kitandani.
” Namshukuru Mungu salama kabisa.
Walifungua ukurasa wa mazungumzo, alimueleza kila kitu kilichoendelea mjini, pamoja na matokeo kuwa mazuri ya kuingia chuo, Bi Najma alimpa hongera mwanae akionekana kuwa na furaha, alipiga miayo akahisi usingizi bado unamuuma machoni, aliinuka alikokuwa amekaa akachukua maji kidogo kwenye kikombe, akatoka nje kunawa uso ili awe sawa.
Siku zilikatika hatimae wiki ikaondoka,
Maisha ya pande zote tatu yalisonga mbele, Mawasiliano ya karibu sana yakiwepo kati ya Ticha, Hamad na Seid, Huku Seid akitumia muda mwingi kumsaidia mama yake na kufanya mambo yake muhimu kwa kutumia laptop ambayo tayari alipatiwa na Hamad.
Nyumba yao ilikuwa ni ya mawe juu iliezekwa makuti, kama ilivyo kawaida ya nyumba za kizanzibar, ngumu sana kuzikuta hazina umeme, nyumba hii nayo ilikuwa ina umeme japo kulipia ilikuwa ni mara moja moja kutokana na kipato kuwa chini sana, ila msimu huo Seid alitoa elfu 20 katika pesa alizopewa na waziri akalipia umeme wa miezi minne au mitano kutokana na matumizi yao kuwa madogo sana.
Baada ya wiki mbili, mchana mmoja wa jumaa nne seid akiwa yuko anahamisha baadhi ya vitu alivyotumiwa na Hamad kupitia njia ya Email kwenye Laptop akivitoa kwenye Email kuvipeleka kwenye my Memories ( kumbu kumbu zangu), alipigiwa cm ghafla na Ticha wakasalimiana kisha akamualika kwenye harusi yake ambayo ingefanyika siku nne mbele.
” Ticha wangu ulikuwa ujaoa Yakhe!.
Seid alimuuliza kwa mshangao, baada ya kuambiwa anaalikwa kwenye harusi.
” Aaaaaah nlikuwa bado bhana, sasa hivi ndio nachukua jiko.
” Aissee hongera sana ticha wangu, mpemba, wa bara au wa hapa hapa unguja.
” Huyu bhana wa unguja hapa hapa.
” Basi hapo najua mambo mazuri, Ikifika Ramadhani mambo ya vireja, na keki keki hazikosekani.
Ticha alicheka sana aliposikia hivyo, mwisho wa kicheko akamilizia na maneno,
” Hamna bhana ,, !
” Itakuwa jumaa mosi?, aliuliza seid
” Hapana ni ijumaa jioni. Nataka nifate sunna za ukoo wetu..
” Rusha roho la nguvu la kukesha au itakuwa mwendo wa madufu?..
” Yani hilo la kutosha baada ya harusi mimi nitakuwa ndani nakula vitu nje mnaendeleza.
” Hahahaaaaaa aya mwalimu wangu nitakuja asubuhi na mapema japo imekuwa ghafla.
” Hapana si ghafla, watu wengi washajua hilo ila wewe nilijua hata nikikutaarifu siku yenyewe hutokosa kuja.
” Kweli, kweli kabisa mwalimu wangu.
Waliagana ticha akakata cm Seid akiwa anacheka, aliangalia screen ya cm kisha akaiweka pembeni, mama yake Bi Najma akamuuliza.
” vipi mbona furaha?. Seid alimgeukia akamjibu.
” si unamkumbuka yule Ticha aliekuja na Hamad nikakuambia amepigwa Risasi?.
” Ehe!
” Anaoa Ijumaa..
” Mashallaah! Mungu amuongoze jamani!.
” Aameen!, Seid aliitikia akiweka sawa baadhi ya mambo kwenye laptop.
Alifungua upande wa email ili amchek rafiki yake hamad kama yuko online amtumie ujumbe mfupi, bahati nzuri alimuona yuko online akaingia upande wa kuandaka message.”Una taarifa kuwa Ticha anaoa ijumaa?
alipomaliza kuandika aliutuma, akatoka upande wa email akaingia upande mwengine huku akiongea na mama yake.
” Mwanangu unapenda Sana Raha Mashallah, hiyo laptop utafikiri ulikuwa nayo miaka mingi na maji yako pembeni mwenyewe. Aliongea baada ya kumuangalia mwanae kwa muda mrefu anavyochezea mashine..
” ndio maana mama niliwahi kukuambia kuwa mimi sio mtu mwenye hadhi ya shida, Shida nimezipata bahati mbaya tu mimi.
Message kutoka kwenye email iliingia.
Aliifungua na kuiangalia. ” Nilikuwa sina habari hizo ila kanipigia sasa hivi na kunambia kuhusu hilo.
(Repley >> ” Hata mimi kanipigia muda huu kunipa hizo habari, vipi!?, sisi ndio watu wake wa karibu, na Shary yule mhindi anasema katika kitabu chake, Kwenda kwenye ndoa ya mtu unae mjua bila zawadi yoyote ni sawa na kinyonga kubadilisha rangi mbele ya mtu mjinga >> Send.
” Mama vipi umepitiwa na usingizi.
Alimuuliza mama yake baada ya kujibu ujumbe wa Hamad, alivyoona hajajibiwa aligeuka nyuma na kukuta tayari mama yake kalala zamani.
Alimuangalia sekunde kadhaa, aliporudisha macho yake kwenye screen tayari alikuta ujumbe akaufungua na kuusoma. >> “Hahahahaaaa naomba unambie hayo maneno yako katika kitabu gani nimekisahau, ikifika hiyo siku wewe njoo tu mjini mambo yote tutayamalizia huku na tutaingia katika harusi yake kama wafalme.
Seid roho yake ilisuuzika aliposoma maneno ya rafiki yake, hakupoteza muda akaripley. << Wao Niko na furaha sana kusikia hivyo, ndio maana nasema wewe ni zaidi ya rafiki kwangu, hayo maneno yanapatikana katika kitabu cha “SHARK SHARQ” mwandishi na mtunzi ni Sharq Muzdeil mwenyewe, humo kuna vitu vizuri hata huyo william mwenyewe haoni ndani.
Akiwa anamaliza kuandika alama nyekundu ilionekana pembeni ya Laptop akajua charj inataka kuisha, na umeme ulikuwa umekatika muda huo, aliisend haraka akafunga laptop na kuanza kufanya mambo mengine ambayo yalibidi wakati huo..
Asubuhi na Mapema ya siku ya Ijumaa alijiandaa pamoja na mama yake kwa ajili ya kwenda kwenye harusi ya Ticha, Ticha alimuomba sana aende na mama yake ili nae kumpa heshima kwenye harusi, Mpaka kufika saa mbili na nusu walikuwa tayari wako mjini, ambapo walipata mawasiliano ya haraka kutoka kwa Ticha baada ya kufika, Seid aliwasiliana na Rafiki yake Hamad ili wakutane, Mama seid alipanda gari nyingine kwenda kuungana na wakina mama wenzake nyumbani kwa bwana harusi kwa ajili ya maandalizi ya vyakula, akiwa tayari amepata kuelekezwa sehemu yenyewe na kutumiwa watu wa kumfata endapo atafika sehemu husika.
Hamad alimfata seid darajani haraka baada ya kupigiwa cm na kuambiwa tayari ashafika, walipokuwa tayari wameonana walikumbatiana kisha wakaanza kutembea kuingia ndani ndani town sehemu zinapouzwa zawadi za harusi, Walinunua vitu kadhaa vya thamani ili kupeleka kama zawadi kwa Ticha, Huku Hamad akitumia tena kiasi cha laki moja na nusu kumnunulia Suti moja matata sana Seid ambayo ilikuwa ikifanana na ya kwake, Ili wakiingia kwenye harusi waweke utofauti wa watu wengine, na watu wajue kuwa kweli hawa ni mabest wa huyu jamaa.
Harusi ilikiwa inaanza saa kumi kamili, waliitaji kutumia muda mfupi uliokuwa umebakia kuhakikisha wanajiandaa vilivyo, walisaidiana kulipamba gari aina ya Suzuki grand Vitara alilokuwa anapenda kutumia hamad kuhakikisha linapendeza, kwani walitakiwa kuongozana na magari matatu ya watu muhimu ambayo yatakuwa yanatoka kumchukua bibi harusi na kumpeleka nyumbani kwa bwana ambapo kuna harusi yenyewe.
Ilipofika muda wa saa saba tayari kila kitu kilishakamilika, Ticha alikuwa ni mtu wa kupiga cm kila wakati kwa kina Hamad ili wawahi, Wazazi wote wa Hamad nao walishaenda kwenye shuguli hiyo ambayo tayari ilishaanza, Seid na hamad walijiandaa kwa ajili ya kwenda mbweni sehemu anayotoka bibi harusi, ili kuungana na msafara utaokuwa umemchukua bibi kumpeleka mchina mwanzo.
Hamad na Seid walivalia na kupendeza wakiwa nyumbani anakoishi hamad, Seid ni kama mtu aliekuwa amezaliwa upya kwa jinsi suti ilivyompendeza na kumfanya ang’ae, Hamad alijikuta akimwambia ,, “Ndugu yangu wewe ni Hand some shida tu ndio zinakufanya uonekane mwanaume wa kawaida. Alienda kwenye kioo kikubwa kilichokuwa chumbani kwa hamad na kujitazama, Yeye mwenyewe alijishangaa namna alivyopendeza, huku akikumbuka msemo usemo “Shida zitakufanya ufanane na nyani hata kama sura yako nzuri zaid ya tunda la apple.
Walitoka nje wote wakiwa ndani ya Suti zenye rangi tofauti tofauti za kung’aa, walifungua gari wakaingia ndani na kuanza safari ya kuelekea Mbweni.
Hamad upara wake aliutia mafuta ya kutosha kiasi cha kumeremeta, walikanyaga mafuta mpaka mbweni ambapo waliwakuta watu tayari wakiwa wamejiandaa, Salam za hapa na pale zilipita, Masheikh waliotakiwa kusimamia ndoa tayari nao walikuwa eneo hilo, Mabasi zaid ya manne yalishaajaza watu kwa ajili ya kumsindikiza mwari wao, huku ngoma aina ya madufu yakipigwa, yaliyoambatana na nyimbo au Qaswida za harusi.
Bibi harusi alikuwa ni binti wa kizanzibar mwenye umri wa miaka 22 aitwae Rahma, tayari akiwa ndani kwao alishaandaliwa na kupewa mafunzo yote ya kwenda kwa mume, machozi yalikuwa yakimtoka pindi alipowaza maisha mapya ya ndoa yake na kuyaacha maisha ya nyumbani aliyoyazoea.
Taratibu walimtoa nje kumpeleka kwenye gari ambalo lilikuwa na mandhari nzuri ya kifahari, aliingia ndani watu wakiwa wanapiga vigele gele huku nyimbo za “ai yaya kuolewa utarudi nyumbani kutembea zikiendelea kwa baadhi ya marafiki zake waliokuwa wakimfaham, na majirani waliokuwa wameizunguka nyumba hiyo, Wengine wakitoa machozi ya furaha kumuona mwenzao kapata mwanaume wa kumuoa mara tu alipofeli, huku kukiwa na mirindimo ya watoto na wasichana wadogo wadogo waliokuwa wakiendelea kupiga ngoma ngoma zilizosababisha tafrani.
Baba yake hakuweza kuudhuria harusi hiyo kwa sababu alikuwa nje ya nchi kimajukumu ya kazi japo tayari alishatoa baraka, ni mama yake na ndugu zake wengine tu waliokuwepo kwenye shuguli hiyo mpaka Rahma anaolewa.
Rafiki yake kipenzi aitwae Raya ndio alikuwa amekaa nae kwenye gari aliloingiamo kwenda kwa mumewe mtarajiwa, hakuitaji kukaa na mtu mwengine wala kusimamiwa na yoyote zaid ya rafiki yake huyo, ambae walikuwa wakisoma wote kidato cha sita shule moja darasa moja ila yeye akafeli na rafiki yake akapita kuendelea na chuo.
Walikuwa wameshibana zaid ya mapacha wawili, wakiwa ndani ya gari ni machozi tu yalikuwa yakiwatoka, Rahma akilia juu ya maisha yake mapya ya kwenye ndoa, Raya akilia kukaa mbali na rafiki yake huyo aliemzoea.
” Rahma, Huna haja ya kulia sana, Kwani yote ni mipango ya Mungu, ila mimi ndie napaswa kulia zaid ya sana kutokana na machungu niliyo nayo, Kwanza naingia chuo rafiki yangu niliekuzoea ukiwa haupo, pili kutumia muda mwingi kuwa mbali na wewe kitu ambacho itanichukua muda kukizoea, Ila mimi nakutakia maisha mema ya ndoa yako, nina amini Mungu atailinda na kuiweka mbali na mitihani ya kila mara, nakupenda sana my real friend, my Mchumba, my Husband, my mpenzi, my Every think kiukweli naumia sana Rahma.
Raya aliongea huku akilia kwa rafiki yake, Dereva alishangaa kusikia watu nyuma wakiitana my mchumba my husband, alitoa macho na kuachia tabasam, aliekuwa pembeni yake akamwambia “mambo ya watoto wa kike hayo achana nayo.
Baada ya kufika kwenye harusi yenyewe ambako kulikuwa na maandalizi yote, Gari zilipaki sehemu husika za kupakia magari, Seid na Hamad ndio walikuwa wa kwanza kushuka kwenye gari lao, kisha wakaenda kufungua milango ya gari alilokuwa amepanda bibi harusi na Raya, makofi ya taratibu yalipigwa kutokana na wale wa uswazi uswazi wote kuishia nje kidogo ya shuguli, Bibi harusi alishuka pamoja na Raya, kisha milango yote ya gari ikafungwa.
Kipindi Raya anapiga hatua nyuma ya bibi harusi huku umati wa watu ukiwa unapiga makofi, kwa bahati mbaya alikanya gauni lake refu akaanguka chini, Upepo kidogo ulikuwa unapiga muda huo, gauni lote lilipanda juu surual ya jinzi aliyokuwa ameivalia ndani ndio ikawa imemnusuru kumwaga radhi mbele ya umati wa watu, huku baadhi ya watu wakianza kutoa macho na maneno ya mshangao kwa kitu wanachokiona.
Itaendelea sehemu ya 14