MBINU ZA KUMFURAHISHA MUWAPO FARAGHA-2 - RAHA ZA KITANDANI

MBINU ZA KUMFURAHISHA MUWAPO FARAGHA-2

Nilikueleza kwamba unapotaka kumfurahisha mwenzi wako muwapo faragha, ni lazima maandalizi yaanze kufanyika mapema. Nilikueleza umuhimu wa kuhakikisha mna maelewano mazuri na mwenzi wako, mnazungumza kwa maelewano, mnacheka na kufurahi na kuweka kando tofauti zenu kabla ya kukutana faragha.

Nilikueleza pia kwamba unapokuwa faragha hutakiwi kuwa na papara na hii inawahusu zaidi wanaume. Upo usemi wa wahenga kwamba mkamia maji hayanywi! Ukifuatilia kwa kina utagundua kwamba wengi kati ya wale wenye matatizo ya kucheza dakika mbili na kufika kileleni, wanakuwa wamekamia sana mchezo namatokeo yake wanashindwa kuwafikisha wenzi waop pale panapostahili.

Kukutana faragha kwa watu wanaopendana halitakiwi kuwa jambo la dakika mbili tatu basi kila kitu kimefika mwisho. Lazima yafanyike maandalizi ya kutosha, muandae mwenzi wako taratibu na kama nilivyosema, muda ambao unashauriwa kitaalamu ni angalau dakika thelathini.
Kubwa zaidi, baada ya kufanya yote hayo niliyoyaeleza hapo juu, unapofika muda wa kazi, hutakiwi kuwa mbinafsi. Raha ya ngoma ucheze na mwenzako, kwa hiyo badala ya wewe kujifikiria wewe tu, kwamba cha msingi ni wewe kufurahi ni vizuri ukamfikiria na mwenzi wako pia.

Wapo wanaoamini kwamba mchezaji mzuri ni yule anayetumia mabavu uwanjani! Hapana, mapenzi hayapo hivyo, ubunifu pekee unaweza kumfanya mwenzi wako akalia chozi la raha. Cha msingi ni kujua namna ya kwenda sawa na hisia zake, kujua maeneo yenye udhaifu na kuyatumia ipasavyo. Jitahidi kuyajua mambo yanayomfurahisha muwapo faragha na ukiona unashindwa kuyagundua mwenyewe, si vibaya kumuuliza anapenda kufanyiwa nini, akikueleza kifanye kile alichokwambia kwa ukamilifu.


Ukifani-kiwa kufanya yale anayo-yapenda, hakuna wasiwasi kwamba lazima atafika kwenye kilele cha furaha na atazidi kukupenda mpaka mwenyewe utashangaa. Baada ya kazi nzito, mpe pole, mshukuru, mbembe-leze na mwambie maneno matamu yatakayo-ufurahisha moyo wake kisha baada ya hapo, pumzikeni mkiwa pamoja.
Image result for couples happy on bed
Wasichokijua wengi ni kwamba kitendo cha kukumbatiana huwa kinaongeza ukaribu na hisia za mapenzi kati yenu kuliko kawaida, kwa hiyo usiogope, mkumbatie kwa hisia na endeleeni na mazungumzo ya chini ya mto.

Kama mnao muda wa kutosha, utashangaa baada ya muda, kila mmoja anaanza kumhitaji tena mwenzake na mambo yataendelea kuwa mazuri kwenu wote wawili, kila mtu atafurahi na ile tafsiri halisi ya mapenzi ya dhati itajionesha waziwasi.

Ukiwa mtu wa aina hii, mwenzi wako hawezi kuchoka kukaa na wewe, hujawahi kuona watu wanaopendana ambao wanaweza kutwa nzima wakashinda ndani wakiwa wenyewe tu? Si kwamba muda wote wapo faragha, hapana! Mazingira wanayoishi pamoja yanamfanya kila mmoja kutamani muda wote awe karibu na mwenzake.

Hata utakapotoka kwenda kazini kwenye shughuli zako nyingine, atakuwa anakumisi na wala hutahitaji kumlazimisha akupigie simu mara kwa mara kukujulia hali, yeye mwenyewe atayafanya hayo tena kwa moyo mkunjufu kabisa na mtayafurahia sana mapenzi yenu.Jambo kubwa na la msingi, unapopata muda wa kuwa naye faragha, hebu achana na mambo mengine yote, achana na simu au sijui tamthiliya kwenye TV, huo ni muda wake, mtendee haki kwa kumpa nafasi yake.