JE VIPIMO VYA UKIMWI VINASOMA BAADA YA MUDA GANI WA MAAMBUKIZI? - RAHA ZA KITANDANI

JE VIPIMO VYA UKIMWI VINASOMA BAADA YA MUDA GANI WA MAAMBUKIZI?



watu wengi hua na wasiwasi sana baada ya kulala na watu ambao tayari ni waathirika au kulala na watu ambao wanashutumiwa kwamba wameathirika...wengi wao huchangachikiwa na kutaka kupima siku hiyohiyo kujua kama wameambukizwa au vipi.
kimsingi vipimo vya ukimwi huanza kusoma positive[umeathirika] au negative[haujaathirika] kwanzia siku ya kumi mpaka miezi mitatu kulingana na kipimo kilichotumika na kinga ya mwili wa muhusika.
hivyo hata kama umeathirika tayari huwezi kujua mpaka muda fulani upite na kipindi hiki ambacho bado vipimo vitaonyesha huna, utakua na uwezo wa kuwaambukiza watu ambao sio waathirika, lakini pia kama ukitembea na mtu leo na ukaenda kupima leoleo ukajikuta ni muathirika basi virusi hivyo haukuvipata kutoka kwa mtu huyo wa siku hiyo.
vipimo mbalimbali huonyesha majibu kulingana na uwezo wake kama ifuatavyo...
rapid antibody test; hichi ni kipimo ambacho kinatumika mara nyingi kwenye vituo vyetu hapa tanzania mfano wa vipimo hivyo ni sd bioline, determine na unigold..kipimo hiki hupima askari wa mwili kitaalamu kama antibody ambao hutengenezwa na mwili kupambana na virusi vya ukimwi, mwili ambao haujaathirika hauwezi kutengeneza askari hawa.
wiki ya 4 mpaka wiki ya 6 watu wengi walioambukizwa huweza kugunduliwa kwa vipimo hivi japokua sio wote.
wiki ya 12 baada ya maambukizi zaidi ya asilimia 98 ya walioambukizwa watakua tayari wanaonyesha kwa kipimo hichi.

rapid antigen/antibody combination test; hichi ni kipimo ambacho kinagundua vimelea vya virusi vya ukimwi kitaalamu kama antigen na kugundua pia askari wanaotengenezwa na mwili kuulinda kupambana na ukimwi kitaalamu kama antibody.
siku ya 12 mpaka ya 26 vimelea hivi au antigen huweza kugundulika kwa kipimo hichi, siku ya 20 mpaka 25 askari wanaopambana na virusi hivi au antibody huweza kugundulika pia.[vipimo hivi havipatikani hapa kwetu na havipatikani kwenye hospitali zetu wala maduka ya madawa]
                                                        


rna test; vipimo hivi vinaona virusi moja kwa moja na vinatoa majibu kwa uhakika sana, kuliko nilivyotaja hapo juu...havipatikani sehemu nyingi sana duniani kwani ni gharama sana na vina uwezo wa kugundua muathirika siku ya 10 mpaka 14 baada ya kuambukizwa.
                                                            

polymerase chain reaction[pcr]; hichi kipimo pia hupima virusi moja kwa moja, hapa nchini kwetu vinatumika kupima kiasi cha virusi kwa waathirika kitaalamu kama viral load, kupima watoto waliozaliwa na mama muathirika kama wameambukizwa.
kipimo hichi husoma wiki ya 2 mpaka ya 3 baada ya maambukizi na hupatikana kwenye hospitali za rufaa tu hapa tanzania kama muhimbili, mbeya, kcmc na bugando...
                                                                      


mwisho; kujipima virusi vya ukimwi nyumbani kwa sheria za nchini kwetu ni kosa, kwani unaweza ukapata majibu mabaya bila kuandaliwa kisaikolojia kwa ushauri kwanza au unaweza ukapima vibaya ikaonekana umeathirika kumbe hujaathirika hivyo kama unataka kujua hali ya afya yako basi nenda ukapime kwenye vituo husika.