Mambo Ya Muhimu Kuyafahamu Katika Safari Yako Ya Maisha. - RAHA ZA KITANDANI

Mambo Ya Muhimu Kuyafahamu Katika Safari Yako Ya Maisha.



Mwanadamu katika safari yake ya maisha kuna elimu muhimu ambazo akizitambua na kuweza kuziishi itamsaidia kuongeza nguvu yake ya kiroho, kiimani na kuweza kuifurahia safari yake ya maisha. Unaweza ukawa haujui elimu hizo kutokana na huwezi kufundishwa shuleni kuhusiana na elimu hizo au kwa sababu wazazi wako hawajaweza kuzifahamu inapelekea na wewe usifahamu kwani tunajifunza dunia ilivyo kupitia waliotutangulia, milango ya ufahamu na intuition yetu.

Tangu miaka ya zamani wanadamu wamekuwa ni watafutaji wa mambo yaliyojificha katika maisha. Tambua kuwa safari ya maisha lengo lake ni kutufundisha na kuimarisha roho zetu.



 
Elimu hizo za muhimu ambazo ni elimu zinazoweza kukusaidia kuelewa siri za ulimwengu na mambo ambayo wanadamu wachache wameweza kuzitambua. Lakini tambua kuwa, kama unajua elimu hizo au kama haujui elimu na laws zake bado zitakuwepo tu. Mfano ukiruka kwenye gorofa hata kama hujui kuwa kuna nguvu ya mvutano (gravity) utatua tu chini na kuumia. Ni sawa na elimu hizi. Uwe unazijua au usipozijua bado zinafanya kazi kila wakati. Hivyo ni muhimu kuzijua ili uweze kuziongoza na kubadili maisha yako. Nazo ni


  • Elimu ya kutambua jinsi akili inavyofanya kazi (mind). Ufahamu ni kitu cha upekee duniani kwani ndio daraja lako na The Great Creator (The Universe/God) na ndipo chemchem ya mawazo inapoanzia. Mwanadamu anayeweza kujifunza jinsi akili ya inavyofanya kazi anaweza kujua mengi ya siri ambayo watu wengi wamelala na hawatambui chochote bali wanaishi kwama jamii walivyoikuta na hawana akili ya kufikiria zaidi ya wanayoyajua.

http://thirdeyeactivation.com/wp-content/uploads/2011/11/spirit-mind.jpg



  • ·   Elimu ya kutambua kuwa kila kitu duniani ni energy. Kila uonacho duniani ni material au vitu ambavyo ukivitazama ndani zaidi (mfano kuvikuza katika darubini kali). Energy hiyo inatetemeka (ina vibrate) katika styles tofauti tofauti na katika waves tofauti tofauti na ndio maana unaona vitu vinatofautiana. Mfano mbao imetengenezwa na Carbon, lakini ukiiview Carbon kiundani zaidi utaona Carbon imetengenezwa na chembechembe tofauti za energy. Hivyo kila kitu ni energy na hakipo kama macho yanavyotafsiri.
 

  • Kutambua nguvu ya mawazo (thoughts). Unaweza ukawa unadharau kuwa mawazo ni kitu cha kawaida lakini amini kuwa mawazo au wazo lolote kichwani ni energy na unaumba kupitia mawazo ukichanganya na hisia juu ya mawazo hayo. Kila kitu hapo kale kilikuwa na wazo. Tazama kila kitu kinachokuzunguka utaona kuwa kila kitu kilikuwa wazo hapo mwanzo halafu uumbaji wake ukafuatia. Mfano dirisha au mlango, hapo kale kabla ya dirisha lilikuwa ni wazo la kitu kama dirisha ndipo wazo lile likatendewa kazi na kutokea katika dunia ya kifizikia. Mfano mwingine ni Computer, Tv, au kila kitu alichotengeneza mwanadamu kabla ya kuwa kitu lilikuwa ni wazo na likafanyiwa plan then likatokea. Hivyo utagundua kuwa miaka ijayo mambo mapya yataendelea kuwepo kwani mawazo yapo kwa baadhi ya wanadamu hivi sasa na wanadamu wachache wanaweza kuhamisha mawazo kutoka kwenye conscious mind kwenda kwenye subconscious mind (The Mind of Inteligence, The Provider). Hivyo kila wazo lililopo kichwani either baya au zuri tambua kuwa linaweza likaumba.

  • Elimu ya nguvu za Imani, conscious mind na subconscious mind. Imani ni daraja linalounganisha wazo/tamaa/desire/thoughts na Subconscious Mind. Kwa kifupi akili imegawanyika pande mbili. Conscious na Subconscious.


Kazi ya Conscious mind ni kutumia milango ya ufahamu kama macho, masikio, pua n.k kuisoma dunia inayotuzunguka, pia ndio sehemu wanadamu wengi hutumia katika maisha yao. Ni asilimia 7% ya ufahamu/mind. Sehemu hii inahukumu vitu kutokana na imani na milango ya ufahamu Haiwezi kufikiria zaidi ya hapo. Sehemu ya puli ni Subconscious mind. Hii ndio sehemu kubwa ya ubongo na ndipo maajabu yalipo. Ni sehemu ambayo inasimamia kazi za mwili kama kiasi cha sukari mwilini, mapigo ya moyo, pumzi na vitendo ambavyo wewe mwanadamu hujui kuongoza. Pia ndio sehemu inayosaidia ukiwa na hatari ikishirikiana na homoni. Sehemu hii haitambui wakati, haijui kama jambo ni la kweli au la.


Ukiamini jambo katika ubongo wako wa conscious mind moja kwa moja jambo hilo linaamia kwenye subconscious mind na kuumba jambo hilo (kukufanya uone ni kweli). Sehemu hii haijui mema wala mabaya, ukweli wala uongo na haijuhukumu unachoamini bali inatekeleza na kukufanya uamini ni kweli. Yapo mengi wanadamu wanaamini lakini hawajui kuwa mambo hayo hayapo bali imani yao ndio imewaumbia mambo hayo.




·          

  • Ufahamu wa kuwa mwanadamu anaweza kuishi bila kuteseka kabisa (enlightenment). Walimu wa imani kama vile Buddha, Yesu, Krishna, Shiva, Haile Selassie, Osho, Lao Tsu n.k ambao waliweza kupata enlightenment (kufunuliwa) wamekuwa wakiongea ujumbe mmoja kuwa wanadamu wamelala. Ni kwa maana kuwa lengo la safari ya maisha ni kujitambua, kutambua your power withing, God Realization, na kuweza kufunuliwa jicho la tatu utagundua kuwa mwanadamu ana nguvu kubwa sana lakini amelala. Ili uweze kufunguka jicho la tatu lazima ujifunze meditation, kutawala akili yako, kuvuta nguvu za kundalini/chakra na kuishi katika njia sahihi na ya haki. (Hii ni mada ndefu na ni ngumu sana kumuelekeza mtu kwa mara ya kwanza).