Je Mwanamke Unafahamu Jinsi ya Kudumisha Penzi Kwa Mumeo na Kumkamata Kisawa Sawa ? - RAHA ZA KITANDANI

Je Mwanamke Unafahamu Jinsi ya Kudumisha Penzi Kwa Mumeo na Kumkamata Kisawa Sawa ?

Mwanaume ameumbwa kumsikiliza mwanamke, niwazi kuwa mwanamke muwazi kwa mwanaume muelewa huwa na furaha sana kwenye mahusiano yake. Japo kihulka mwanaume ameumbwa na tamaa hasa za kimwili lakini uwezekano wa kumdhibiti mwanaume ni mkubwa hasa endapo mwanamke utaweza kuyafanyia kazi mambo kadhaa ambayo ni muhimu katika kulitunza na kulikuza penzi lenu.
Wanasema PENZI NI MAUA HUCHANUA NA KUNYAUKA  msemo huu una maana moja fupi tu kuwa mahussiano ya mapenzi hayana tofauti na maua ambayo yanahiyaji matunzo kama kumwagiliwa maji,mbolea na kuhakikisha jua haliyasumbui,vivyo hivyo kwenye mapenzi kunahitaji malezi,matunzo flani ambayo yatalistawisha penzi na kuliacha likichanua kila wakati.



Mwanamke kama utahitaji kumuweka mwanaume wako kwenye himaya yako na awe wako wa kudumu fanya yafuatayo

i) Hakikisha unakuwa karibu na mumeo.
Ukaribu huu ni khakikisha mara zote mumeo anapokuwa maeneo yasiyo ya kazi basi unapata muda wa kuzungumza naye,kukumbushana baadhi ya mambo mliyopitia au hata kupangilia yajayo.
Pata muda wa kutosha kuzungumza na mumeo kutamfanya asikuchoke na akuone muhimu kila wakati. Mfanye mumeo kuwa rafiki anayezijua shida zako na wewe kuzijua shida zake. 

ii) Mumeo akirudi kutoka safarini au kazini mupokee kwa mabusu na upendo wa hali ya juu.
POLE ni neno muhimu sana katika mapenzi huleta hamasa na kuonesha kujali. Mume hana tofauti na mtoto anahitaji kujiona kama anaye mtu anayemjali ukiacha wazazi wake, nafasi hii ni muhimu sana sana na ukiitumia vizuri basi sio rahisi mwanaume wako akawa na michepuko.

iii) Kama utakuwa na nafasi jitahidi kumuandikia msg mumeo za upendo na kumfariji.

iv) Na mwisho kumbuka kuwa munapokuwa katika sita kwa sita jitahidi kutoa sauti ya mahaba huku ukijitahidi sana kumpa penzi kutumia ujanja wako, na kama atamaliza mwambie "POLE MUME WANGU".

Kwa leo ninakomea hapo kumbuka kuwa wanaume ni watu wa kujaliwa kila wakati na kubembelezwa Mwanasaikolojia wa mapenzi Dr. Linda wa chuo kikuuu cha Oxford aliwahi kunena ya kwamba hakuna dawa ya mapenzi zaidi ya kuonyesha upendo kwa umpendae.

#Share Post Hii na Marafiki Pia.